kiranga mbona unarukaruka sana? Ni nimeomba unijibu ndiyo au hapana umekimbilia kwenye kitu kipya, muda. Unasema kuwa kitu kimoja ili kiongoze kingine kunahitajika uwepo wa muda ambao kiuhalisia haupo kwa hiyo hatuwezi kusema Luna kitu kinachoongoza kingine. Uliposema kuwa The Second Law of Thermodynamics inaiongoza dunia na unaniforce nikubali kuwa kama The Second Law of Thermodynamics ni Mungu. Hiyo The Second Law of Thermodynamics inaiiongoza dunia na vilivyomo kwa kupitia kanuni zipi? Na umesema kuwa kimoja kuongoza kingine ni kitu ambacho hakipo.
Muda haupo.
The Second Law of Thermodynamics ndiho kitu kinachofanya muda uonekane upo, hivyo, kila kitu kinachokuwa ndani ya muda ya kuweza kuwa na muda, kinaendeshwa na The Second Law of Thermodynamics (entropy).
Soma kitabu cha Dr. Stephen Hawking "A Brief History of Time: From The Big Bang To Black Holes". kuna sura moja inaitwa "The Aarrow of Time" inaelezea kwa lugha nyepesi sana kwa nini muda unaonekana upo na kwa nini muda unaenda mbele tu na haurudi nyuma.
Tusome tuelewe sababu za mambo, sio kuyapa jina tu "Mungu" kabla hata hatujayaelewa.
Kwa sababu ukianza kurahisisha tu kwamba "kinachoongoza maisha ndiyo Mungu" utakuja kuambiwa kwamba hiyo dhana nzima ya kitu kimoja kusababisha kingine, tunayo kwa upofu wetu tu wa large scale universe.
Aat the quantum level, causality as we know it breaks down. Cause and effect is violated.
Sasa hapo utaona kwamba msingi wako mzima wa kufikiri kwamba kuna Mungu, dhana ya kwamba kuna kilichosababisha, unavunjwa.
Kwa sababu causality and cause and effect is no longer necessary or central to existence.
Ndiyo maana ukifikiria haya mambo bila kujua na kuchunguza mambo kwa kina, unatoa jibu la kuchekesha kwamba chochote kitakachokuwa chanzo ni Mungu, katika ulimwengu ambao hauhitaji na wala hautambui habari nzima ya chanzo na matokeo ya chanzo.
Kungelea "chochote kilichoanzisha na kinachoongoza ni Mungu" kwa muktadha huu, ni sawa na kusema "rangi ya wimbo wa taifa ni bluu".
Ni sentensi ambayo inaumbika, lakini haina maana.
Unaelewa kwamba hizi habari zinaweza kuwa tofauti, tofauti, tofauti, tofauti kabisa na namna nzima ya kufikiria tuliyozoea?