Je, muungano wa Tanganyika na Zanzibar upo kwa vigezo vipi?

Umeandika majibu tupu!
 
Ukiwa na wazanzibari utakuta wanalalamikia muungano, wanasema wanapunjwa kwenye muungano. Hawana nafazi UN. Hawana sarafu etc.
Ukiwa na wapogoro huku bara wanalalamikia wazanzibari wanatunyonya, hatuwezi kununua ardhi kwao, ukiwa unafanya kazi Zanzibar ubaguzi nje nje ilhali sisi huku hatuwabagui kwa namna yoyote.
Ukiwa na wanasiasa wanasema muungano umetusaidia Sana.
Wasomi wako njia panda.
Kwanini Sasa tusipige kura tuone Kama wengi ndio wanautaka au wengi wanauponda.
 
Muungano ni mzuri, ila huu tulionao sio Muungano, ni unyonyaji! Tunaataka Muungano wa kweli chini ya Rais mmoja!
 
Kwa sasa hakuna Muungano bali ukoloni.
 
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 
Zipi Ni faida za muungano huu?
Zipi Ni hassra zake?
Huu sio Muungano, ni utegemezi nanunyonyaji. Faida kwa Zanzibar nimeziorodhesha kwenye uzi, hasara kwa Tanganyika nimeziorodhesha pia
 
1. Ajira za serikali huku bara Wazanzibari wana asilimia yao imetengwa kila zinapotoka na lazima wapewe.
2. Tunatumia fedha moja, TZS.
3. Jeshi la polisi moja.
4. Vyama vya siasa viko pande zote.
5. Mwenge wa Uhuru unaenda hadi Zanzibar
6. Kule kuna majimbo ya uchaguzi ambapo hutoka wabunge na wanachaguliwa wakati wa uchaguzi na wanakuja huku bara vikaoni.

Haya ndio mambo yaliyopo kwenye muungano tunayoyajua sisi. Ndani huko hatuambiwi. Inawezekana hata Tanganyika inatoa pesa kuipa Zanzibar na sisi hatujui na ni siri za serikali. Si unaonaga wanaapa kutunza siri za serikali.

Kwa ufupi, Tanganyika ni kama mwanaume anayehenyeka na kukomaa ambakishe dem ambaye anamkataa. Kwa kufosi mambo ndio maana Tanganyika inaonekana hakuna inachopata, Zanzibar yenyewe imekaa pale inasema kama hutaki basi.
 
Haahaha, hakuna muungano hapa, Zanzibar ni kupe!
 
Muongo mkubwa Wazanzibari hawautaki Muungano hata leo wanaomba uvunjike na iko siku utavunjika. .Watanganyika ndio vinganganizi wa Muungano na faida kubwa wanapata wao Tanganyika .Nyerere alimtisha Karume kama hutaki kuungana utapinduliwa ,hakuna hata Mzanzibari mmoja alieulizwa kuhusu Muungano .Huu Muangano zaidi upo kisiasa na kuizibiti Zanzibar katika Dini na maendeleo mengine.Tanga la wanyika kubalini jina lenu na kuweni na nchi yenu nyinyi mungeungna na Kenya or Uganda .By the way Zanzibar ndio iliowafundisha Tanganyika Ustarabu mulikuwa hamuvai nguo kama huyajui waulize watu wanaojua,
 
Inaelekea wewe ni raia wa Zanzibar.

Hongera kwa kulipenda Taifa lako la Zanzibar.
 
Inaelekea wewe ni raia wa Zanzibar.

Hongera kwa kulipenda Taifa lako la Zanzibar.
 
Tanganyika inafaidika vipi na hiki kinachoitwa Muungano?
 
Nyinyi Wazanzibari ni wanafiki tu. Sasa kama hamuutaki huu muungano, si muendeshe kura ya maoni ili mjitenge. Maana kwenu ni rahisi zaidi kufanya hivyo kuliko upande wa Tanganyika.
 
Nyinyi Wazanzibari ni wanafiki tu. Sasa kama hamuutaki huu muungano, si muendeshe kura ya maoni ili mjitenge. Maana kwenu ni rahisi zaidi kufanya hivyo kuliko upande wa Tanganyika.
Wanamwogopa Rais wa Tanzania.
 
undefined Muungano.! Haieleweki mpk watu tunazeeka na kufa aileweki maana yake. Karne hii ya uwazi! Tunaona mwisho wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…