Kiranga.
Maisha kwako ni nini? Kipi kinatambulisha uovu kwako [jambo baya kama wewe unavyoita]
Hata nikikwambia sijui majibu ya maswali haya yote. Hilo halithibitishi Mungu yupo.
Ni kama vile unaniuliza sauare root ya 2 ni nini?
Hata nikisema sijui. Ukiniambia jibu ni 10.
Nitakwambia jibu hilo ni la uongo. Si la kweli. Maana lina cintradiction.
Mungu ana contradiction. Hivyo hata kama sijui maisha ni nini, yalianzaje, jibu la Mungu ni contradiction.
Uovu kwanza kabisa ni hali ya kuleta maumivu, kukosa furaha, ubaya, kitu usichotaka kufanyiwa, bila haki.
Mathalani. Mtu kuuawa bila hatia ni jambo ovu.
Pia, watoto wachanga kufariki inasikitisha sana. Ndiyo maana dunia nzima watu wanafanya jitihada kuzuia vifo, hususan vya watoto wachanga.
Sasa inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, akaumba ulimwengu na kuruhusu matetemeko ya ardhi kwa mfano, yanayoua watoto wachanga na kuwafukia hai?
Huyu Mungu kwa nini mkatili hivi? Hahurumii hata watoto wachanga? Alishindwa nini kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko haya?
Yupo kweli? Au ni wa hadithi tu? Mbona anaachia viumbe wake wapate uchungu sana kwa kuondokewa na ndugu zao?
Imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao maovu na mabaya mengi sana yanawezekana, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Mbona ulimwengu huu tunaouona uko tofauti sana na huyo Mungu anayesemwa? Mbona ulimwengu unampinga? Unam contradict?
Mbona inaonekana huyo Mungu ni kama katungwa kwa hadithi za kitoto ambazo ukizipima kwa logic zinaonekana za uongo?
Hakuna hata mtu mmoja anayesema Mungu yupo ambaye ameweza kujibu swali hili.