Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Lau kam watu humu wangekuwa wanataka kuelewa kile unachokisimamia kupitia kwa kusoma unachokiandika humu basi wasingekuchukulia kama wanavyokuchukulia sasa,ila bahati mbaya watu wanaishia tu kusoma unachoandika.

Ubishi ni kitu tofauti na ukweli. Ubishi ulivyo unaweza ukamshinda mtu kwa ubishi hata kama huyo mtu alikuwa anasimamia ukweli.

Na wewe ndiyo ulipojikita huko kwenye ubishi kwa kudhani kunakufanya wewe kuwa upande sahihi na ndiyo maana muda wote umekuwa ukirudia kusema tumeshindwa kuthibitisha mara sijui kuondoa contradictions.
Na mimi naweza kusema ubishi ni tofauti na ukweli, wewe unaweza kusemakwaubishi Mungu yupo,wakatihayupo, huwezi kumthibitisha, na ukibanwa unajificha nyuma ya vichaka kadhaa.

1. Imani.
2. Logical non sequitur
3. Deus ex machina
4. General absurdities to confound any reason
5. Not answering logical questions with logical answers
6. Refusing to acknowledge you don't know what you don't know
7. Claiming to know what you don'tknow
8. Lack of intellectual honesty
9. Unmitigated false equivalence
10. Lackof acknowledging the most basic established principles of logic and mathematics

Utasemaje?
 
Kama huna tatizo na imani na haupo hapa kubishana kuhusu imani,maana yake huna tatizo na imani ya kuwa mungu yupo kama ambavyo umekuwa na imani yako ya kuchomoza jua kesho.
Sina tatizo na imani kwamba Mungu yupo.

Mimi ni libertarian.

Katiba ya tanzaniainatetea mtu yeyote kuwa na imani hiyo.

Universal Declaration of Human Rights inatetea mtu yeyote kuwa na imani hiyo.

Serikali ikitaka kuondoa uhuru wa watu kuamini Mungu yupo nitapingana vikali na serikali na kuishutumu serikalikwakuingilia uhuru wa watu kuamini Mungu kwa jinsi ya wanavyotaka wao.

Sitamfuata mtu nyumbani kwake, msikitini kwake, kanisani kwake au nyumba/ sehemu yoyote ya ibada na kumkashifu au kumwambia kwamba imani yake ni potofu.

Lakini, ukija kuhubiri hapa JF kwamba Mungu wako si imani tu, ni ukweli, umevuka mpaka wa imani, na kuingia uwanja wa facts.

Tunajadilihoja kama fact, si imani tu tena.

Ukitaka kuamini unachoaminikwako siwezi na sitaki kukubugudhi.
 
Nikisoma Vitabu Vya Dini Hasa Biblia... Mungu wa Kuanzia Kitabu Cha Mwanzo Au Vitabu Vya Kale Ni Tofauti Sana kitabia na Mungu wa Agano Jipya.

Tabia za KiMungu Alizokuwa nazo Katika agano la Kale Nikilinganisha Na Agano jipya naona Tofauti Kubwa Sana

Mfano AGANO LA KALE
Mungu Alikuwa ni Wa Hasira Sana na Anayependa Sana Waumini wake Wafuate Sheria ... Kulikuwa na Sheria Za Kitakatifu Mfano Kujiosha Mwili... mavazi.. Kuhudumia Sehemu ya Kuabudia kwa usafi wa hali ya juu... kuvukisha Ubani... kujitawaza... n.k n.k

Sasa Nitapokuja Kusoma Agano jipya Mungu anakuwa Amebadilika Sana Hasa Katika Kuabudiwa.. .. Yale Mambo ya kale aliyotaka hayapo tena.. Je Mungu amebadilika Hataki Tena Ubani... Zawadi za kuteketezwa Alizosema zinamvutia?

Je Kuna Ubaya Gani Kutoa Sadaka Za hivyo.. kuna Ubaya Gani Kurudia Kule kwa Kale.. Kujisafisha Uendapo Kuabudu..... Kuwa Msafi Au kujitawaza kama kale...

