Mkuu hizo issue si za kweli ni mistori ya kutunga tu.
Hivi unajua Yesu ali wahidi wale watu walioishi kipindi chake kuwa angerudi kabla wao hawajafa?.......yaani angerudi kabla ya kufa kwa wale waliokuwa wakimsikiliza.
Mat. 16:27-28, Kwa maana mwana wa Adam atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hamtaonja mauti kabla ya kumwona mwana wa Adam akija katika ufalme wake.
Huu utabiri wa Yesu kwenye Mathayo 16:27-28, ulifeli mara baada ya vifo vya waliokuwa wakimsikiliza unless kama kuna watu walioishi nyakati za Yesu ambao watukuwa hai hadi hivi sasa.
Kuna watu walioishi nyakati za Yesu walioamini kuwa angerudi kabla wao hawajafa lakini hadi leo ni miaka 2000 hajarudi.
Ufufuo plus ujio wa pili ni kama hekaya za Abunuasi, endeleeni kusubiri mkiamini atakuja.,.....lakini kaeni mkijua hakuna kitu kama hicho.