Je! Mungu ni yule yule?

Kama umeshindwa kuviweka hapa kwenye hiyo simu yangu ndo utaweza?
Kwanini uone kuwa ni hitimisho kama sio mwisho wako wa kufikiria? Thibitisha tu mkuu hadithi hazitakusaidia chochote
Kwa hiyo wewe umefikiria ukahitimisha kwamba hayupo...?! Jibu la swali uliloniuliza hapo juu jibu ni NDIO...

Sasa unataka nikuthibitishie kwa namna gani...?! Kwa kutumia keyboard..?!
 
"Bora hiyo mi nimeenda dhehebu moja ivi, vikapu vya sadaka mtu anavisimamia pembeni hahaaa chezea"
 
Kwa hiyo wewe umefikiria ukahitimisha kwamba hayupo...?! Jibu la swali uliloniuliza hapo juu jibu ni NDIO...

Sasa unataka nikuthibitishie kwa namna gani...?! Kwa kutumia keyboard..?!
Mimi najua hayupo, sasa wewe unaesema yupo ndo umdhihirishe, kuhusu namna hiyo ni juu yako
 
Mimi najua hayupo, sasa wewe unaesema yupo ndo umdhihirishe, kuhusu namna hiyo ni juu yako
Umewezaje kujua kama hayupo...?!
hebu nipatie njia uliyopitia...?! Mimi namuishi sasa ndio nafikiria namna ya kukudhihirishia wewe, ni sawa sawa na ninapo hisi njaa, nitawezaje kukudhihirishia wewe kwamba nahisi njaa...?! Tena kwa kupitia keyboard...
 
Sasa huyo Mungu wanaemsema wenzio itakuwa sio huyo wako anaeweza kufananishwa na njaa. Wa kwao ana sifa kibao ambazo zote kimsingi hazina uthibitisho kama ambavyo wa kwako pia hana uthibitisho.
Kujua kitu hakipo ni rahisi sana, maana kutokuwepo kwake ndo kunakopelekea wewe ujue kuwa hakipo
 
Kutokuwepo kwake ni aje...?! Wewe unadhani Mungu yupo zizini anaonekana kama wanayama basi usipomuona unasema hayupo...?!

Unazijua sifa za Mungu...?! Sifa yake moja haonekani, halafu yupo mahali pote lakini ni "invisible" yaani unahisi uwepo wake tu...

Kitu kingine imani huwa haiendani na "logic"...
 
Ukiielewa hii process (below) itakusaidia sana

From #Unseen > #Seen >#Unseen > Seen

Kumbuka #Imani ni kuona visivyoonekana kabla havijaonekana.
mkuu hapo umemaliza asipo elewa hapo tena baaasi
 
Sasa hiyo ni imani.....

Imani ni kuwa na hakika na mambo yatarajiwayo.

Mambo ambayo hayapo ila unatarajia yatakuwepo, Kwa maana hiyo basi huyu Mungu hayupo bali mnaamini atakuwepo (rejea maana ya imani)
 
Nani kasema hayapo...?! Nimeshagundua tatizo lako unaelewa kinyume nyume... hebu rudia kusoma hiyo Waebrania 11:1 na kuendelea huone ulichoongea na chako ni tofauti kabisa...

Kitu kingine unaaamini Yesu aliwahi kutokea Duniani...?! Nataka nikupeleke kwa God Incarnate...
 
Siamini vitabu vya hadithi hasa hivyo vinavyoitwa vya Mungu, full contradiction sasa ntaviaminije?
 
ushauri wa haraka haraka

bora uamin Mungu yupo mwisho wa siku hata usipo muona itakua shwari sasa ww unavyosema ayupo siku ukimuona sijui utamwambia nn
 
Jimena hizi ni fact ya kwamba Yesu alitukia hata na kumbukumbu zipo zinaonyesha, fact ni kwamba temple lilikuwepo Jerusalem hata ukienda utapata vithibitisho...

Sasa nashangaa kitu akili yako isipokubali unakiita hadithi... wakati hizo ni fact kabisa na historia zipo za kuthibitisha hilo na sio watu walikaa wakatunga tu...

Hata historia ya BC na AD zinaendana na Yesu, we unadhani watu walikaa wakajitungia tu...?!
 
Mkuu hebu n saidie asili ya mwanadam n ipi? Ikiwa mungu hayupo
Nahtaji kujifunza ktk hili co kubishana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…