Mkuu, nadhani wote tunaamini kua BIBLIA Takatifu imeandikwa na watu wa Mungu walioongozwa na ROHO wa Mungu.
Agano la kale lina vitabu ambayo vingi ni torati za Musa na habari za Waamuzi, Wafalme na Manabii...
Agano jipya lina vitabu vya Injili vilivyoandikwa na Wainjilisti (wanafunzi wa Yesu) pamona na Mitume (Mf Paulo).

Ujio wa Agano jipya ni utimilifu wa yaliyoandikwa katika vitabu vya Agano la kale....
Ndio maana mwenyewe Yesu alisema "Siajaja kuibadilisha torati bali kuitimiza" (Sikumbuki kutabu gani nikipata ntaweka)

Agano la kale Mungu alikua anaongea na Manabii ndio Nabii alete ujumbe and vice versa....
Agano jipya baada ya Yesu kusulubiwa na pazia la Hekaluni kupasuka, hii inamaanisha mlango wa kufikisha maombi yako na ibada zako moja kwa moja bila kupitia kwa Manabii kama ilivyokuwa awali.....

Yapo mengi sana ambayo kuandika sitoweza maana mimi sio muandishi mzuri...
 
Sina tatizo na imani kwamba Mungu yupo.

Mimi ni libertarian.

Katiba ya tanzaniainatetea mtu yeyote kuwa na imani hiyo.

Universal Declaration of Human Rights inatetea mtu yeyote kuwa na imani hiyo.

Serikali ikitaka kuondoa uhuru wa watu kuamini Mungu yupo nitapingana vikali na serikali na kuishutumu serikalikwakuingilia uhuru wa watu kuamini Mungu kwa jinsi ya wanavyotaka wao.

Sitamfuata mtu nyumbani kwake, msikitini kwake, kanisani kwake au nyumba/ sehemu yoyote ya ibada na kumkashifu au kumwambia kwamba imani yake ni potofu.

Lakini, ukija kuhubiri hapa JF kwamba Mungu wako si imani tu, ni ukweli, umevuka mpaka wa imani, na kuingia uwanja wa facts.

Tunajadilihoja kama fact, si imani tu tena.

Ukitaka kuamini unachoaminikwako siwezi na sitaki kukubugudhi.
Ndiyo maana nikasema kuwa wewe huna tatizo na imani kuwa mungu,haupingi imani ya uwepo wake mungu..hivyo mie sina tatizo na wewe maana suala la uwepo wa mungu ni imani.

Na imani haina tafsri ya kuwa ni uongo na hakuna anayeamini kitu huku akijua ni uongo.
 
Imani ukiileta JF kujadiliana ushaileta katika uwanja wa mjadala.

Imani inaweza kuwa potofu,unaruhusiwa kuwa na imani potofu, lakini ukiileta JF kwenye mjadala tutasemahii ni imani potofu.

Ukisema hapa unaamini square root ya 2 ni 10, katikabase 10 math, nitakwambia imani hiyo ni potofu.

Ukisema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo na kaumba ulimwengu huu, nitakwambia imani hiyo potofu.

Hata kama ninakwambia kwamba una uhuru wa kukubali imani potofu, huna uhuru wa kuleta imani potofu hapaJF bila watu kusemakwamba imani hiyo ni potofu.

Na imani potofu zipo, kwa sababu wanaoamini square root ya 2 haiwezi kuwa zaidi ya 2 na wanaoamini square root ya 2 ni 10 hawawezi wote kuwa na imani sahihi.
 
Mazee huwa huchoki ku debate kuhusu mungu?
 
Mazee huwa huchoki ku debate kuhusu mungu?
Hakuna debate hapa.

Kuna mijeledi tu ya kichwa watu wanapata.

Siwezi kuchoka kwa sababu hawanifikishi hata kwa Alvin Plantinga, St. Anselm, St. Augustine, Lord Russell, John Mbiti, Richard Dawkins.

Mtu hajui alama ya greater than na less than zikoje na tofauti yake maana yake ni nini, mtu hajui logical consistency ni nini, mtu hajui contradiction maana yake ni nini.

