Je! Mungu ni yule yule?

Je! Mungu ni yule yule?

Nimekuuliza na wewe Thibitisha mwanzo Wako..
Kwanza nijibu swali langu la kuthibitisha Mungu wako yupo, au kubali huwezi kuthibitisha kwamba Mungu wako yupo.

Hutakiwi kukataa kunijibu swali langu halafu ukataka mimi nikujibu swali lako.
 
Kwanza nijibu swali langu la kuthibitisha Mungu wako yupo, au kubali huwezi kuthibitisha kwamba Mungu wako yupo.

Hutakiwi kukataa kunijibu swali langu halafu ukataka mimi nikujibu swali lako.
Hahahaa Si Jambo Baya Mtu Kuulizwa Swali na Kujibiwa na Swali! Mara nyingine Swali Huwa ni Jibu La Swali! Haya Mzee Kiranga Kwa Hekima narudia, "Thibitisha mwanzo wako"
 
Hahahaa Si Jambo Baya Mtu Kuulizwa Swali na Kujibiwa na Swali! Mara nyingine Swali Huwa ni Jibu La Swali! Haya Mzee Kiranga Kwa Hekima narudia, "Thibitisha mwanzo wako"
Ungekuwa unajua kusoma ungeona swali hili lishajibiwa.

Ila swali langu kukutaka uthibitishe uwepo wa Mungu hujalijibu.
 
Kama Sijui Kusoma nawezaje Kuwasiliana na wewe kwa maandishi?
Hilo swali unauliza kwa sababu hujui hata "hujui kusoma" maana yake ni nini

Hujui tofauti ya muktadha wa kusoma kwa ufahamu na kusoma kielimu ya ngumbaru ni nini.
 
Hilo swali unauliza kwa sababu hujui hata "hujui kusoma" maana yake ni nini
Sijakuuliza Swali Hilo Nimekuuliza "Uthibitishe Mwanzo wako" Usipate Taabu Kama Huelewi Vizuri sema Hata "Sijui" Au Kama Una Jibu Thabiti Nieleze Nijue,

Maana Umeshasema Mtu akikudanganya Wewe unajua, Sasa Hebu Kata Mzizi wa Fitna Hapa Kwa Wale ambao Huwa wanatuletea Habari Eti Wameumbwa na Mungu!

Najua wewe Unajua Jibu, Maana Kama Wanadanganya wewe Unajua, Tuambie "Source Yako ni Nini"?
Au Tupe kanuni Ya kujua source Yetu Ili Tufanye Hesabu wenyewe, Kama Source ni Hisabati
 
Nataka kurudi mwaka 1982, siwezi kurudi mwaka huo, kwa sababu nimepangiwa tayari kwamba muda unaenda mbele tu, haurudi nyuma.

Sasa kama naishi katika ulimwengu ambao muda unaenda mbele tu, haurudi nyuma, na mimi nataka kurudi nyuma kwenye muda, siwezi, utasemaje nina freewill?
Nani kakukataza kurudi nyuma. Wewe unahesabu vipi muda? Nani kakuambia kuwa hicho kipimo unachopimia muda kiko sahihi? Nikikuambia sasa hivi unaelekea huko ulikozaliwa taratibu kama wish yako ilivyo utabisha? What is reality to you really?
 
Thibitisha Mungu yupo.

Kwenye hili la kurudi nyuma katika muda unathibitisha kichaa chako tu hakuna kingine hapo.
 
Hata nikikwambia sijui majibu ya maswali haya yote. Hilo halithibitishi Mungu yupo.

Ni kama vile unaniuliza sauare root ya 2 ni nini?

Hata nikisema sijui. Ukiniambia jibu ni 10.
Nitakwambia jibu hilo ni la uongo. Si la kweli. Maana lina cintradiction.

Mungu ana contradiction. Hivyo hata kama sijui maisha ni nini, yalianzaje, jibu la Mungu ni contradiction.

Uovu kwanza kabisa ni hali ya kuleta maumivu, kukosa furaha, ubaya, kitu usichotaka kufanyiwa, bila haki.

Mathalani. Mtu kuuawa bila hatia ni jambo ovu.

Pia, watoto wachanga kufariki inasikitisha sana. Ndiyo maana dunia nzima watu wanafanya jitihada kuzuia vifo, hususan vya watoto wachanga.

Sasa inakuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, akaumba ulimwengu na kuruhusu matetemeko ya ardhi kwa mfano, yanayoua watoto wachanga na kuwafukia hai?

Huyu Mungu kwa nini mkatili hivi? Hahurumii hata watoto wachanga? Alishindwa nini kuumba ulimwengu ambao hauna matetemeko haya?

Yupo kweli? Au ni wa hadithi tu? Mbona anaachia viumbe wake wapate uchungu sana kwa kuondokewa na ndugu zao?

Imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaumba ulimwengu ambao maovu na mabaya mengi sana yanawezekana, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Mbona ulimwengu huu tunaouona uko tofauti sana na huyo Mungu anayesemwa? Mbona ulimwengu unampinga? Unam contradict?

Mbona inaonekana huyo Mungu ni kama katungwa kwa hadithi za kitoto ambazo ukizipima kwa logic zinaonekana za uongo?

Hakuna hata mtu mmoja anayesema Mungu yupo ambaye ameweza kujibu swali hili.
Unaweza kumuoa dada yako au mkakubaliana kuwa wapenzi?

Au mama yako let's say she have raised you as a single mother, Je ukikua unaweza kumuomba muwe wapenzi??

Na kama hauwezi ni kwa nini? Kwani hii nayo inaingia katika katika maana zako za kutambua uovu?
 
Thibitisha Mungu yupo.

Kwenye hili la kurudi nyuma katika muda unathibitisha kichaa chako tu hakuna kingine hapo.
afadhali sasa kichwa kinaanza kupona. kama unaanza kujua mwingine ni kichaa basi ujue unapona. utapona tu kwa neema.

Now let's go back to your question/assertion
Sina freewill.

Nataka kurudi mwaka 1982, siwezi kurudi mwaka huo, kwa sababu nimepangiwa tayari kwamba muda unaenda mbele tu, haurudi nyuma.
Nani huyo amekupangia tayari kwamba muda unaenda mbele tu, haurudi nyuma?
 
Kuna watu hawaamini Mungu yupo na hawataki kuwafanyia wengine mabaya.

Na kuna magaidi wanaua watu kibao kwa kutumia jina la Mungu.

Ukiwa unaogopa kufanya mabaya kwa kumuogopa Mungu, wewe wema wako unatokana na uoga. Huna wema wa asili ya kwako mwenyewe.

Ukifanya wema wakati unajua hakuna Mungu, mbingu wala pepo, umefanya wema kwa kutaka tu kwa sababu wewe mtu una asili na akili ya kupenda mema, wema wako ni wa asili kwako mwenyewe.

Anayefanya wema kwa kumuogooa Mungu na kutaka pepo anafanya wema wa biashara. Anafanya wema ili apate faida ya kupata pepo na kuepuka moto.

Anayefanya wema huku anajua hakuna Mungu, pepo wala mbingu, anafanya mema kwa asili yake.

Niko na waamini Mungu kibao katika kundi moja. Mwenzetu ameumwa mpaka anataka kufa. Watu wanajibalaguza. Mimi nisiyeamini Mungu nikawa wa kwanza kutoa msaada.

Wanaoamini Mungu wamebaki kuwa wanaamini kwa jina tu.

Mtu asiyeamini Mungu ndiye katokea kufanya kama anayeamini Mungu anavyotakiwa kufanya.

Kwa hiyo usikariri tu kwamba kutoamini Mungu ni kufanya mabaya na kuamini Mungu ni kufanya mazuri.

Mimi kutoamini Mungu kunanichochea kufanya mazuri zaidi.

Ningeamini Mungu ningeweza kukuta mtu anaumwa anataka kufa nikasema ni kazi ya Mungu, tumuombee tu. Nikasepa. Au nikasema huyu Mungu anamuadhibu.

Lakini sasa hivi siamini Mungu nikiona mtu anaumwa, nasema hakuna Mungu wa kumsaidia. Ni wajibu wangu mtu mwenzake nimsaidie maana hakuna Mungu.
Big up sana mkuu kwa majibu yako yaliyoshiba.Usife moyo,endelea kutoa shule japo cognitive dissonance bado imewalevya baadhi ya watu humu na hivyo hwataki kurudi kwenye njia waliyoanza kupotea wakajipanga upya.Natamani na mimi ningekuwa na uwezo huo wa kujibu kwa usahihi kama ufanyavyo wewe haya mambo.
 
Shetani ndiyo nini,jibu maswali mazuri ya Kiranga.
Mimi siamini kuwepo kwa Shetani wala Mungu.

Mtu ananiita agent wa shetani. Shetani hayupo. Kwa sababu Mungu hayupo.Anayemtaja Shetani hawezi kuthibitisha Mungu yupo. Hawezikuthibitisha Shetani yupo. Nitakuwaje agent wa kitu ambacho hakipo?

Wakati yeye anayeamini Mungu yupo na Shetani yupo anakuwa karibu zaidi kuwa agent wa huyo Shetani kuliko mimi nisiyeamini hata kuwapo kwa Shetani.
 
Big up sana mkuu kwa majibu yako yaliyoshiba.Usife moyo,endelea kutoa shule japo cognitive dissonance bado imewalevya baadhi ya watu humu na hivyo hwataki kurudi kwenye njia waliyoanza kupotea wakajipanga upya.Natamani na mimi ningekuwa na uwezo huo wa kujibu kwa usahihi kama ufanyavyo wewe haya mambo.
Cognitive dissonance kubwa sana.

