Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Baada ya yesu kuja kwenye agano jipya alitengua sheria ya musa kwenye agano la kale yesu amebadili mambo mengi sana yaliyokua kwenye agano la kale ndo maana unaona tofaut lakini Mungu ni mmoja unaonekana hujui biblia vzur bado tafta watumishi wa Mungu wakufundishe uelewe vzur
 
RGforever said:
Nikisoma Vitabu Vya Dini Hasa Biblia... Mungu wa Kuanzia Kitabu Cha Mwanzo Au Vitabu Vya Kale Ni Tofauti Sana kitabia na Mungu wa Agano Jipya.
Hiki ni kitu ambacho tunakitegemea kutoka kwenye Riwaya ndefu yenye waandishi zaidi ya 40 waliotumia mda wa miaka 1500 kuiandika.

Na kila mwandishi ameshiriki kuiandika hiyo Riwaya katika kipindi tofauti na mtindo/style tofauti

Waandishi wa Agano la Kale,ni tofauti na waandishi wa Agano Jipya.Ndio unaona vinatofautiana kidhima na kifalsafa

Mfano kitabu cha kwanza cha Biblia,kiliandikwa na Musa

Miaka 1500 baadae Yohana akaandika kitabu cha mwisho cha Bibli,Ufunuo

Sasa tofauti ya miaka 1500 si ndogo.Falsafa ya waandishi imebadilika kwa kiasi kikubwa,ndio maana unaona hio tofauti

Na falsafa ya mwandishi ikibadilika katika Riwaya,na tabia ya Main character itabadilika pia

That's why unaona tabia ya Mungu imebadilika

Tabia ya Mungu haijabadilika kwasababu Mungu hayupo.Falsafa ya waandishi ndio iliyobadilika.
 
Mkuu wa chuo said:
Umejuaje...?!
Rational person hawezi kuamini kitu asichoweza kukitetea

Mimi naamini ongezeko la Joto duniani halisababishwi na shughuli za mwanadamu

Au hewa ya Ukaa,kwasababu nina hoja za kutetea imani yangu hio

Na zaidi ya hapo naweza kuthibitisha kuwa Ongezeko la joto duniani halisababishwi na hewa ya ukaa,

Kama nikipewa nafasi

Ukiamini bila kuwa hoja au uthibitisho wewe ni sawa na mtoto mdogo,anayeamini uwepo wa Santa

Pia kuwa na hoja ya kutetea unachoamini na kuthibitisha unachoamini ni vitu viwili tofauti

Ukifatilia huu uzi,Kiranga ameomba mthibitishe kuwa Mungu yupo,mmeshindwa.

Na kuna baadhi wameshindwa kutofautisha hata Bahati na miujiza
[@TheMeek]

Kuingia airport bila passport ni bahati na si miujiza

Kujidunga damu ya mtu mwenye HIV+ na wewe usiathirike si miujiza,ni natural consequence ya HIV/AIDS Denialism.

Sasa mimi siwaombi uthibitisho,mimi nataka mlete hoja zinazotetea imani yenu.
 