Mtu hajui intersection wala union katika set theory ni nini.

Ni kama Usain Bolt atake kukimbizana na mtoto wa miezi mitatu.

Ataanzaje kuchoka?
 
Unadhani wanaelewa hata kinachojadiliwa ni nini?

Manake mtu ukishajua maana ya imani ni nini sidhani tena kama kuna haja ya mjadala.....

Sometimes huwa naona kama vile hata hawajui maana na tofauti ya ‘kujua’ na ‘kuamini’ ni nini!!
 
Na mimi huwa nawaambia kwamba mimi ni libertarian, natetea uhuru wa watu tofauti kuamini imani zao tofauti.

Nakubali na kutetea "Universal Declaration of Human Rights". Universal Declaration of Human Rights

Nakubali na kutetea vipengele vya katiba na sheria Tanzania vinavyotoa uhuru wa kuabudu.

Sina tatizo na imani ya mtu.

Ila mtu akileta habari za imani yake kama fact hapa JF, tunajadili kama fact na kuhoji.

Hapo nawachanganya kabisa.
 
1.qn.nani alitengeza(umba) ulimwengu.
 
Kwa nini swali lako linauliza "nani"?

Nikikuuliza bendera ya taifa ya Tanzania ni ya rangi nyekundu ipi utajibu vipi?
Kiranga imani yako ya kutokuamini Uwepo Wa Mungu, "Inakutesa"

Kila Siku inaonyesha wazi unaumia Moyo wako kuhusu Mungu na una hasira Fulani kumuhusu! ila sababu kumfikia ni Changamoto unaona bora hasira zako uzimalizie kwa wanaomfagilia Mungu[emoji4]

Imani ya kutokuamini Uwepo Wa Mungu Ingekuwa haikutesi tusingeona Michango yako kadhaa katika threads kadhaa zinazohusu Uwepo wa Mungu..
 
Sijawahi kuanzisha mada kuhusu Mungu kutokuwepo, najibu hoja za watu tu. Sasa imani inanitesa mimi au hao wanaoanzisha maada?

Pia, kama kusema Mungu hayupo ni imani, basi kunyoa kipara ni mtindo wa kusuka nywele.

Zaidi, unaweza kuona nina hasira hata nikipiga chafya tu, kwa sababu wewe unaogopa mtu anayefanya passionate argument.

Mwisho, hujathibitisha Mungu yupo wala kuondoa contradictions katika dhana ya kuwepo kwake.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Nimeanza Kuona Michango yako katika Threads mbalimbali Kwa miaka Kadhaa sasa, Lakini Ajabu ni Kwamba Hadi leo, Swali Ambalo Huwa Unauliza Maelfu ya Watu humu JF ni "Thibitisha uwepo Wa Mungu"

Watu kutoka Imani Tofauti Wamejitahidi Kukuelekeza Kwa kila Njia Lakini Imekuwa Ni ngumu Mno kwako kuelewa, Kila Siku Umekuwa ukija na swali lile lile!.

Isitoshe Hoja Yako ya Kusema Hujui Lolote Kuhusu Mungu na Baadae Mtu akaja na Kukufunza Kuhusu Mungu (Jambo Usilolijua) Na Ukampinga!, Inamaanisha Wazi Kuwa Unajua Jambo Kuhusu Uwepo Wake au Kutokuwepo na Ndo maana Unapinga! Maana Huwezi Kupinga Jambo Usilolijua!

Tukirudi kwenye Nyuzi zote Ambazo umeshawahi Kuchangia Humu, Kila siku Umekuwa Ukiwauliza Watu Swali Moja Tu! "Thibitisha Uwepo Wa Mungu"! (Hili Linatufundisha nini kukuhusu?)

Ina maana Kuwa Una Ukweli Unaoujua Kuhusu uwepo wa Mungu, au Kutokuwepo Kwake.
Ingawa mara kadhaa umekuwa ukidai Kuwa Hujui lolote Kuhusu Mwanzo wetu, Dunia na Universe.

