Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Hata kama nikikwambia sijui jibu, ila ukiniambia jibublake ni Mungu nitajua jibubsi sahihi.

Kama ambavyonunaweza kuniuliza "nini square root ya 2?" nikakwambia sijui.

Lakini nikajua jibu lake si 10.

Kwa sababu square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa kuliko 2. Hiyo itakuwa contradiction.

Hivyo hivyo, jibubla Mungu kwa maswali yakobsi sahihi. Kwa sababu lina contradiction.

The problemnof evil contradicts the existence of God.

Sijui kama umeelewa.

Ukisema Mungu ndiye chanzo cha maisha haya ni sawa sawa na anayesema square root ya 2 ni 10.
nahitaji mawazo yako juu la swala zima la uumbaji basically on ur belief...
 
Sitaki kuamini. Nataka kujua.

Shetani anayesemwa katoka kwa Mungu hayupo. Kwa sababu Mungu hayupo.

Unapoandika "super power" unamaanisha nini?
Ninaposema super power namaanisha nguvu kuu, nguvu kubwa kuliko uwezo wa kawaida wa kibinadamu
 
Deadbody, Biblia inasema kuwa "mpumbavu amesema moyoni mwake kuwa hakuna Mungu.".

Sasa unataka huyo mtu athibitishiwe vipi kuwa kuna Mungu wakati Biblia inamwita mtu wa namna hiyo kuwa ni mpumbavu? Unathubutu vipi kubishana na 'mpumbavu '?

Vv
Biblia inajipinga yenyewe sehemu nyingi sana kiasi kwamba haifai kuchukuliwa kama neno la Mungu.

Quran pia.

Halafu, mpumbavu wa kweli ni yule anayeogopa kuitwa mpumbavu kuliko anavyouogopa upumbavu wenyewe.

Wajanja walijua hili. Wakahusisha kutoamini Mungu na upumbavu ili wapumbavu waogope kuitwa wapumbavu na kuamini kuwepo Mungu kwa jumla jumla kuliko wanavyoogopa upumbavu wenyewe wa kuamini kuwepo Mungu kijumla jumla.
 
Skeptics kama hao hatupotezi muda. Tunawaelekeza kwenye hoja ya msingi. Mambo ya Mungu hayajulikani kwa kuona, kutazama, kuchunguza na mengineyo bali kwa imani. Biblia ibasema wazj ni *********** tu anayesema hakuna Mungu. Yaani "common sense" itakueleza tu Mungu yupo. Philosophy of Religion inadeal na maswali ambayo Kiranga hagusii sasa nipoteze muda wa nini. Aamini tu asisumbue watu humu JF.
ila naona kama kuna haja ya yeye kutuelezeakwa kirefu the other side ambao hatuujui walau uelewa tuupate juu ya ulimwengu wao
 
Tunaporuhusu bongo zetu zitawaliwe na kutaka majibu na ithibati za kidunia kwenye ulimwengu wa roho ndio hapo mkanganyiko unapoanza....
Jambo lolote la kiroho halina ithibati za kisayansi hivyo mtu anapokukazania umthibitishie uwepo wa Mungu nawe ukaanza kubabaika jua umekwisha... Atacheza nawe atakavyo kwakuwa tayari ameshakutega nawe ukategeka
Ww mshirikina huku huna say
 
Skeptics kama hao hatupotezi muda. Tunawaelekeza kwenye hoja ya msingi. Mambo ya Mungu hayajulikani kwa kuona, kutazama, kuchunguza na mengineyo bali kwa imani. Biblia ibasema wazj ni *********** tu anayesema hakuna Mungu. Yaani "common sense" itakueleza tu Mungu yupo. Philosophy of Religion inadeal na maswali ambayo Kiranga hagusii sasa nipoteze muda wa nini. Aamini tu asisumbue watu humu JF.
mpka hapa niwazi umeshindwa kuthibitisha kuwa Mungu yupo ..una amino vitabu ambavyo vinetungwa na watu kama wewe ..tena wakati wanatunga hata hukuwapo unajuaje kama hawakuvifanyia editing nakuingiza maneno ambayo waliyapendekeza wao wenyew "" ninani ambaye alikuwa nishuhuda akiona roho mtakatifu akiwaa hadithia hizo habari hao ambao walioziandika ..!?? tuwe tunajipa muda wakujifanyia tafakuri aiseee ...sipingi uwepo wa Mungu "" lakini naamini sio huyu aliyetajwa ktika hvi vitabu vyetu. Mungu wa kwenye hivi vitabu amejaa udahifu mnoo ..tunaambiwa kuwa NI Mungu anaye tupenda hapo hapo anawaacha watu wanakufa kwa vimbunga.. matetemeko ..wanaokufa wanaacha mayatima na wajane wasio jua hatima ya maisha yao ..matokeo take wanaishi kwa mateso na manyanyaso huku Mungu anayetupnda na muweza wa yote akiwatizima tu "" huyu Mungu anaye tupenda na muweza wa yote anashindwa vipi kuondoa uwepo wa ISIS KULE SYRIA ..KWANINI ASIIFNYE CONGO IWE NA AMANI ..HUYU MUNGU ANASHINDWA NINI KUWAONDOA BOKO HARAMU NIGERIA ..kama hayo bado yanafanyika huku tunaamini kuwa Mungu yupo na anatupnda ..nitakuwa siko sahihi endapo nikihoji huo upendo na uwezo wa yote alionao dhidi Yetu ....
 