Kwa hiyo Mkuu Kiranga huwezi kuamini kuwa Mungu yupo hadi umuone? Tutaaminije kuwa kuna mtu aliitwa Vasco da Gama ilihali hatumuoni. Kama historia iliyo ktk vitabu vya dini ni maneno ya watu tu unatushauri tusiamini historia kwa sababu ni hadithi tu zilizotungwa na watu?
Unataka kutuaminisha kuwa hata wajerumani hawakuitawala Tanganyika kwa sababu kina Gen. Smutts hatuwaoni?
Lakini nyinyi kina Kiranga msioamini uwepo wa supreme being, kama wengine wanavyoita, mna ushahidi gani wa coincidence ya namna hii, kuwa eneo moja watokee viumbe hai wa aina tofauti, wenye uwezo tofauti bila kuwa na mpangaji? Tizama tu ulivyo, macho mawili, Masikio mawili, siyo moja nk. Angalia hizo sense zinavyofanya kazi. Mfumo wa mwili na ubongo, kwamba vitu hivi vijitengeze vyenyewe kwa mpango mkuu kiasi hiki cha kustaajabisha. Hakuna ushahidi wa kisayansi hadi muda huu wa kuthibitisha hayo mnayoyasema. Hakuna pori lolote, mahali popote, ktk Dunia hii, ambapo imegundulika kuwapo na aina yoyote ya kiumbe kinachoanza kujiumba chenye mwelekeo wa baadaye kuja kuwa binadamu au ht Simba. Mfumo wa kujiumba ungekuwepo mfumo huo usingehangaika kutengeneza dume na jike ambao ni very sophisticated. Mfumo ungeendelea kuproduce viumbe kwa njia hiyo hiyo iliyoanza nayo. Kwa vyovyote, mfumo tulio nao wa reproduction ni planned very carefully. Tatizo lenu ni huyo, the great planner, hamumuoni, na nyinyi mnataka ushahidi wa 5 senses, kuona, kusikia, kugusa, kunusa na kuonja. Nyinyi ni sawa na watu waliokuta hoteli kubwa porini, wakaingia ndani, wakakuta kila kitu, wakala, wakaoga na kulala bila kumuona mwenye hoteli. Kesho wakaondoka na kuamua kuwa hoteli ilijijenga yenyewe kwa sababu hawakumuona mjenzi wa Hoteli.
Mpango wa Mungu unatisha, the universe inavyofanya kazi. Mwendo wa kasi wa Dunia ya speed zaidi ya 105,000 kwa saa, haijapungua wala kuongezeka. Na hii ni kuwahi majira ya siku na mwezi. All these are the plans of the Great Being.
Jamani, wakati fulani tunatakiwa kuamini ukuu na uwepo wa huyu Muumbaji na mpangaji Mkuu kwa kuona na kushuhudia uumbaji na ubunifu huu wa ajabu.
Sio lazima Mungu awaeleze kila kitu kuhusu yeye. Sio lazima Baba au Mama yako akueleze kila kitu kuhusu kupatikana kwako. Siyo lazima akuambie mimba yako ilipatikana muda gani, kwa staili gn ya kujamiana.
Wapi nimesema siamini mungu mpaka nimuone?

Au unaamini amini hilo kama unavyoamini mungu yupo? Bila kuelewa?
 
Rational person hawezi kuamini kitu asichoweza kukitetea

Mimi naamini ongezeko la Joto duniani halisababishwi na shughuli za mwanadamu

Au hewa ya Ukaa,kwasababu nina hoja za kutetea imani yangu hio

Na zaidi ya hapo naweza kuthibitisha kuwa Ongozeko la joto duniani halisababishwi na hewa ya ukaa,

Kama nikipewa nafasi

Ukiamini bila kuwa hoja au uthibitisho wewe ni sawa na mtoto mdogo,anayeamini uwepo wa Santa

Pia kuwa na hoja ya kutetea unachoamini na kuthibitisha unachoamini ni vitu viwili tofauti

Ukifatilia huu uzi,Kiranga ameomba mthibitishe kuwa Mungu yupo,mmeshindwa.

Na kuna baadhi wameshindwa kutofautisha hata Bahati na miujiza
[@TheMeek]

Kuingiza airport bila passport ni bahati na si miujiza

Kujidunga damu ya mtu mwenye HIV+ na wewe usiathirike si miujiza,ni natural consequence ya HIV/AIDS Denialism.

Sasa mimi siwaombi uthibitisho,mimi nataka mlete hoja zinazotetea imani yenu.
Heri kidogo wewe unaeleweka, kuliko wengine ni kama kasuku na wimbo wa "thibitisha" na wengine wameiga kuimba wimbo huo huo, hawajui hata niwathibitishie kwa namna gani wanakwambia vyovyote, sasa nitathibitisha kwa keyboard...?!

ulishawahi kusoma elimu ya roho...?!
 
Tatizo lako hujui kusoma au mvivu wa kufikiri, quite possibly so.

Nimesema thibitisha, nikaulizwa vipi, nimesema thibitisha kwa namna iliyo logically consistent.

Lakini wewe kwa sababu kichwapanzi hujaweza kuona hilo, unalalamika kwa jambo ambalo lishaelezwa. Directly kwako.

Roho ni nini?
 
Elimu ya roho au nadharia ya roho?

Mimi nimesoma nadharia ya Roho si Elimu ya roho

Nadharia itageuka kuwa Elimu kama ikithibitishwa kwa majaribio na kukubaliwa na wote.
 