Jibu lako La Kusema Hujui Kitu!, Lina Mashaka Kwa Sababu,
* Huwezi Kubisha Jambo ambalo hujui!
* Huwezi Kuspend Kwa Miaka Ukiwapinga Watu Na
Kujaribu Kuwafanya waamini, Usichokijua!

Sina hakika kama Hujawahi Kupata Muda wa Kujifunza habari za Mungu Ulipokuwa mdogo, Naamini Ulijifunza na Kuna Mambo Kadhaa yaliyokutokea Maishani Mwako, Ndiyo Yaliyokuja kukupa Mashaka Kuhusu Uwepo wa Mungu.

Kilichobaki Sasa Ni kama kupoza Maumivu, Kila Ukiona Uzi Wowote Wa Watu wazungumziao Mungu, Unaingia Na Kuanza kupinga, "Ukiwauliza Wathibitishe Uwepo wake!" Na si hapa JF tu najua Hadi Kwenye Mizunguko yako ya Kila siku.

Naamini Kuna Kipindi Katika maisha yako ambacho Ulitumatumai, Mambo Yataenda Kulia Sababu Ulimuamini Mungu, Ila Yakaenda Kushoto, Ukabaki na Kisasi na Na Maumivu Juu Ya kuamini Uwepo wake, (Kitu Useless!,)

Nadhani huu Ni Muda kwako sio wa Kuendelea kupinga, Ila Jaribu Kufikiri maradufu ya Ulivyowahi Kufikiri kuhusu Manbo haya, Utapata Jibu na ahueni ya Maumivu Uliyonayo Juu Ya Mungu Itatoka Kabisa.

Hakuna Kilichopo kwa bahati mbaya Kiranga.
 
Mkuu kiranga mimi nilikuwa na swali..

Hivi unaamini uchawi upo? Pia na majini yapo?
 
Imani ukiileta JF kujadiliana ushaileta katika uwanja wa mjadala.

Imani inaweza kuwa potofu,unaruhusiwa kuwa na imani potofu, lakini ukiileta JF kwenye mjadala tutasemahii ni imani potofu.

Ukisema hapa unaamini square root ya 2 ni 10, katikabase 10 math, nitakwambia imani hiyo ni potofu.

Ukisema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo na kaumba ulimwengu huu, nitakwambia imani hiyo potofu.

Hata kama ninakwambia kwamba una uhuru wa kukubali imani potofu, huna uhuru wa kuleta imani potofu hapaJF bila watu kusemakwamba imani hiyo ni potofu.

Na imani potofu zipo, kwa sababu wanaoamini square root ya 2 haiwezi kuwa zaidi ya 2 na wanaoamini square root ya 2 ni 10 hawawezi wote kuwa na imani sahihi.
Ona sasa umeanza kuzungumzia imani potofu wakati ulishasema hauzungumzii imani hapa.

Ukianza kuleta habari za usahihi na upotofu wa imani hapo tutakuwa tunajadili imani na wewe ulishasema hautaki kujadili imani.
 
Hebu tuangalie point moja baada ya nyingine, kwa kina, kwa uangalifu, kwa jitihada ya kuona kama kuna kipya, bila dharau.

Nimeanza Kuona Michango yako katika Threads mbalimbali Kwa miaka Kadhaa sasa, Lakini Ajabu ni Kwamba Hadi leo, Swali Ambalo Huwa Unauliza Maelfu ya Watu humu JF ni "Thibitisha uwepo Wa Mungu"

Swali ambalo mpaka leo halijajibiwa kwa ufasaha, na hivyo litarudiwa tu.

Unamuuliza mtu athibitishe uwepo wa Mungu, anakuambia pumzi yako, uhai, sayari zinavyozunguka jua, vinathibitisha Mungu yupo.

Unamuuliza, vinathibitishaje? Unajuaje kwamba vitu hivyo vinathibitisha uwepo wa Mungu na si uthibitisho wa jingine lolote? Mtu anashindwa kujibu.

Halafu anakwambia kashakujibu, kwa kukariri maneno asiyoyaelewa. Kwa msingi huo, swali lazima lirudiwe, kwa sababu halijajibiwa.

