Je! Mungu ni yule yule?

Kuna watu hawaamini Mungu yupo na hawataki kuwafanyia wengine mabaya.

Na kuna magaidi wanaua watu kibao kwa kutumia jina la Mungu.

Ukiwa unaogopa kufanya mabaya kwa kumuogopa Mungu, wewe wema wako unatokana na uoga. Huna wema wa asili ya kwako mwenyewe.

Ukifanya wema wakati unajua hakuna Mungu, mbingu wala pepo, umefanya wema kwa kutaka tu kwa sababu wewe mtu una asili na akili ya kupenda mema, wema wako ni wa asili kwako mwenyewe.

Anayefanya wema kwa kumuogooa Mungu na kutaka pepo anafanya wema wa biashara. Anafanya wema ili apate faida ya kupata pepo na kuepuka moto.


Anayefanya wema huku anajua hakuna Mungu, pepo wala mbingu, anafanya mema kwa asili yake.

Niko na waamini Mungu kibao katika kundi moja. Mwenzetu ameumwa mpaka anataka kufa. Watu wanajibalaguza. Mimi nisiyeamini Mungu nikawa wa kwanza kutoa msaada.

Wanaoamini Mungu wamebaki kuwa wanaamini kwa jina tu.

Mtu asiyeamini Mungu ndiye katokea kufanya kama anayeamini Mungu anavyotakiwa kufanya.

Kwa hiyo usikariri tu kwamba kutoamini Mungu ni kufanya mabaya na kuamini Mungu ni kufanya mazuri.

Mimi kutoamini Mungu kunanichochea kufanya mazuri zaidi.

Ningeamini Mungu ningeweza kukuta mtu anaumwa anataka kufa nikasema ni kazi ya Mungu, tumuombee tu. Nikasepa. Au nikasema huyu Mungu anamuadhibu.

Lakini sasa hivi siamini Mungu nikiona mtu anaumwa, nasema hakuna Mungu wa kumsaidia. Ni wajibu wangu mtu mwenzake nimsaidie maana hakuna Mungu.
 
Kuwepo kwa maovu duniani hakuonyeshi kuwa Mungu hayupo.
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, uoendo wote, kama mnavyomsema, kama yupo, pale alipoanza kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi yanayoua kwa kuzuka hai watoto wachanga hayawezekani kuwepo katika ulimwengu wake.

Hapa usiseme habari za shetani, dhambi etc. Hayo yote ni mambo ambayo, kwa mujibu wenu, yamekuja baadaye. Mwanzo Mungu alikuwa na uamuzi yawepo au yasiwepo.

Hakuumba ulimwengu huo ambao matetemeko hayo hayawezekani.

Ilikuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu unaoruhusu matetemeko haya, wakati alikuwa na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao matetemeko haya hayawezekani?

Hujajibu swali hili.
 
Hujanijibu swali langu kwanza, je unaamini kuwa dunia iliumbwa na Mwenyezi Mungu?
 
Hujanijibu swali langu kwanza, je unaamini kuwa dunia iliumbwa na Mwenyezi Mungu?
Kwa nini niamini hivyo? Kwa nini nithamini kuamini katika ulimwengu unaotaka kujua?

Kwa nini niamini contradiction?

Kwa nini niamini kuna pembetatu yenye pembe sita?

Hujaondoa contradiction katika idea ya kuwepo kwa Mungu wako.
 
Kwanini iwe vile utakavyo wewe?
Sijaongelea chochote kuhusu nitakavyo mimi.

Nimeongelea logical consistency.

Non self contradicting.

Dhana ya Mungu isiyojipinga yenyewe.

Unaelewa naongelea nini?

Nakwambia dhana ya Mungubwenu kuwepo inajipinga yenyewe kabla sijaipinga.

Wewe unasema nataka ninavyotaka mimi.

Huelewi contradictiin ni nini. Huelewi logical consistency ni nini.

Huelewi hata wewe unavyouliza unatymia logical consistency, otherwise kusingekuwa na swali.

Ndiyo maana kuekewana vigumu.

Unaelewa contradiction ni nini? Unaelewa logical consistency ni nini?
 
Bila shaka wewe sio binadamu ni agent wa shetani.
 
Rafiki yangu kiranga sasa umewezaje kutambua mema na mabaya
 
Rafiki yangu kiranga sasa umewezaje kutambua mema na mabaya
Sasa nambie brother kama mtu ataamua kutembea na mzazi wake akatembea na wanawe hakuna dhambi yoyoye hapo maana mungu wakuandika dhambi hayupo au unasemaje
 
kwanin alipe kisasi,kwani asipolipa kisasi yeye inampunguzia nin?
 
we jamaa una uwezo mdogo sana wa kufikiri asee
kwa hiyo wanaotembea na watoto wao wamekuwaje kwani?wanao ua kila siku kama hawajakamatwa na serikali wamefanyaje kwani,yaan hayo maelezo yako yana prove vipi uwepo wa huyo mungu
 
Kwa nini niamini hivyo? Kwa nini nithamini kuamini katika ulimwengu unaotaka kujua?