"Maandiko yanasema Mungu ni Roho"

Ili uweze kumuelewa lazima uwe mtu wa kiroho pia. Huwezi kutaka kumthibitisha Mungu kisayansi na aonekane kiuhalisi kama huyo jamaa atakavyo ndio shida ilipokuwa pamoja na wachangiaji walivyomjibu

Lakini hiyo haina maana Mungu hayupo laa Mungu yupo na tunamthibitisha kupitia neno lake maana yote aliyoyasema tunayaona yalitokea yanatokea na yatatokea.
Ukitaka kumuamini Mungu unatakiwa uipuuze sayansi??
 
"To the one who has faith, no more explanation is needed, to the one who has no faith even in more explanation can not understand "-St. Thomas Aquinas.
Umeona hiyo nukuu kwa vile ni ya kiingereza ina mashiko?? Bado haina hoja na ndo yaleyale mnayajibu kila siku
 
HAKUNA ANAYEWEZA KUMJIBU KIRANGA HOJA ZAKE ....WOTE WANAOJARIBU KUZIJIBU WAMEKUWA WANAISHIA KUONGEA BLAAA BLAA TU "''Jamaa ana maswali mazito mtu ambayo mtu mwenye upeo mdogo hawezi kung'amua kitu
"Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu. ..."Zaburi 14;1b

Kama unafahamu maana ya nomino mpumbavu basi hata sababu ya kujibu hoja za kipumbavu nao ni upumbavu na anayefanya hivyo naye pia ni mpumbavu.

Vv
 
Kama kitu hakipo. Unaanzia wapi kuthibitisha kwamba hakipo?

Uthibitisho wa aina gani utakufaa kuonesha kwamba kitu hakipo?

Nikikwambia pembetatu yenye pembe sita ipo, ila wewe huijui na huna akili za kuiona tu (wakati kwa kweli haipo), utanithibitishiaje kwamba haipo?

Aliyeua kwa kisu unaweza kutoa ushahidi wa alama za vidole zake ukasema huyu kaua kwa kisu, kisu kimepatikana eneo la mauaji kina damu, kina alama zake za vidole, jeraha lililoua limetokana na kisu hiki, huyu ambaye alama zake za vidole zipo kwenye kisu hana alibi.Zaidi kuna video imemrekodi akiua. Zaidi, nyumba ina alarm na ikajifunga milango, polisi wakaja wakamkuta muuaji ndani. Jirani walimuona dirishani akiua.

Overwhelming evidence. Huyu kaua.

Sasa kama hakuna aliyeua kwa kisu, utathibitishaje kwamba hakuna aliyeua kwa kisu wakati hakuna maiti, hakuna kisu, hakuna alama za vidole?

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, kama alivyoandikwa katika vitabu vya Biblia na Quran, hayupo.

Hayupo kwa sababu, dhana nzima ya kuwepo kwake, inajipinga yenyewe.Contradiction.

Dhana ya kuwepo kwake inajipinga yenyewe, kwa sababu, kwa upande mmoja, Mungu huyu ni mtakatifu sana kiasi kwamba kibaya chochote hakiwezi kutoka kwake. Kwa maana hiyo, angekuwepo, dunia isingewezekana kuwa na mabaya. Ukisema aliumba dunia isiwe na mabaya ila Shetani ndiye akaleta mabaya, nitakuambia hata huo uwezo wa Shetani kuweza kuleta mabaya ni ubaya ambao Mungu mwenye utakatifu unaosemwa hatakiwi kuwa nao.

Kwa hiyo, utaona kwamba, kuwepo kwa mabaya, na zaidi, kuwezekana kuwepo kwa mabaya katika dunia hii, ni uthibitisho kwamba Mungu huyu hayupo.

Wengine wamejaribu kujibu kwa kusema Mungu kaachia mabaya ila katupa uwezo wa kuchagua mabaya na mazuri. Hili ni jibu lisilo na mantiki. Ukiwa na mtoto wako mchanga ambaye uelewa wake ni mdogo sana, na wewe una helewa mkubwa sana kujilinganisha naye, unampenda, utampa chupa ya maziwa na pembeni umuwekee chupa ya sumu ili tu aweze kuchagua anachotaka? Hapana. Utahakikisha nyumba nzima haina sumu anayoweza kuifikia. Utampa maziwa tu.

Sasa kama binadamu mwenye uwezo mdogo, upendo mdogo na ujuzi mdogo anakataa kumpa mtoto wake mchanga maziwa na sumu ili mtoto awe na uhuru wa kuchagua, imekuwaje Mungu huyu mnayemsema mwenye uwezo usio na mwisho, ujuzi usio na mwisho na upendo usio na mwisho ameruhusu ulimwengu uwe na mazuri na mabaya ili watu wawe na uhuru wa kuchagua tu?

