Mnasema Mungu ana ujuzi wote, upendo wote na uwezo wote.
Mnasema Mungu anajithibitisha mwenyewe.
Kuna wanaosema yupo, apparently amejithibitisha kwao.
Kuna tunaokataa. Hajajithibitisha kwetu.
Inakuwaje Mungu huyu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote, awapendelee wengine kwa kujithibitisha kwao, halafu wengine atutuoe, asijithibitishe kwetu?
Tukikosa kumjua na kufariki na dhambi (kwa sababu hajajithibitisha kwetu), suku ya hukumu akituuliza kwa nini nyinyi mlinikana nanhamkunioenda, tykasema Mungu wewe mwenye uwezo wote, unayepanga yote, hukutuoa neema ya kujithibitisha kwetu, atasemaje?
Hivi mzazi anaweza kumnyima mtoto nafasi ya kujifunza kusoma, halafu mtoto akishindwa kujua kusoma, mzazi awe na haki ya kumuadhibu mtoto kwa sababu mtoto hajui kusima?