Kwa nini niamini contradiction?

Kwa nini niamini kuna pembetatu yenye pembe sita?

Hujaondoa contradiction katika idea ya kuwepo kwa Mungu wako.
Na ndiyo maana haya mabishano huwa hayana mwisho kwa sababu kama hizo,hauoni sababu ya kuamini au tuseme hautaki kuamini ila hapo hapo unajadili suala la uwepo wa mungu. Ni sawa na kutaka kuongea na mtu ila umezipa masikio usisikie.

Ikiwa hauoni umuhimu wa kuamini sijui ni vp mtu atakueleza imani ya uwepo wa mungu na mkaelewana?
 
Rafiki yangu kiranga sasa umewezaje kutambua mema na mabaya
Mengine ni kwa mantiki na utu bora tu.

Kwa mfano, sitaki kumfanyia mtu kile ambacho mimi sitaki kufanyiwa. Pia, napenda kutoa msaada ule ambao mimi ningependa kusaidiwa.

Kanuni hii, pamoja na nyingine nyingi secular kama hii zinanifanya niweze kufanya mazuri mengi na kuepuka mabaya mengi bila kuamini Mungu wala mtume yeyote.

Kwa kweli, imani ya Mungu inaweza kupalilia mengi mazuri. Mambo kama sadaka za kusaidia masikini, upendo etc ni mazuri. Lakini mimi naona kitu kizuri kilichojengwa kwa msingi wa uongo kinaingia ubaya wa uongo wa msingi. Pia, dini inapalilia mengi mabaya kama ubaguzi, kujiona Mungu wako ndiye wa kweli, mpaka mauaji na mabaya mengine yanayofanywa kwa jina la dini.

Nitatumia mfano wa dini kubwa kwetu huko. Uislamu na Ukristo. Ukiwa Mkristo unaambiwa hakuna atakayeiona pepo bila kupitia kwa Yesu. Maana yake dini zote zisizomtambua Yesu kama Mungu ni za uongo.

Ukienda kwa Waislamu wasio Waislamu wanaonekana makafiri na kuna mpaka aya za kuhalalisha kuwaua kwenye vita takatifu.

Mimi sitaki kujiweka katika mafungu haya kwa sababu naamini watu wote wana uwezo wa kuungana pamoja bila ubaguzi na kuishi kwa utu bora wakipewa nafasi nzuri ya kustawisha elimu yao ya falsafa na maadili. Na hata wakishindwa katika kuufuata ukweli mgumu, ni bora kuliko kuishi kwa uongo mzuri.

Tatizo watu wengi wanapenda uongo mzuri kuliko ukweli mgumu.

Ukiwaambia watu mvua hazinyeshi sana siku hizi, kuna ukame. Idadi ya watu watakaokimbilia makanisani na misikitini kumuomba Mungu ambaye hayupo ni kubwa sana kuliko idadi ya watu watakaochunguza habari za kukata miti na carbon emissions inavyohusiana na climate change.
 
Sasa nambie brother kama mtu ataamua kutembea na mzazi wake akatembea na wanawe hakuna dhambi yoyoye hapo maana mungu wakuandika dhambi hayupo au unasemaje
Dhambi ni nini?

Mbona mimi nisiyeamini Mungu naona hayo mambo mabaya na kuna Makasisi wa Kikatoliki ma Mashehe wamewafanyia waumini wao ushenzi?

Unaelewa kwamba inawezekana akawepo mtu ambaye haamini Mungu akaikataa hiyo mnayoiita dhambi kuliko hao wanaosema wanaamini Mungu? Kwa kutaka yeye mwenyewe tu, bila ya sababu ya kutaka pepo au kumuogopa Mungu na moto?

Kwangu mimi, mtu anayetenda mema na kukataa mabaya huku haamini Mungu anakuwa amepevuka kimaadili kwa kiwango cha juu sana kuliko yule anayetenda mema na kukataa mabaya kwa sababu ya tamaa ya kwenda peponi na kuogopa moto wa Mungu.

Anayetenda mema bila kumuamini Mungu anaweza kutenda mema bila ya sababu za ubinafsi, kwa utubora tu.

Anayetenda mema kwa tamaa ya pepo na kumuogooa Mungu na moto wake mara zote anakuwa na aina ya ubinafsi. Hatujui akipata uhakika Mungu hayupo na moto haupo valangati lake litakuwaje. Huu umekuwa msingi mkubwa wa watu wanaojua Mungu hayupo lakini ni wasomi wa falsafa na viongozi -wapo wengi sana hawa katika uongozi wa dini na serikali- kutetea habari za Mungu na dini, kwa msingi wa kwamba hata kama si za kweli, zinasaidia kuweka utulivu katika jamii. Mimi naikataa hoja hii kwa sababu utulivu uliojengwa katika uongo si utulivu wa kweli. Ni ulaghai. Kufanya hivi ni kutukana uwezo wa watu wa kufikiri, kwamba watu wanahitaji kulelewa na kuamuliwa kama watoto, hawana uwezo wa kufanya mema bila kutiwa woga wa moto na ahadi za pepo. Kadiri dunia inavyopata elimu zaidi, watu wanaondoka kwenye misingi hii.
 
