Je! Mungu ni yule yule?

Uchawi ni nguvu fulani zinazotumiwa na watu wenye ujuzi maalum

Na majini ni viumbe fulani wenye uwezo mkubwa na wasioonekana kwa macho ila tu mpaka uwe na elimu au ujuzi fulani wa kiroho
Nuclear bombs ni nguvu fulani zinazotumiwa na watu wenye ujuzi maalum.

Nuclear bombs ni uchawi?

Unaposema majini hayaonekani mpaka uwe na ujuzi wa kiroho, roho ni nini? Unaweza kuthibitisha ipo?
 
Mkuu kiranga mimi nilikuwa na swali..

Hivi unaamini uchawi upo? Pia na majini yapo?
Sawa, Mzee Miaka Yote Utakuwa Ukiuliza Swali Hilo hilo, Na Hutakuja Kupata Jibu Lolote, Ushauri wangu "Amini Unachoamini" Kisha Uendelee Na Mambo Mengine Tofauti na Hili.
 
Sawa, Mzee Miaka Yote Utakuwa Ukiuliza Swali Hilo hilo, Na Hutakuja Kupata Jibu Lolote, Ushauri wangu "Amini Unachoamini" Kisha Uendelee Na Mambo Mengine Tofauti na Hili.
Hujathibitisha Mungu yupo.

Ukimwambia mtu "Amini Unachoamini" hiyo sentensi ni logical tautology.

Mimi najadili fact. Imani kila mtu ana yake na anaruhusiwa kuamini anachotaka.

Pia, ukimwambia mtu "Amini unachoamini" ushamtaka aamini unachoamini wewe na si kufanya kile anachotaka kufanya yeye. Umempa fundisho yeye kwamba aamini anachoamini, wakati hujui kama anataka kuamini ama la, pengine hatakibkuamini, anataka kujua.
 
Nuclear bombs ni nguvu fulani zinazotumiwa na watu wenye ujuzi maalum.

Nuclear bombs ni uchawi?

Unaposema majini hayaonekani mpaka uwe na ujuzi wa kiroho, roho ni nini? Unaweza kuthibitisha ipo?
Mkuu sasa mfano watu wanapowekana misukule huwa wanatumia nguvu gani?
Si ndo uchawi wenyewe huo
 
Mkuu naona umemtaja St Augustine...
 
Mkuu sasa mfano watu wanapowekana misukule huwa wanatumia nguvu gani?
Si ndo uchawi wenyewe huo
Misukule ni nini? Utajuaje misukule ni uchawi wakati hata uchawi wenyewe hujaweza kuuelezea ni kitu gani?

Unajuaje kwamba hiyo unayoiita misukule si watu wenye aina fulani ya matatizo ya akili tu, wewe unaita uchawi bila hata ya kuweza kuelezea uchawi ni kitu gani?
 
Mkuu naona umemtaja St Augustine...

Bora hata wewe umemtambua St. Augustine.

Umemsoma St. Augustine?

Hapa nabishana na watu wanaotetea uwepo wa Mungu, mimi nimewasoma hao wote niliowataja.

Wao hawamjui hata mmoja, hawajawahi kusoma chochote kati ya kazi za hao watu.

Lazima tukose kuelewana.

St. Augustine unamtambua kwa lipi katika muktadha wa mjadala huu?
 

Usiwasemee watu..unawezaje kujua kuwa hawajui hao unaowazungumzia..!?

Kwani ni lazima kuwajua,ili kuelewa Umaana wa Maisha?

Acha Majivuno yasiyo ya Lazima.

Napenda unavyosababu,lakini maneno ya namna hii yanaonesha aina fulani ya Udhaifu uliokua nao. Majivuno,kujihesabu kabla Ujahesabiwa.

Yaani wewe na Kukariri kwako huku ukiongeza jitihada kidogo Tu..Ya Unyenyekevu Unatoboza
 
Siogopi kusema kile ninachoona kuwa ni sawa kwa sababu ya kukuogopa wewe utanifikiri mimi vipi.

Hiyo ni moja kati ya tabia za kijinga kabisa na kikondoo, sijawahi kuwa na tabia hiyo hapa JF na sitaki kuanza sasa baada ya miaka yote hii.

Kama watu, kutokana na maandishi yao hapa (kujibu swali lako nitajuaje watu hawajui maandishi ya St. Augustine) wanaonekana hawajasoma the basic arguments for and against the existence of God, nitasema hilo.