Tatizo walio na hii cognitive dissonance wengine iko so subconscious hata hawajijui. Inakuwa natural kama kupumua. Hata mtu kalala anapumua bila kujua kwamba anapumua. Na hii cognitive dissonance yao hivyo hivyo.
 
Hivi jamani kama maumbile yamekuja nature bila kuumbwa na mungu mbona yana mfanano, kwa mfano binaadam wote tuna maumbile yaliyofanana, wote tuna macho pua mdomo na yote yapo kichwani hoja yangu ipo hapa kwanin hii nature haikufanya macho yakawa makalioni, kwanin pua haikukaa kwenye nyayo kwanin tunatia chakula mdomoni lkn kinatoka mk...... jamani ndo kweli nature imefanya yote haya maana ukijiangalia mwanaadam ulivyoumbwa kwa ustadi lazma ujue kama yupo alie kuswarif hivyo kiranga vp
Nadhani hujui kinachoongelewa hapa.Nani aliyesema kuwa hayo maumbile yametoakana na nature!!?

Kiranga ameshasema hajui.Na kutokujua kwake usimlazimishe aamini kuwa tumembwa na fulani wakati hata hata kwa akili ndogo tu inagoma.
 
Naomba nijaribu kujibu swali na mtoa uzi ambalo linamtatiza.
Sikumbuki imeandikwa katika kitabu gani ila Yesu mwenyewe alipo ulizwa na mafarisayo kuwa mbona mafundisho unayotufundisha ni tofauti na yale ya manabii kama musa na Eliya akawajibu sikuja kutengua tolati bali nimekuja kutimiliza maneno ya unabii.
 
Nataka kusikia habari za kuamini, lakini kuamini kuwe ni njia ya kuelekea kujua.

Kusiwe mwisho wa habari.

Kuamini kukiwa mwisho wa habari, unaweza kuamini chochote.

Sasa, katika muktadha huo, unaamini kwamba kuna pembe tatu hiyo yenye pembe sita?
Una maana gani kusema kuamini kuwe njia ya kujua?

Hebu fafanua mkuu maana kushindwa kuelewana huku ndiyo sababu za hii mijadala kutokuisha.
 
Sijakuuliza Swali Hilo Nimekuuliza "Uthibitishe Mwanzo wako" Usipate Taabu Kama Huelewi Vizuri sema Hata "Sijui" Au Kama Una Jibu Thabiti Nieleze Nijue,

Maana Umeshasema Mtu akikudanganya Wewe unajua, Sasa Hebu Kata Mzizi wa Fitna Hapa Kwa Wale ambao Huwa wanatuletea Habari Eti Wameumbwa na Mungu!

Najua wewe Unajua Jibu, Maana Kama Wanadanganya wewe Unajua, Tuambie "Source Yako ni Nini"?
Au Tupe kanuni Ya kujua source Yetu Ili Tufanye Hesabu wenyewe, Kama Source ni Hisabati
Nilimuuliza swali linalofanana la lako, kwamba atuambie "what is the source of life and diversity of all life forms", hakujibu pia akakaa kimya.

Mi nadhani ni vizuri pia akiwa anajibu maswali anayoulizwa, sio kukimbia swali kwa kujibu kwamba hata nikisema source ya life ni nn, haimaanishi Mungu yupo.

Kiranga hakubali kwamba kuna elimu ambayo hana na ujuzi ambao haujui. Na anaamini kwamba kili ujuzi unafahamika kwa njia moja tu kama ambavyo anatoa mifano yake ya square root ya 2.

Kuna vitu ambavyo vina contradict nature totally na vipo vina exist. Nakupa mfano wa species moja ya samaki (jina nimesahau) ambao wana uwezo wa kubadili jinsia toka ya kike na kuwa dume (and vice versa) na kuweza kutoa mbegu zinazorutubisha mayai ya samaki jike. Naamini hili hukuwa unalijua, na unaweza ukabisha pia. Lakini ni kitu ambacho logically haki-make any sense.
 
Naomba nijaribu kujibu swali na mtoa uzi ambalo linamtatiza.
Sikumbuki imeandikwa katika kitabu gani ila Yesu mwenyewe alipo ulizwa na mafarisayo kuwa mbona mafundisho unayotufundisha ni tofauti na yale ya manabii kama musa na Eliya akawajibu sikuja kutengua tolati bali nimekuja kutimiliza maneno ya unabii.
Sasa mtu anafanya tofauti, halafu anakwambia hajaja kutengua, hiyo inaingiaje akilini?

Swali la imekuwaje Mungumuweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana mpaka sasa halijajibiwa.

Mathalani. Imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wite na uoendo wite aumbe ulimwengu ambao unaruhusu matetemeko ya ardhi yanayofukia watoto wachanga na kuwaua?

This aspect of nature contradicts that God to the extent that we can logically say that that God does not exist.
 
Back
Top Bottom