Hebu tuangalie point moja baada ya nyingine, kwa kina, kwa uangalifu, kwa jitihada ya kuona kama kuna kipya, bila dharau.
Nimeanza Kuona Michango yako katika Threads mbalimbali Kwa miaka Kadhaa sasa, Lakini Ajabu ni Kwamba Hadi leo, Swali Ambalo Huwa Unauliza Maelfu ya Watu humu JF ni "Thibitisha uwepo Wa Mungu"
Swali ambalo mpaka leo halijajibiwa kwa ufasaha, na hivyo litarudiwa tu.
Unamuuliza mtu athibitishe uwepo wa Mungu, anakuambia pumzi yako, uhai, sayari zinavyozunguka jua, vinathibitisha Mungu yupo.
Unamuuliza, vinathibitishaje? Unajuaje kwamba vitu hivyo vinathibitisha uwepo wa Mungu na si uthibitisho wa jingine lolote? Mtu anashindwa kujibu.
Halafu anakwambia kashakujibu, kwa kukariri maneno asiyoyaelewa. Kwa msingi huo, swali lazima lirudiwe, kwa sababu halijajibiwa.
Hata wewe nakuuliza, unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Watu kutoka Imani Tofauti Wamejitahidi Kukuelekeza Kwa kila Njia Lakini Imekuwa Ni ngumu Mno kwako kuelewa, Kila Siku Umekuwa ukija na swali lile lile!.
Taja njia moja ambayo inathibitisha Mungu yupo tuichambue hapa, usiongelee mambo kijumla jumla, toa uthibitisho kwamba Mungu yupo. Let's go with the specifics.
Isitoshe Hoja Yako ya Kusema Hujui Lolote Kuhusu Mungu na Baadae Mtu akaja na Kukufunza Kuhusu Mungu (Jambo Usilolijua) Na Ukampinga!, Inamaanisha Wazi Kuwa Unajua Jambo Kuhusu Uwepo Wake au Kutokuwepo na Ndo maana Unapinga! Maana Huwezi Kupinga Jambo Usilolijua!
Wapi nimesema sijui lolote kuhusu Mungu? Nimesema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu uliojaa mabaya, hayupo, kwa sababu kuwepo kwake ni contradiction kama kuwepo pembetatu mviringo katika plane Euclidean geometry, au square root ya 2 kuwa 10. Habari zote hizi haziwezekani kuwepo, kwa sababu zina contradiction.
Unaelewa contradiction ni nini?
Tukirudi kwenye Nyuzi zote Ambazo umeshawahi Kuchangia Humu, Kila siku Umekuwa Ukiwauliza Watu Swali Moja Tu! "Thibitisha Uwepo Wa Mungu"! (Hili Linatufundisha nini kukuhusu?)
Kwanza kabisa si kweli kwamba nimeuliza swali moja tu "thibitisha uwepo wa Mungu". Kusema hivyo kunaonesha mawili.
1. Hujui/ huwezi kunisoma kwa ufasaha
2. Unaweza kunisoma kwa ufasaha ila unapindisha mambo kwa kutaka tu.
Kwa sababu nimeuliza mengine mengi tu zaidi ya hilo. Hata kwenye uzi huu tu, sembuse nyuzi nyingine nyingi.
Nimeuliza.
1. Kama Mungu mwenye ujuzi wote, uwezo wote na upendo wote yupo, na kaumba ulimwengu huu, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea? (the problem of evil)
2. Kama Mungu kweli anajua kila kitu, anajua maisha ya watu yote mwanzo mpaka mwisho, na anachojua yeye hakiwezi kubadilika,hivyo anaweza kujua fulani ataua hata kabla fulani hajazaliwa, sasa hapo Mungu akishajua fulani ataua, kabla fulani hajazaliwa, huyo fulani akizaliwa, ana uhuru gani wa kuepuka kuua? ( human free will cannot be reconciled with God's perfect knowledge, this leads to a contradiction)
3.Kama mtu tu wa kawaida, ambaye hana upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote, akijenga nyumba na kuitegeshea mabomu yatakayofanya watoto wake wafe, tutamuona mnyama au kichaa, inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu na kuujaza natural disasters zinazoua mpaka watoto wasio na hatia tunamsifu kwamba ana upendo mkuu wakati amefanya chini ya hata haki za kibinadamu? 9Gods morality failing to meet even the most basic of human standards shows God is a hoax)
4. Kama Mungu anaweza yote, je anaweza kuumba jiwe zito sana kiasi kwamba hawezi kulibeba? Aakiweza, kuna kitu atakuwa kashindwa (kulibeba jiwe) asipoweza, kuna kitu atakuwa kashindwa (kuumba jiwe zito kiasi kwamba hawezi kulibeba). Mungu muweza vyote hawezekani kuwapo. (The idea of God crumbling under it's own weight)
5. Kwa nini kuna contraditions nyingi sana katika Quran?
Contradictions / Difficulties in the Qur'an
6. Kwa nini kuna contradictions nyingi sana katika Biblia
Bible Inconsistencies - Bible Contradictions
7. Kama Mungu yupo, kwa nini hajiweki wazi katika njia ambayo kila mtu atamjua bila shaka?
8. Kama Mungu yupo, na anajulikana kwa neema yake tu, na si kwa jitihada ya mtu, watu ambao wamejitahidi sana kumjua kwa kuuliza maswali mengi sana kama mimi lakini bado wakawa hawajapata neema ya kumjua, kesho kama kiyama kipo kweli, tukikutana naye, akataka kutuhukumu, tukamwambia Mungu tulikutafuta sana, angalia servers za JF maswali tuliyouliza kuhusu uwepo wako, kwa kutumia akili ulizotupa mwenyewe, lakini hukutupa neema ya kukujua, kwa nini unataka kutuhukumu sisi kwa jambo ambalo wewe mwenyewe hujatupa neema ya kulijua licha ya sisi kuhangaika sana kulijua. Mungu atajitetea vipi?
