Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kwa mfano wako huo ina maana mwenye nyumba endapo atasema nyumba yake haina madawa (kisichokuwepo) je,kauli yake hiyo ndiyo itakuwa ukweli wenyewe kisa tu hawezi kuthibitisha kisichokuwepo?
Maana kuna tofauti ya kusema kitu fulani hakipo na kusema huna uhakika kuwa hicho kitu kipo au hakipo.
Hapana.
Wajibu wa kuthibitisha ni wa yule anayesema madawa yapo. Ndiyo maana polisi wanaosema madawa yapo wanafanya msako. Wakishindwa kuthibitisha kwamba madawa yapo hawana haki ya kusema madawa yapo.
Other than abstracts logical constructs, kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo. Kwa sababu hakipo. Kinachothibitishwa ni kilichopo. Kwa hiyo suala zima la kumtaka anayesema kitu hakipo athibitishe -out of logical constructs- kwamba hakipo ni kutoelewa dhana ya kuthibitisha.
Nimeeleza kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye ameumba ulimwengu huu hayupo.
Kwa sababu ulimwengu huu kuruhusu mabaya kutokea kunam contradict huyo mungu kuwepo.
Kama vile pembetatu isivyoweza kuwa duara ndivyo mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote asivyoweza kuwa kaumba ulimwengu huu.
Unaweza ku reconcile hii contradiction?
Imekuwaje mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?