Hata wewe nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Watu kutoka Imani Tofauti Wamejitahidi Kukuelekeza Kwa kila Njia Lakini Imekuwa Ni ngumu Mno kwako kuelewa, Kila Siku Umekuwa ukija na swali lile lile!.

Taja njia moja ambayo inathibitisha Mungu yupo tuichambue hapa, usiongelee mambo kijumla jumla, toa uthibitisho kwamba Mungu yupo. Let's go with the specifics.

Isitoshe Hoja Yako ya Kusema Hujui Lolote Kuhusu Mungu na Baadae Mtu akaja na Kukufunza Kuhusu Mungu (Jambo Usilolijua) Na Ukampinga!, Inamaanisha Wazi Kuwa Unajua Jambo Kuhusu Uwepo Wake au Kutokuwepo na Ndo maana Unapinga! Maana Huwezi Kupinga Jambo Usilolijua!

Wapi nimesema sijui lolote kuhusu Mungu? Nimesema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu uliojaa mabaya, hayupo, kwa sababu kuwepo kwake ni contradiction kama kuwepo pembetatu mviringo katika plane Euclidean geometry, au square root ya 2 kuwa 10. Habari zote hizi haziwezekani kuwepo, kwa sababu zina contradiction.

Unaelewa contradiction ni nini?

Tukirudi kwenye Nyuzi zote Ambazo umeshawahi Kuchangia Humu, Kila siku Umekuwa Ukiwauliza Watu Swali Moja Tu! "Thibitisha Uwepo Wa Mungu"! (Hili Linatufundisha nini kukuhusu?)

Kwanza kabisa si kweli kwamba nimeuliza swali moja tu "thibitisha uwepo wa Mungu". Kusema hivyo kunaonesha mawili.

1. Hujui/ huwezi kunisoma kwa ufasaha
2. Unaweza kunisoma kwa ufasaha ila unapindisha mambo kwa kutaka tu.

Kwa sababu nimeuliza mengine mengi tu zaidi ya hilo. Hata kwenye uzi huu tu, sembuse nyuzi nyingine nyingi.

Nimeuliza.

1. Kama Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote yupo, na kaumba ulimwengu huu, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea? (the problem of evil)

2. Kama Mungu kweli anajua kila kitu, anajua maisha ya watu yote mwanzo mpaka mwisho, na anachojua yeye hakiwezi kubadilika,hivyo anaweza kujua fulani ataua hata kabla fulani hajazaliwa, sasa hapo Mungu akishajua fulani ataua, kabla fulani hajazaliwa, huyo fulani akizaliwa, ana uhuru gani wa kuepuka kuua? ( human free will cannot be reconciled with God's perfect knowledge, this leads to a contradiction)

3.Kama mtu tu wa kawaida, ambaye hana upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote, akijenga nyumba na kuitegeshea mabomu yatakayofanya watoto wake wafe, tutamuona mnyama au kichaa, inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu na kuujaza natural disasters zinazoua mpaka watoto wasio na hatia tunamsifu kwamba ana upendo mkuu wakati amefanya chini ya hata haki za kibinadamu? 9Gods morality failing to meet even the most basic of human standards shows God is a hoax)

4. Kama Mungu anaweza yote, je anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi kwamba hawezi kulibeba? Aakiweza, kuna kitu atakuwa kashindwa (kulibeba jiwe) asipoweza, kuna kitu atakuwa kashindwa (kuumba jiwe zito kiasi kwamba hawezi kulibeba). Mungu muweza vyote hawezekani kuwapo. (The idea of God crumbling under it's own weight)