Sitaki kuamini. Nataka kujua. Kwa muktadha wa mantiki isiyojipinga yenyewe.

Mungu wenu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni wa uongo.

Kwa sababu dhana ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe (self contradicting).

Kumuamini Mungu huyu ni sawa na kuamini uwepo wa "pembetatu yenye pembe sita".

Definition ya hiyo pembe tatu inatuhakikishia kwamba pembetatu hiyo yenye pembe sita haiwezi kuwepo.

Kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe.

Jambo hili la kuwepo Mungu huyu ni wazi kama hivyo.

Unaamini pembe tatu yenye pembe sita, katika one dimensional Euclidean planes, ipo?
 
Na hauwezi kuamini usilolijua,kinachoendelea hapa ni kwamba watu wanajaribu kukujuza kuhusiana na imani ya uwepo wa mungu ila wewe unasema hautaki kuamini.

Na kwa hivyo hamtaelewana maana msingi wa hicho unachotaka kujua umebebwa kwenye imani na wewe hautaki kitu kinachoitwa imani,hivyo ukitala kujua kuhusu uwepo wa mungu basi unapaswa kujua kwanza ya kuwa suala la uwepo wa mungu ni suala lenye kuhitaji
 
Brother ukijitahidi unaweza kua mwanasiasa maana una maneno mengi, brother hoja ya mashekh na makasisi kufanya matendo mabaya ni udhaifu wa kibinaadam kama wafanyavyo binaadam wengine kwasbb na wao wanamatamanio hoja yangu brother no ndogo tu hivi mtu alie ishi kwa kuua na kuwafanyia wenziwe ukatili hana malipo yoyote? Umbake mzazi wako mwanao pia huna malipo yoyote kwa vile mungu hayupo kweli akili yako inaamini ni nothing hakuna lolote wala malipo kwa mtu huyu
 
Brother ukijitahidi unaweza kua mwanasiasa maana una maneno mengi,

Kwa nini unafikiri uanasiasa ni kitu ninachotaka mpaka kuweka jitihada? Unajuaje kwamba sijakimbia kazi za kunifanya niwe mwanasiasa?

Tatizo letu si kwamba maneno mengi, tatizo letu watu wanapoogopa maneno mengi.

Hakuna maendeleo bila maneno mengi, hata kama ni kwa minajili ya kuyachuja tu.

Kwa hiyo usiniambie habari za kujitahidi ili niwe mwanasiasa, nimeanza kutembea corridor za Ikulu on a daily basis tangu niko tumboni mwa mama yangu na mpaka leo kuna mzee wa familia yangu yupo baraza la mawaziri la Magufuli, ningetaka habari za siasa ningekuwa ndani yazo miaka 20 iliyopita. Nimezikimbia.

brother hoja ya mashekh na makasisi kufanya matendo mabaya ni udhaifu wa kibinaadam kama wafanyavyo binaadam wengine kwasbb na wao wanamatamanio

Sasa kama kuna Mungu, muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote, kwa nini kawaumba hao watu akiwa na udhaifu na matamanio, halafu wakianguka kwa sababu ya udhaifu na matamanio aliyowaumba nayo, Mungu huyo awadhibu?

Wwewe mzazi unaweza kumtoboa macho mwanao ashindwe kuona, wakati unaweza usimtoboe akaona, halafu mwanao ashindwe kujua kusoma kwa sababu haoni, halafu umuadhibu kwa sababu hajui kusoma?

Kama baba mtu tu, asiye na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote hawezi kufanya hivi, kufanya hivi ni jambo baya sana, imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote afanye hivyo hivyo?

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu ambao viumbe wake hawawezi kupata udhaifu wala matamanio?


hoja yangu brother no ndogo tu hivi mtu alie ishi kwa kuua na kuwafanyia wenziwe ukatili hana malipo yoyote?

Mbona mahakama zisizo na mfungamano na dini yoyote zinatoa hukumu kwa aliyeua?

Mbona hata jamii inatoa hukumu kwa aliyeua? Mbona Wakomunisti ambao hawakuamini Mungu walitoa hukumu kwa walioua?

Umbake mzazi wako mwanao pia huna malipo yoyote kwa vile mungu hayupo kweli akili yako inaamini ni nothing hakuna lolote wala malipo kwa mtu huyu

Hii ni logical non sequitur. Umeunganisha vitu ambavyo haviunganishiki.

Ukimbaka mwanao sheria za nchi zitakufunga, huhitaji Mungu hapo.

Ukiendekeza hilo hata kisiri mwanao akapata mimba, sheria za asili zitakuhukumu, utapata mtoto ambaye ni mjukuu ambaye ana matatizo ya genetics.

Huhitaji Mungu kushitakiwa kwa kosa hili.

Na wala sielewi kwa nini unashindwa kuelewa kwamba kosa hili lina hukumu zimewekwa kisheria, katika nchi ambayo sheria ni secular, haziongozwi kidini.

Ssa hapo kigumu cha kuelea kipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…