Je! Mungu ni yule yule?

Unajuaje kwamba mungu yupo na haonekani na si kwamba hayupo katungwa kwenye hadithi kama Willy Gamba tu na waliomtunga wamesema haonekani?

Kama imani haiendani na logic, utajuaje kama unavyoamini ni ukweli au uongo?

After all, process ya kujua kitu ni cha ukweli au uongo ni logical, si ya kuishia kwenye imani tu.
 
Unajuaje kwamba mambo unayoamini yapo yapo kweli kwa imani tu?

Maana mtu anaweza kuamini kitu kwa kujifariji tu, wakati kitu hakipo. Au, mtu anaweza kuona kitu kwamba kipo akaamini kipo wakati hakipo.

Wewe utajuaje kwamba unavyoamini kipo kwa kutumia imani tu?

Au hujui unalazimisha tu?
 
Mpaka hapo bado hujathibitisha kuwa Mungu yupo, naona unatoka nje ya mada tu
 
Mmeshibaa nyieee mnajadiliii shibee
Shibe na njaa ni ushahidi kwamba mungu hayupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumbaje ulimwengu ambao una wengine wana shibe mpaka bajeti yao ya kulisha mbwa inaweza kulisha kijijini kizima Africa, na wengine wanakufa kwa njaa na Ebola?

Ushawahi kujiuliza hilo?
 
Una matatizo ya akili wewe mtu.
 
Ulivyomuona Nyerere alisemaje?

Unajuaje huna matatizo ya akili yanayokupa hallucinations?

Hujathibitisha mungu yupo.

hhhaaaaa,eti Kiranga huyu Mungu kwanini anatuacha tunateseka na maradhi,umaskini, huzuni kwanini ,mi mwenyewe nishajiuliza sana
 
Halafu Jimena mtu kushindwa kukuthibitisha ndio inapelekea kitu fulani kisiwepo...?! Hii mantiki ya namna hii mmejifunzia wapi...?!
Sasa si tutakuwa vichaa kuamini kitu ambacho hakipo?
Sasa kama kweli hicho kitu kipo kwanini ushindwe kukithibitisha? Unashindwa kwasababu hakipo
 
Ni utumwa mbaya sana kuamini kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, aliyeko kila mahali, nk. Huo ni upunguani na ni upumbavu kukubali hayo.

Tujikomboe na huu utumwa [emoji16]
 
Kwa nini unafikiri kuna kitu kama "mwanadamu wa kwanza" in the first place?

Kipimo chako cha kusema "huyu ni mwanadamu" ni kipi?

sasa sisi ni kina nani na ilikuwaje tukawepo hapa duniani
 
Ni utumwa mbaya sana kuamini kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, aliyeko kila mahali, nk. Huo ni upunguani na ni upumbavu kukubali hayo.

Tujikomboe na huu utumwa [emoji16]

Kuna thread huko tunaambiwa hakuna HIV Bali ni wapiga dili wameturubuni ili wauze dawa arvs ,sasa kila kitu humu duniani tunadanganywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…