Watu kama wangeumbwa katika dunia ambayo haiwezekani kuwa na mabaya na mabaya hata hayajulikani, in fact hayapo kabisa hata kidhana, wangekosaje uhuru wa kitu ambacho hakijulikani wala kufikirika wala kuwepo kidhana tu?

Huyu Mungu yupo kweli au hadithi tu?

Kaachia dunia yenye magonjwa, vita, matetemeko, mafuriko, njaa, umasikini, kuteseka etc, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hivyo vyote haviwezekani watu wakaishibraha mustarehe.

Kwa nini?

Sijajibiwa jibu la kueleweka kwenye swali hili.
ni vile akili ya kibinaadamu na kufananisha na Mungu, lkn sawa hivi ndivyo Mungu anavyochuja kati ya pumba na mchele maana ww si wa kwanza ktk fikra ulizonazo hata farao alikuwa na fikra ka zako au pengine kukuzi lkn now imebaki historia hakika mwisho wa watu dizaini hii ni mbaya mno, "Mungu atuongoze tuwe wenye kutenda mema"
 
"Mpumbavu amesema moyoni, hakuna Mungu. ..."Zaburi 14;1b

Kama unafahamu maana ya nomino mpumbavu basi hata sababu ya kujibu hoja za kipumbavu nao ni upumbavu na anayefanya hivyo naye pia ni mpumbavu.

Vv
neno mpumbavu sihata mimi naweza kukwambia tu "" kwahiyo kwakuwa limetoka kwenye Bible basiii umehadaika ..empty set kabisaa
 
Hata jua lina nguvu kubwa kuliko uwezo wa binadamu. Jua ndilo linalo support maisha katika dunia hii. Likizimika maisha yote yatakufa.

Hilo nalo unalihesabu kama ni super power?
Namaanisha nguvu zaidi ya hilo jua.

Hata unaposema jua lina nguvu zaidi ya binadamu sio ukweli moja kwa moja, kwani binadamu pia ana nguvu kuliko jua kwenye maeneo flani flani (kumbuka nguvu simaanishi misuli, simaanishi physical strength pekee). In a way kuna mambo binadamu anaweza fanya lkn jua haliwezi.

Sio jua tu, hata maji, yanasapoti maisha katika dunia hii

Hata hewa pia.

Turudi kwenye swali la msingi, najua umelielewa...... Je unajua/unaamini kuna nguvu kubwa zaidi ya uwezo wa kibinadamu?

Hapa ndio PA kuanzia
 
Kama mtapenda kupata ufahamu mnaweza kusoma kitabu cha Hawking: The Brief History of Time baadhi ya majibu Hawking anayajibu! It is piece written by Genius who is also a Nobel Prize Laurent! The degree of abstraction and sophistication of this book is so high but some answers to Mkuu Kiranga are found in this piece!

Nimependa critical arguments za Kirenga! Taabu sisi wanadamu hupokea mambo yaliyoanzishwa na watu wengine duniani bila kuuliza critically ili kufahamu!

Juzi tu Rwanda Kagame amefunga makanisa zaidi ya 600! Argument ni kuwa kwa nini makanisa mengi sana yanafunguliwa Kigali na siyo Visima vya maji, hospitali au shule?
 
ni vile akili ya kibinaadamu na kufananisha na Mungu, lkn sawa hivi ndivyo Mungu anavyochuja kati ya pumba na mchele maana ww si wa kwanza ktk fikra ulizonazo hata farao alikuwa na fikra ka zako au pengine kukuzi lkn now imebaki historia hakika mwisho wa watu dizaini hii ni mbaya mno, "Mungu atuongoze tuwe wenye kutenda mema"
Kabla ya kusema akili za kibinadamu kufananisha na Mungu, unajuaje Mungu yupi kwa akili hizo za kibinadamu?

Nikikwambia kuna pembetatu yenye oembe sita ambayo kwa akili za kibinadamu huwezi kuijua, ila aminintu ipo, wakati haipo, utathibitishaje kwamba haipo?

Nikikwambia dhana ya huyo Mungu wako kuwepo haina tofauti na hii pembe tatu yenye oembe sita, utathibitishaje vinginevyo?
 
View attachment 714415



View attachment 714416

View attachment 714419

View attachment 714421


View attachment 714422

View attachment 714425
View attachment 714428

View attachment 714430

View attachment 714438

View attachment 714444

View attachment 714445

View attachment 714446


Mkuu anahoja za msingi mzijibu kwa ustaarabu tu msimtukane huku hamna jibu mlililolitoa.Sasa mtumishi wa Mungu unatukana wazi tu halafu mpagani Kiranga ndio anakwambia usitukane jibu tu kistaarabu.Hapa kuna tatizo

Mjitokeze mjibu kwa hoja na akiamini ataenda kuongeza Kanisa

Yeye mwenyewe pia ameshindwa kuthibitisha kama aidha yupo au hayupo!
 
Back
Top Bottom