Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hatuwezi kujadiliana kama hutaki kujibu maswali.Sidhani kama hapa tupo kwenye chumba cha mtihani,nachojua hapa tunajadiliana. Tatizo umejielekeza ushindani wa ubishi na mie sipo hapa kushindana na wewe kuonesha ni nani mbishi au ana maswali magumu.
Sioni haja ya kunilazimisha kujibu tu maswali wakati nimeshajieleza,kama unaona kuna nilipochanganya elezea hiyo sehemu.
Eleza ni vp nimekosea kwa kulinganisha dodoma na imani ya kuchomoza jua kuliko kunilazimisha nikujibu tu maswali.
Nitakuelewa vipi kama maswali yangu hutaki kujibu?