Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Kutokuwepo kwake ni aje...?! Wewe unadhani Mungu yupo zizini anaonekana kama wanayama basi usipomuona unasema hayupo...?!

Unazijua sifa za Mungu...?! Sifa yake moja haonekani, halafu yupo mahali pote lakini ni "invisible" yaani unahisi uwepo wake tu...

Kitu kingine imani huwa haiendani na "logic"...
Unajuaje kwamba mungu yupo na haonekani na si kwamba hayupo katungwa kwenye hadithi kama Willy Gamba tu na waliomtunga wamesema haonekani?

Kama imani haiendani na logic, utajuaje kama unavyoamini ni ukweli au uongo?

After all, process ya kujua kitu ni cha ukweli au uongo ni logical, si ya kuishia kwenye imani tu.
 
Nani kasema hayapo...?! Nimeshagundua tatizo lako unaelewa kinyume nyume... hebu rudia kusoma hiyo Waebrania 11:1 na kuendelea huone ulichoongea na chako ni tofauti kabisa...

Kitu kingine unaaamini Yesu aliwahi kutokea Duniani...?! Nataka nikupeleke kwa God Incarnate...
Unajuaje kwamba mambo unayoamini yapo yapo kweli kwa imani tu?

Maana mtu anaweza kuamini kitu kwa kujifariji tu, wakati kitu hakipo. Au, mtu anaweza kuona kitu kwamba kipo akaamini kipo wakati hakipo.

Wewe utajuaje kwamba unavyoamini kipo kwa kutumia imani tu?

Au hujui unalazimisha tu?
 
Jimena hizi ni fact ya kwamba Yesu alitukia hata na kumbukumbu zipo zinaonyesha, fact ni kwamba temple lilikuwepo Jerusalem hata ukienda utapata vithibitisho...

Sasa nashangaa kitu akili yako isipokubali unakiita hadithi... wakati hizo ni fact kabisa na historia zipo za kuthibitisha hilo na sio watu walikaa wakatunga tu...

Hata historia ya BC na AD zinaendana na Yesu, we unadhani watu walikaa wakajitungia tu...?!
Mpaka hapo bado hujathibitisha kuwa Mungu yupo, naona unatoka nje ya mada tu
 
Mmeshibaa nyieee mnajadiliii shibee
Shibe na njaa ni ushahidi kwamba mungu hayupo.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumbaje ulimwengu ambao una wengine wana shibe mpaka bajeti yao ya kulisha mbwa inaweza kulisha kijijini kizima Africa, na wengine wanakufa kwa njaa na Ebola?

Ushawahi kujiuliza hilo?
 
Je , umewahi kujiuliza kwanini watu wengine kabla ya kifo chao wanao uwezo wa kuita watu / Ndugu na kuongea nao , then ndio wanakufa? ( wanao pia uwezo wa kumsubiri hata MTU akiwa mbali)

Je umewahi kujiuliza hiyo pumzi asili yake ni wapi?

Umewahi kujiuliza kwanini ni vigumu sana kwa MTU muovu kusoma Biblia hata nusu page, lakini ukimpa magazeti 30 anao uwezo wa kuyamaliza?

Je una amini kwamba shetani yupo? Una amini kwamba hapo ulipo unaishi chini ya maji kama samaki?

Je una elewa siri iliyopo katika kuzaliwa , kuoa na kufa?

Je umewahi kuushughulisha mwili wako kutafuta, MTU akifa huwa pumzi yake inaenda wapi? Mbona unaweza sana kujishughulisha kwenda kwa waganga na kutafuta wanawake?

Kwanini usitafute ukweli ukawa huru? Nina Amini, mpaka hapo ulipo hauna ukweli wowote; Unaishi tu bila kujielewa; Unashindwa hata na nyumbu , ambae anaelewa nyakati au hata na ndege anaye elewa kiota chake kilipo hata akienda sehemu ya ugenini.

Na Je, umewahi kujiuliza kuhusu moto wa jehanamu? Na paradiso?
Una matatizo ya akili wewe mtu.
 
Ulivyomuona Nyerere alisemaje?

Unajuaje huna matatizo ya akili yanayokupa hallucinations?

Hujathibitisha mungu yupo.

hhhaaaaa,eti Kiranga huyu Mungu kwanini anatuacha tunateseka na maradhi,umaskini, huzuni kwanini ,mi mwenyewe nishajiuliza sana
 
Halafu Jimena mtu kushindwa kukuthibitisha ndio inapelekea kitu fulani kisiwepo...?! Hii mantiki ya namna hii mmejifunzia wapi...?!
Sasa si tutakuwa vichaa kuamini kitu ambacho hakipo?
Sasa kama kweli hicho kitu kipo kwanini ushindwe kukithibitisha? Unashindwa kwasababu hakipo
 
Ni utumwa mbaya sana kuamini kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, aliyeko kila mahali, nk. Huo ni upunguani na ni upumbavu kukubali hayo.

Tujikomboe na huu utumwa [emoji16]
 
Kwa nini unafikiri kuna kitu kama "mwanadamu wa kwanza" in the first place?

Kipimo chako cha kusema "huyu ni mwanadamu" ni kipi?

sasa sisi ni kina nani na ilikuwaje tukawepo hapa duniani
 
Ni utumwa mbaya sana kuamini kuna mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, aliyeko kila mahali, nk. Huo ni upunguani na ni upumbavu kukubali hayo.

Tujikomboe na huu utumwa [emoji16]

Kuna thread huko tunaambiwa hakuna HIV Bali ni wapiga dili wameturubuni ili wauze dawa arvs ,sasa kila kitu humu duniani tunadanganywa
 
Back
Top Bottom