9. Kle ambacho kinaweza kuaminiwa bila ushahidi, kinaweza kutupiliwa mbali bila kuaminiwa bila ushahidi (Hitchens Razor). Ushahidi kwamba Mungu yupo uko wapi?
10. Kwa nini mnatumia logical non sequitur, deus ex machina and random unmitigated arbitrariness kumtetea Mungu ambaye hana ushahidi wala uthibitisho kuwepo?
Hakuna hata moja lililojibiwa kimantiki hapo. Kama una jibu weka hapa.
Ina maana Kuwa Una Ukweli Unaoujua Kuhusu uwepo wa Mungu, au Kutokuwepo Kwake.
Ingawa mara kadhaa umekuwa ukidai Kuwa Hujui lolote Kuhusu Mwanzo wetu, Dunia na Universe.
Nina ukweli ninaoujua. Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ambaye kaumba ulimwengu huu hayupo. Kwa sababu kuwepo kwake ni contradiction kama kuwepo kwa pembetatu duara ama square root ya 2 kuwa 10.
Jibu lako La Kusema Hujui Kitu!, Lina Mashaka Kwa Sababu,
* Huwezi Kubisha Jambo ambalo hujui!
* Huwezi Kuspend Kwa Miaka Ukiwapinga Watu Na
Kujaribu Kuwafanya waamini, Usichokijua!
Unajua kusoma? Nimesema sijui kitu kuhusu nini?
N kwa nini nisibishe jambo ambalo sijui?
Sijui square root ya 2 ni nini katika decimal point system. Hakuna binadamu anayeweza kuiandika na kuimaliza, kwa sababu hii ni irrational number ambayo hai truncate katika decimal system, lakini mtu akiniambia square root ya 2 ni 10, najua hilo ni jibu la uongo, kwa sababu lina contradiction.
Ukiletewa mtoto wa miezi miwili leo, ukaambiwa huyu ndiye baba yako mzazi wa kibaiolojia, hata kama humjui huyo mtoto, utakataa hiyo hoja kwa sababu mtoto wa miezi miwili hawezi kuwa baba yako mzazi wa kibaiolojia. Hapo kuna contradiction.
Nani anafanya watu wajaribu kuamini? Mbona huelewi somo? Sipo hapa kujadili imani, najadili facts. Sitaki habari za kuamini, nataka kujua.
Sina hakika kama Hujawahi Kupata Muda wa Kujifunza habari za Mungu Ulipokuwa mdogo, Naamini Ulijifunza na Kuna Mambo Kadhaa yaliyokutokea Maishani Mwako, Ndiyo Yaliyokuja kukupa Mashaka Kuhusu Uwepo wa Mungu.
Ttaizo unaandika mambo mengi ambayo huna hakika nayo kama una hakika nayo, likiwemo la kuwepo kwa Mungu.
Unaweza kuthibitisha Mung yupo na kujibu maswali yangu 10 hapo juu?
Kilichobaki Sasa Ni kama kupoza Maumivu, Kila Ukiona Uzi Wowote Wa Watu wazungumziao Mungu, Unaingia Na Kuanza kupinga, "Ukiwauliza Wathibitishe Uwepo wake!" Na si hapa JF tu najua Hadi Kwenye Mizunguko yako ya Kila siku.
Thibitisha Mungu yupo.
Naamini Kuna Kipindi Katika maisha yako ambacho Ulitumatumai, Mambo Yataenda Kulia Sababu Ulimuamini Mungu, Ila Yakaenda Kushoto, Ukabaki na Kisasi na Na Maumivu Juu Ya kuamini Uwepo wake, (Kitu Useless!,)
Mambo yataenda kulia halafu yakaenda kushoto? Mimi mambo yangu yako safi wewe, nimeridhika kiasi changu, maisha yangu yameenda vizuri tu.
I got a crib i the hood, the burb and the city
I split ribs over wood, I blurb what a pity
I was walking the corridors of Ikulu since in my mama's womb
And now I'm joking with Natal Zulu til the days of my tomb
I got connections, New York Geneva to Magogoni
Like Lexis-Nexis, you're starting to bore me
I got cribs, a good family whips and I help people
And I am aging gracefully no Blood or Crips, even as I love hip hop
Take a ride in my beemer, ain't no ancient steamer
Tell your friends Kiranga treated you, the nascent redeemer
Nadhani huu Ni Muda kwako sio wa Kuendelea kupinga, Ila Jaribu Kufikiri maradufu ya Ulivyowahi Kufikiri kuhusu Manbo haya, Utapata Jibu na ahueni ya Maumivu Uliyonayo Juu Ya Mungu Itatoka Kabisa.
Nadhani, nadhani, nadhani, nadhani. Kuna chochote unachojua na kuwza kuthibitisha?
Nikisema nadhani una ugonjwa wa akili utakubali?
Hakuna Kilichopo kwa bahati mbaya Kiranga.
Nani kasema kuna kilichopo kwa bahati mbaya? Kwa nini unaniambia mimi hivyo?
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na kujibu maswali yangu 10 hapo juu?