5. Kwa nini kuna contraditions nyingi sana katika Quran?

Contradictions / Difficulties in the Qur'an

6. Kwa nini kuna contradictions nyingi sana katika Biblia

Bible Inconsistencies - Bible Contradictions

7. Kama Mungu yupo, kwa nini hajiweki wazi katika njia ambayo kila mtu atamjua bila shaka?

8. Kama Mungu yupo, na anajulikana kwa neema yake tu, na si kwa jitihada ya mtu, watu ambao wamejitahidi sana kumjua kwa kuuliza maswali mengi sana kama mimi lakini bado wakawa hawajapata neema ya kumjua, kesho kama kiyama kipo kweli, tukikutana naye, akataka kutuhukumu, tukamwambia Mungu tulikutafuta sana, angalia servers za JF maswali tuliyouliza kuhusu uwepo wako, kwa kutumia akili ulizotupa mwenyewe, lakini hukutupa neema ya kukujua, kwa nini unataka kutuhukumu sisi kwa jambo ambalo wewe mwenyewe hujatupa neema ya kulijua licha ya sisi kuhangaika sana kulijua. Mungu atajitetea vipi?

9. Kle ambacho kinaweza kuaminiwa bila ushahidi, kinaweza kutupiliwa mbali bila kuaminiwa bila ushahidi (Hitchens Razor). Ushahidi kwamba Mungu yupo uko wapi?

10. Kwa nini mnatumia logical non sequitur, deus ex machina and random unmitigated arbitrariness kumtetea Mungu ambaye hana ushahidi wala uthibitisho kuwepo?

Hakuna hata moja lililojibiwa kimantiki hapo. Kama una jibu weka hapa.

Ina maana Kuwa Una Ukweli Unaoujua Kuhusu uwepo wa Mungu, au Kutokuwepo Kwake.
Ingawa mara kadhaa umekuwa ukidai Kuwa Hujui lolote Kuhusu Mwanzo wetu, Dunia na Universe.

Nina ukweli ninaoujua. Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu hayupo. Kwa sababu kuwepo kwake ni contradiction kama kuwepo kwa pembetatu duara ama square root ya 2 kuwa 10.

Jibu lako La Kusema Hujui Kitu!, Lina Mashaka Kwa Sababu,
* Huwezi Kubisha Jambo ambalo hujui!
* Huwezi Kuspend Kwa Miaka Ukiwapinga Watu Na
Kujaribu Kuwafanya waamini, Usichokijua!

Unajua kusoma? Nimesema sijui kitu kuhusu nini?

N kwa nini nisibishe jambo ambalo sijui?

Sijui square root ya 2 ni nini katika decimal point system. Hakuna binadamu anayeweza kuiandika na kuimaliza, kwa sababu hii ni irrational number ambayo hai truncate katika decimal system, lakini mtu akiniambia square root ya 2 ni 10, najua hilo ni jibu la uongo, kwa sababu lina contradiction.

Ukiletewa mtoto wa miezi miwili leo, ukaambiwa huyu ndiye baba yako mzazi wa kibaiolojia, hata kama humjui huyo mtoto, utakataa hiyo hoja kwa sababu mtoto wa miezi miwili hawezi kuwa baba yako mzazi wa kibaiolojia. Hapo kuna contradiction.

Nani anafanya watu wajaribu kuamini? Mbona huelewi somo? Sipo hapa kujadili imani, najadili facts. Sitaki habari za kuamini, nataka kujua.

Sina hakika kama Hujawahi Kupata Muda wa Kujifunza habari za Mungu Ulipokuwa mdogo, Naamini Ulijifunza na Kuna Mambo Kadhaa yaliyokutokea Maishani Mwako, Ndiyo Yaliyokuja kukupa Mashaka Kuhusu Uwepo wa Mungu.

Ttaizo unaandika mambo mengi ambayo huna hakika nayo kama una hakika nayo, likiwemo la kuwepo kwa Mungu.

Unaweza kuthibitisha Mung yupo na kujibu maswali yangu 10 hapo juu?

Kilichobaki Sasa Ni kama kupoza Maumivu, Kila Ukiona Uzi Wowote Wa Watu wazungumziao Mungu, Unaingia Na Kuanza kupinga, "Ukiwauliza Wathibitishe Uwepo wake!" Na si hapa JF tu najua Hadi Kwenye Mizunguko yako ya Kila siku.

Thibitisha Mungu yupo.