Tatizo lako na wewe sijui ni kichwa panzi...?! Au hukuona, mi nimekwambia utathibitishaje kwa logic kitu kisicho na logic...

Nikakupa mfano kuna logic gani kulisha maelfu kwa samaki wawili na mikate mitano...?! Hukujibu...
 
Kama kitu hadithini hakina logic Unajuaje kwamba kipo? Kama huwezi kuthibitisha, Unajuaje kama ni ukweli au hadithi tu ambayo si ukweli?
 
Elimu ya roho au nadharia ya roho?

Mimi nimesoma nadharia ya Roho si Elimu ya roho

Nadharia itageuka kuwa Elimu kama ikithibitishwa kwa majaribio na kukubaliwa na wote.
Majaribio ya kisayansi...?! Kwa kufanya observation...?! Vitu vingine sio vya kisayansi, na sayansi imeshindwa baadhi ya vitu, mfano Yesu alienda tofauti na sayansi kutembea juu ya maji bila kuzama...

Hivi energy healing huwa ni scientific...?!
 
Kama kitu hadithini hakina logic Unajuaje kwamba kipo? Kama huwezi kuthibitisha, Unajuaje kama ni ukweli au hadithi tu ambayo si ukweli?
Kama kitu na kiishi nawezaje kukuthibitishia wewe...?! Vitu vya hisia nawezaje kukuthibitishia...?!

Kwa mfano nikihisi kitu fulani nawezaje kukuthibitishia huko ulipo madongo kuinama tena kwa kutumia keyboard...?!
 
Ningekujibu vema swali lako laiti kama ningekuwa ndiye mwenye kipawa, lakini bahati mbaya babu na bibi zetu hawakuwahi kuishi na Mungu huyo umsemaye bali waliletewa habari baadaye juu ya uwepo wake. Je, kuna mbegu nzuri ya mihogo inayoweza kutoa ishara nzuri ya hali ya kustawisha migomba ukizingatia kwamba inahitaji maji mengi?
Iko kama unajitambua.......
 
Tukiwa wadogo tulifundishwa kuwa MUNGU ni kama Upepo au Umeme; Upo na wewe wajua upo, lakini hauuoni kwa macho.......ila mambo yake wayajua....
 
Mkuu wa chuo said:
utathibitishaje kwa logic kitu kisicho na logic
Kwanza hakuna kitu kilichokosa Logic/mantiki

Kila tukio lazima liwe na mtiririko unaoeleweka hata kama sio mtiririko wa kawaida

Katika nadharia ya uhusianifu ya Albert Einstein,tunaambiwa mda unaathiriwa na mwendokasi au tungamo

Kwa haraka haraka,unaweza kusema hio nadharia haina mantiki kwasababu mda si kitu kinachoshikika mpaka kiathiriwe.

Lakini ukichimba chini zaidi utaona ina mantiki.

Nikakupa mfano kuna logic gani kulisha maelfu kwa samaki wawili na mikate mitano...?! Hukujibu
Logic inaweza kuwepo,

Lakini Je hilo tukio ni la kweli?

Kuna uthibitisho wowote wa kihistoria nje ya Biblia?

Au ni hadithi?
 
Kama kitu na kiishi nawezaje kukuthibitishia wewe...?! Vitu vya hisia nawezaje kukuthibitishia...?!

Kwa mfano nikihisi kitu fulani nawezaje kukuthibitishia huko ulipo madongo kuinama tena kwa kutumia keyboard...?!
Unaweza kuhusu ambacho sicho.

Unaweza kuona mirage na kufikiri sehemu Ina maji, wakati ni illusion tu.

Ndiyo maana anarudi kwenye logical consistency.

Is the feeling of hunger logically consistent with the functioning of living human beings? Yes.

If you tell me you are feeling hungry, is that conceivable? Yes. Because it is logically consistent with the functioning of a human body.

On the other hand, if you tell me you have never felt hunger, I will have grounds to doubt that because that is not logically consistent with the functioning of human beings.They need to feed.No contradiction there.

There you go, the test of logical consitency neatly applied to a feeling.

Can you show God exist similarly in a way that is not prone to contradiction?
 