Kama una inferiority complex ya kuona mimi kusema hivyo ni ujivuni, hilo ni tatizo lako la kisaikolojia, si tatizo langu. Mimi nashikilia kusema ukweli tu, sijali ukweli utaumiza vipi ego yako.

Kama kuna cha kubishana, tubishane kama ninachoandika ni kweli au si kweli.

Nishapandishiana mpaka na Invisible hapa, kwa kuwa nilisimamia msimamo wangu, to his credit, alikubali JF ilipopinda na hakuwa na maneno zaidi. Sasa wewe nani utake kunipangia nini cha kusema?

Mjadala ni, je kuna watu wanabishana habari za kuwepo Mungu wakati hata hawajasoma falsafa hii ya kuwapo kwa Mungu hata kwa ngwe ya awali kabisa? Kama wapo, kusema kwamba wapo, kwa kutiliamkazo wajifunze zaidi kablaya kubishana, kuna ubaya gani?

Unachoweza kuona wewe majivuno, wengine wataona ni uwazi tu. Pengine watu wanatafuta cha kusoma zaidi ya Quran na Biblia, na mimi kumtaja tu St. Augustine na hao wengine kunawapa watu pa kuanzia kutafuta kazi zao wasome ili waje na nondo za maana hapa kueleweshana, badala ya kuamini Mungu yupokwa sababu umezaliwa katika familia inayoamini Mungu yupo tu. Hapo kuna ubaya gani kusema watu wengi wanabishana bila kusoma?

Na kama ni kweli watu wanamtetea Mungu bila kusoma kwa undani falsafa za kumtetea Mungu, nitasema hilo. Na wewe huwezikunizuia kwa blackmail ya kunipaka rangi ya ujivuni.

Kama kusema kile ninachoona kweli ni ujivuni, naomba ruhusa nibadili jina nijiite "Mjivuni No. 1". Hiyo itakuwa sifa nzuri kwangu, si mbaya.

Na kuna watu wengi wanabishana na mimi kumtetea Mungu wakati hata hawajamsoma St. Augustune.

Na ingawa ninkweli si lazima kumsoma St. Augustine ili kuweza kujenga hoja, nikibishana na mtu ambaye hajamsoma St. Augustine na faksafa zake kuhusu kumtetea Mungu na mtu aliyemsoma St. Augustine, kuna mambo tutaobgea mara moja tu nabkuelewana, mtu ambaye hajamsoma St. Augustine inaweza kynichukua mwaka kuwa naye pamoja.

Mimi usiniambie habari za kutoboa, huji kama sinatobia, hujui kama kutobia ni muhimu kwangu, hujuibkama nataka kutoboa.

I don't need your fake modesty.

I would rather be real.

Ukweli ni kwamba wabingo watu wengi ninaobishana nao hapa hata Kiingereza, lugha ambayo mijadala hii imeandikwa kwa kina, ni cha manati.

Hata wanaojua hawafuatulii haya mambo na wengi hawajamsoma St. Augustine. Arguments zao, au kukisekana kwa argument kutoka kwao, kunaonesha hilo.

Sasa kwa nini unataka nisiseme ukweli ninaouona na kujifanya nina adabu za uongo?

Adabu za uongo ni kujosa adabu kwangu.

Usitake kunifundisha cha kusema.

Sikohapa kukupendeza wewe au mtu mwingine yeyote.

Kwa nini unataka kunipangia priorities,unipangie kwamba adabu ya uongo ni kitu muhimukuliko kusema kile ambachonakiona ni kweli?

Kwa nini?

Jadili.
 
@Kiranga , Toa darasa kidogo kuhusiana na st. Augustine ili na siye tusiojua kimombo tuambulie lolote kutoka kwake!!
 
@Kiranga , Toa darasa kidogo kuhusiana na st. Augustine ili na siye tusiojua kimombo tuambulie lolote kutoka kwake!!
Shukurani kwa kuona umuhimu wakusoma mambo na kuyachambua kabla ya kurukia kujadili.

Kwa sasa nipo mzigoni,siwezikulifanyiaombi lako kazi vizuri.

Ila sishindwi kuchukua muda wangu baadaye kuandika au kutafsiri kitu kama ninaona kinafaa.

