Usiwasemee watu..unawezaje kujua kuwa hawajui hao unaowazungumzia..!?
Kwani ni lazima kuwajua,ili kuelewa Umaana wa Maisha?
Acha Majivuno yasiyo ya Lazima.
Napenda unavyosababu,lakini maneno ya namna hii yanaonesha aina fulani ya Udhaifu uliokua nao. Majivuno,kujihesabu kabla Ujahesabiwa.
Yaani wewe na Kukariri kwako huku ukiongeza jitihada kidogo Tu..Ya Unyenyekevu Unatoboza
Siogopi kusema kile ninachoona kuwa ni sawa kwa sababu ya kukuogopa wewe utanifikiri mimi vipi.
Hiyo ni moja kati ya tabia za kijinga kabisa na kikondoo, sijawahi kuwa na tabia hiyo hapa JF na sitaki kuanza sasa baada ya miaka yote hii.
Kama watu, kutokana na maandishi yao hapa (kujibu swali lako nitajuaje watu hawajui maandishi ya St. Augustine) wanaonekana hawajasoma the basic arguments for and against the existence of God, nitasema hilo.
Kama una inferiority complex ya kuona mimi kusema hivyo ni ujivuni, hilo ni tatizo lako la kisaikolojia, si tatizo langu. Mimi nashikilia kusema ukweli tu, sijali ukweli utaumiza vipi ego yako.
Kama kuna cha kubishana, tubishane kama ninachoandika ni kweli au si kweli.
Nishapandishiana mpaka na Invisible hapa, kwa kuwa nilisimamia msimamo wangu, to his credit, alikubali JF ilipopinda na hakuwa na maneno zaidi. Sasa wewe nani utake kunipangia nini cha kusema?
Mjadala ni, je kuna watu wanabishana habari za kuwepo Mungu wakati hata hawajasoma falsafa hii ya kuwapo kwa Mungu hata kwa ngwe ya awali kabisa? Kama wapo, kusema kwamba wapo, kwa kutiliamkazo wajifunze zaidi kablaya kubishana, kuna ubaya gani?
Unachoweza kuona wewe majivuno, wengine wataona ni uwazi tu. Pengine watu wanatafuta cha kusoma zaidi ya Quran na Biblia, na mimi kumtaja tu St. Augustine na hao wengine kunawapa watu pa kuanzia kutafuta kazi zao wasome ili waje na nondo za maana hapa kueleweshana, badala ya kuamini Mungu yupokwa sababu umezaliwa katika familia inayoamini Mungu yupo tu. Hapo kuna ubaya gani kusema watu wengi wanabishana bila kusoma?
Na kama ni kweli watu wanamtetea Mungu bila kusoma kwa undani falsafa za kumtetea Mungu, nitasema hilo. Na wewe huwezikunizuia kwa blackmail ya kunipaka rangi ya ujivuni.
Kama kusema kile ninachoona kweli ni ujivuni, naomba ruhusa nibadili jina nijiite "Mjivuni No. 1". Hiyo itakuwa sifa nzuri kwangu, si mbaya.
Na kuna watu wengi wanabishana na mimi kumtetea Mungu wakati hata hawajamsoma St. Augustune.
Na ingawa ninkweli si lazima kumsoma St. Augustine ili kuweza kujenga hoja, nikibishana na mtu ambaye hajamsoma St. Augustine na faksafa zake kuhusu kumtetea Mungu na mtu aliyemsoma St. Augustine, kuna mambo tutaobgea mara moja tu nabkuelewana, mtu ambaye hajamsoma St. Augustine inaweza kynichukua mwaka kuwa naye pamoja.
Mimi usiniambie habari za kutoboa, huji kama sinatobia, hujui kama kutobia ni muhimu kwangu, hujuibkama nataka kutoboa.
I don't need your fake modesty.
I would rather be real.
Ukweli ni kwamba wabingo watu wengi ninaobishana nao hapa hata Kiingereza, lugha ambayo mijadala hii imeandikwa kwa kina, ni cha manati.
Hata wanaojua hawafuatulii haya mambo na wengi hawajamsoma St. Augustine. Arguments zao, au kukisekana kwa argument kutoka kwao, kunaonesha hilo.
Sasa kwa nini unataka nisiseme ukweli ninaouona na kujifanya nina adabu za uongo?
Adabu za uongo ni kujosa adabu kwangu.
Usitake kunifundisha cha kusema.
Sikohapa kukupendeza wewe au mtu mwingine yeyote.
Kwa nini unataka kunipangia priorities,unipangie kwamba adabu ya uongo ni kitu muhimukuliko kusema kile ambachonakiona ni kweli?
Kwa nini?
Jadili.