Naamini Kuna Kipindi Katika maisha yako ambacho Ulitumatumai, Mambo Yataenda Kulia Sababu Ulimuamini Mungu, Ila Yakaenda Kushoto, Ukabaki na Kisasi na Na Maumivu Juu Ya kuamini Uwepo wake, (Kitu Useless!,)

Mambo yataenda kulia halafu yakaenda kushoto? Mimi mambo yangu yako safi wewe, nimeridhika kiasi changu, maisha yangu yameenda vizuri tu.

I got a crib i the hood, the burb and the city
I split ribs over wood, I blurb what a pity
I was walking the corridors of Ikulu since in my mama's womb
And now I'm joking with Natal Zulu til the days of my tomb
I got connections, New York Geneva to Magogoni
Like Lexis-Nexis, you're starting to bore me
I got cribs, a good family whips and I help people
And I am aging gracefully no Blood or Crips, even as I love hip hop
Take a ride in my beemer, ain't no ancient steamer
Tell your friends Kiranga treated you, the nascent redeemer

Nadhani huu Ni Muda kwako sio wa Kuendelea kupinga, Ila Jaribu Kufikiri maradufu ya Ulivyowahi Kufikiri kuhusu Manbo haya, Utapata Jibu na ahueni ya Maumivu Uliyonayo Juu Ya Mungu Itatoka Kabisa.

Nadhani, nadhani, nadhani, nadhani. Kuna chochote unachojua na kuwza kuthibitisha?

Nikisema nadhani una ugonjwa wa akili utakubali?

Hakuna Kilichopo kwa bahati mbaya Kiranga.

Nani kasema kuna kilichopo kwa bahati mbaya? Kwa nini unaniambia mimi hivyo?

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na kujibu maswali yangu 10 hapo juu?
 
Ona sasa umeanza kuzungumzia imani potofu wakati ulishasema hauzungumzii imani hapa.

Ukianza kuleta habari za usahihi na upotofu wa imani hapo tutakuwa tunajadili imani na wewe ulishasema hautaki kujadili imani.

Wwe have been here before. Nikakuuliza swali. Ukalikimbia bila kulijibu.

Nilikuuliza.

Nikisema sitaki kukaa Dodoma, nataka kupita tu Dodoma kuelekea Mwanza, ukinikuta nipo Dodoma katika gari barabarani nipo katika mwendo nakwenda Mwanza, utasema "ona sasa umekaa Dodoma ambapo ulisema hutaki kukaa"?

Kujadili imani kama ni potofu au si potofu ni njia ya kutoka katika imani tu na kuelekea kwenye ujuzi wa kweli.

Nikisema sitaki imani, nataka kujua, hilo halina maana sijadili imani katika muktadha wa kutaka kujua ukweli.

Nikisema sitaki kukaa Dodoma, nataka kwenda kukaa Mwanza, hilo halina maana kwamba sipiti Dodoma katika muktadha wa kuwa njiani kwenda Mwanza.

Swali langu hukulijibu. Ulilikimbia.

Narudia kuuliza.

Nikisema sitaki kukaa Dodoma, nataka kupita tu Dodoma kuelekea Mwanza, ukinikuta nipo Dodoma katika gari barabarani nipo katika mwendo nakwenda Mwanza, utasema "ona sasa umekaa Dodoma ambapo ulisema hutaki kukaa"?
 
Mkuu kiranga mimi nilikuwa na swali..

Hivi unaamini uchawi upo? Pia na majini yapo?
Uchawi ni nini na majini ni nini?

Kabla ya kujibu swali lako naomba unieleweshe.

Ni katika kuwekana sawa tu ili nisije kujibu kitu ambacho sijaulizwa na kuacha kujibu nilichoulizwa.
 
Uchawi ni nini na majini ni nini?

Kabla ya kujibu swali lako naomba unieleweshe.

Ni katika kuwekana sawa tu ili nisije kujibu kitu ambacho sijaulizwa na kuacha kujibu nilichoulizwa.
Uchawi ni nguvu fulani zinazotumiwa na watu wenye ujuzi maalum

Na majini ni viumbe fulani wenye uwezo mkubwa na wasioonekana kwa macho ila tu mpaka uwe na elimu au ujuzi fulani wa kiroho
 
Back
Top Bottom