Nishawahi kutafsiri moja kati ya misahafu ya Buddhism "Dhammapada" kwenda Kiswahili, katika jitihada za kupanua mawazo na uelewa wa watu wetu katika falsafa za dini mbalimbali zaidi ya hizi tulizozoea za Ukristo na Uislamu.

Kwa sasa, wanaoelewa Kiingereza wanaweza kuanza kusoma hii document hapa imejaribu kuelezea.

https://philarchive.org/archive/CHAAAF-3
 

Sijui hata kama unaelewa hizo point vizuri ulizoziandika mwenyewe!!
Sasa sijui kwenye fact tunaanzaje kujadili imani ipi sahihi na ipi sio sahihi!!.

Hasa tukitumia tafsiri yako kwamba kuamini ni kukubali jambo bila uthibitisho.
 
Sijui hata kama unaelewa hizo point vizuri ulizoziandika mwenyewe!!
Sasa sijui kwenye fact tunaanzaje kujadili imani ipi sahihi na ipi sio sahihi!!.

Hasa tukitumia tafsiri yako kwamba kuamini ni kukubali jambo bila uthibitisho.

Nibaki namfano wangu wa kusafiri kwenda Mwanza kwakupitia Dodoma.

Unachouliza hapo ni kama vile umuulize mtu, wewe unataka kwenda Mwanza, unaanzaje kujadili kwamba ukiwa Dodomauelekee muelekeo gani?

Usipokadili uelekee muelekeo gani kutokaDodoma ili ufike Mwanza, unaweza kujikuta unazunguka Dodoma hapohapo Mwanza hufiki, au unarudiulikotoka Dar.

Kama natafuta fact, na kuna imani nyingi tofauti, nazichuja imani kutafuta ipiya ukweli.

Ntest ya kwanza ni logical consistency.

Kama naenda Mwanza kutoka Dodoma kwa barabara nyoofu (for simplicity's sake), Mwanza ni magharibi ya Dodoma, kurudi mashariki ni kurudi DAR.

Sasa kwa nini unaniambia niende Mwanza kutoka Dodoma bila kuangalia naelekea muelekeo upi?

Kwa nini unataka nitafute fact kutoka imani bila kuhoji imani tofauti?
 
Kwa nini swali lako linauliza "nani"?

Nikikuuliza bendera ya taifa ya Tanzania ni ya rangi nyekundu ipi utajibu vipi?
Basi naweka vizuri s
Kwa nini swali lako linauliza "nani"?
Nikikuuliza bendera ya taifa ya Tanzania ni ya rangi nyekundu ipi utajibu vipi?
Nabadili muundo wa swali.
.........is/are creater of universe.
Jaza nafasi iliowazi hapo juu.
 
Hii ni moja ya nukuu yakee..

[W]hat is believed without being known cannot be said to have been found, and no one can become fit for finding God unless he believes first what he shall know afterwards.

Mkuu Kiranga.. St Augustine nimemsomaa ilaaa so deep kivilee na bado naendeleaa kumsomaa itaquwaa vidhurii zaidii kamaa una nondo zake ningeziomba...huyu jamaa life ake imevutiaa sana mpka kuja kumsomaa,,, ofcoz wakat tuko pre-form one nakumbuka tulimgusia kidogo pale utawan katikaa shirika la mt Augustino(kituo cha malezi)... Mahanje
 
Hiyo quote yake inapinga zaidi hoja ya kuwepo kwa Mungu kuliko inavyotetea.

Jamaa ni master wa kuji contradict kwa passive aggressive humility.

Na ni mmoja kati ya theologians wakubwa wanaoheshimika.

I personally think Aquinas was deeper than Augustine.
 
Tafuta maana ya - Agano Jipya utaelewa nini kimebadilika!
 
Je Mungu anabadilika
Mungu Habadiliki! Kuna kitu kilitokea ndio maana unaona kuna mabadiliko katika baadhi ya maswala na ndio hicho ninachotaka ukijue baada ya kujuaa maana ya Agano Jipya! Don't be lazy now!!
 
Mungu Habadiliki! Kuna kitu kilitokea ndio maana unaona kuna mabadiliko katika baadhi ya maswala na ndio hicho ninachotaka ukijue baada ya kujuaa maana ya Agano Jipya! Don't be lazy now!!
Sasa kama habadiliki iweje nisome Agano Jipya Wakati la Kale Linatosha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…