Mkuu wa chuo said:
Majaribio ya kisayansi...?! Kwa kufanya observation...?! Vitu vingine sio vya kisayansi,
Kazi ya sayansi ni kuelezea vitu halisi,nje ya hapo sayansi haifanyi kazi

Kama kitu hakiwezi kuelezewa na sayansi,hicho si halisi
na sayansi imeshindwa baadhi ya vitu,
Sayansi kamwe haishindwi,huwa inachelewa kutoa majibu tu
mfano Yesu alienda tofauti na sayansi kutembea juu ya maji bila kuzama...
Tatizo hapa ni moja

Je,tukio la Yesu kutembea juu ya maji ni kweli?

Kuna ushaidi wowote wa kihistoria nje ya Biblia?

Mimi naweza kutunga kisa chochote kinachopingana na sayansi

Naweza kusema,"mwanga wa simu yangu unasafiri kwa kasi kuliko mwanga wa kawaida"

Lakini,je kisa changu ni cha kweli?
Hivi energy healing huwa ni scientific...?!
Energy healing ni Pseudoscience!
 
Unaweza kuhusu ambacho sicho.

Unaweza kuona mirage na kufikiri sehemu Ina maji, wakati ni illusion tu.

Ndiyo maana anarudi kwenye logical consistency.

Is the feeling of hunger logically consistent with the functioning of living human beings? Yes.

If you tell me you are feeling hungry, is that conceivable? Yes. Because it is logically consistent with the functioning of a human body.

On the other hand, if you tell me you have never felt hunger, I will have grounds to doubt that because that is not logically consistent with the functioning of human beings.They need to feed.No contradiction there.

There you go, the test of logical consitency neatly applied to a feeling.

Can you show God exist similarly in a way that is not prone to contradiction?
Huo mfano wako ulioufananisha na illusion, ni sawa sawa na mimi niseme unaweza ukawa unahisi unaunguzwa na moto kumbe ni barafu ndio inakuunguza... hapo utanielewaje...?!

Hivi kwa mfano hapa nilipo nikikwambia nahisi upendo , ukiniambia hebu nithibitishie unategemea nikuthibitishie kwa namna gani...?!

au nikikwambia nahisi nguvu zisizo za kawaida zimenizunguka, ukitaka uthibitisho nitakuthibitishiaje...?!

nikikwambia naona aura unataka nikuthibitishieje...?!
 
Kwanza hakuna kitu kilichokosa Logic/mantiki

Kila tukio lazima liwe na mtiririko unaoeleweka hata kama sio mtiririko wa kawaida

Katika nadharia ya uhusianifu ya Albert Einstein,tunaambiwa mda unaathiriwa na mwendokasi au tungamo

Kwa haraka haraka,unaweza kusema hio nadharia haina mantiki kwasababu mda si kitu kinachoshikika mpaka kiathiriwe.

Lakini ukichimba chini zaidi utaona ina mantiki.

Logic inaweza kuwepo,

Lakini Je hilo tukio ni la kweli?

Kuna uthibitisho wowote wa kihistoria nje ya Biblia?

Au ni hadithi?
Sasa watunge hadithi kwa faida ya nani...?! Ndio maana nakwambia imani haina "logic" ndio maana unaona kama hadithi
 
Huo mfano wako ulioufananisha na illusion, ni sawa sawa na mimi niseme unaweza ukawa unahisi unaunguzwa na moto kumbe ni barafu ndio inakuunguza... hapo utanielewaje...?!

Hivi kwa mfano hapa nilipo nikikwambia nahisi upendo , ukiniambia hebu nithibitishie unategemea nikuthibitishie kwa namna gani...?!

au nikikwambia nahisi nguvu zisizo za kawaida zimenizunguka, ukitaka uthibitisho nitakuthibitishiaje...?!

nikikwambia naona aura unataka nikuthibitishieje...?!
Two words.

Logical consistency. Mbona nishakupa jibu?

Unaweza kuthibitisha mungu in a way that is logically consistent?

Kama huwezi, Unajuaje kwamba mungu yupo?
 
Two words.

Logical consistency. Mbona nishakupa jibu?

Unaweza kuthibitisha mungu in a way that is logically consistent?

Kama huwezi, Unajuaje kwamba mungu yupo?
Najua yupo sababu alishakuja Duniani... mtoto wake... imeandikwa namna hiyo, labda uniambie hizo habari ni za uongo...
 
Back
Top Bottom