Je Mwanadamu atafufuliwa akiwa na Umri Gani?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamaa wew upo upande gani
f1955856f524010a88b5dbf93ebdbf84.jpg
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Biblia haijaeleza sana kuhusu ufufuo but Quran imeeleza kwa kirefu.Nakuja na aya za kutosha
 
Wanadamu wt wtafufliw wkiwa na umri swa na maumbo swa na umri ni umrialiokaa na bii Issa alayhima ssalam ambao ni miaka 33 kwa mujbu wa (Qua'n)
nilikua nasubiri aya kwenye bible kuhusu hili lakini inaonekana hakuna hivyo bible ipo nyuma ya kur an kwa mambo mengi tu
 
I don't know where you are, but it would be absurd for me to presume that you are not alive simply because I don't know where you are!
Ndio umemjibu vizuri chamilton kwamba hujui Yohana alipo kwa sasa kwa nn unashindwa kuamini kwamba hakuna ufufuo maana aliwaambia wanafunzi wake kwamba bado kitambo kidogo tu anakuja akaenda moja kwa moja!!
 
Hakuna jibu hata kwenye Qur'an maana Qur'an ilikoti kwenye biblia kama tourat zaburi na injili
 
Habari zenu wana JF Poleni na Mihangaiko ya Dunia hii.

Okay leo nina swali kuhusu suala la siku ya kufufuliwa wanadamu wote. (Kwa wale wanaoamini kua baada ya kifo kuna siku ambayo tutafufuliwa)

Ningependa kufahamu

Je mwanadamu atafufuliwa akiwa na umri Gani?

kama atafufuliwa na umri aliokufa nao je wale wabibi ambao wamekufa hawaoni, hawana meno, wanajisaidia vitandani vipi watafaidi huko peponi?

Na je mtoto mchanga akifufuliwa hivyo hivyo nae atafaidi vipi ufalme wa mbinguni?

Asanteni.

c3cc96485cee8ffd6ca6ee0c73532b78.jpg
Wakati wa ufufuo miili tuliokuwa nayo( yenye kuharibika) itabadilishwa na kupewa miili mipya isiyoharibika!
 
Siku ukifa ndo siku utakua unazaliwa upya hospital.peoples hatutaisha duniani
 
Mkuu hizo issue si za kweli ni mistori ya kutunga tu.

Hivi unajua Yesu ali wahidi wale watu walioishi kipindi chake kuwa angerudi kabla wao hawajafa?.......yaani angerudi kabla ya kufa kwa wale waliokuwa wakimsikiliza.

Mat. 16:27-28, Kwa maana mwana wa Adam atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hamtaonja mauti kabla ya kumwona mwana wa Adam akija katika ufalme wake.

Huu utabiri wa Yesu kwenye Mathayo 16:27-28, ulifeli mara baada ya vifo vya waliokuwa wakimsikiliza unless kama kuna watu walioishi nyakati za Yesu ambao watukuwa hai hadi hivi sasa.

Kuna watu walioishi nyakati za Yesu walioamini kuwa angerudi kabla wao hawajafa lakini hadi leo ni miaka 2000 hajarudi.
Ufufuo plus ujio wa pili ni kama hekaya za Abunuasi, endeleeni kusubiri mkiamini atakuja.,.....lakini kaeni mkijua hakuna kitu kama hicho.

Injili haikuwa kwa Wale waliokuwa katika nyakati za yesu tu! Bali hata waliokatika wakat pia ujao!! Hivyo yesu hakumaanisha kwa wale waliopo,pia hii ndio maana dhahiri ya kusema Kuwa ujio wake utakuwa wa ghafla!
 
Wacha kupotosha wewe! Mimi nimenukuu maandiko ya injili, Yesu anawaambia wafuasi wake hawatakufa kabla ya yeye kuja.

Je hadi leo wapo? Yesu alisharudi?...........Kitu kipo wazi lakini unataka kupotosha kisa ni ukweli mchungu?
 
Muda ndio Jawabu la kweli.

Wanadamu hupenda kujua mambo wasio yajua.

Hujihangaisha katika ukosefu wao.

Kama vile ukivyokuwa hujui mambo mengi ukiwa unanyonya maziwa ya mamaako na sasa unajua chembe ndogo ya ujuzi. Basi hata hayo mambo yapo na yapo mbioni kumjia kila mwenye nafasi naam ndio pumzi ya uhai
 
Ulivyokufa ndivyo utafufuliwa.ila wapo watakaofufuliwa kwa maumbo tofauti tofauti.ila umri ule ule.
Ndugu yangu kumbe nayo majina hutia upofu.Sihitaji kujua kama wewe ni mkristo au vinginevyo ila itoshe tu kukuambia siku ya ufufuo kitakachofufuliwa ni roho na sio mwili.Mwili utarudia mavumbi ila pumzi ya Mungu aliyokupulizia na ndio roho ataihitaji kwa ajili ya hukumu.
 
Mkuu hizo issue si za kweli ni mistori ya kutunga tu.

Hivi unajua Yesu ali wahidi wale watu walioishi kipindi chake kuwa angerudi kabla wao hawajafa?.......yaani angerudi kabla ya kufa kwa wale waliokuwa wakimsikiliza.

Mat. 16:27-28, Kwa maana mwana wa Adam atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kadiri ya matendo yake. Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hamtaonja mauti kabla ya kumwona mwana wa Adam akija katika ufalme wake.

Huu utabiri wa Yesu kwenye Mathayo 16:27-28, ulifeli mara baada ya vifo vya waliokuwa wakimsikiliza unless kama kuna watu walioishi nyakati za Yesu ambao watukuwa hai hadi hivi sasa.

Kuna watu walioishi nyakati za Yesu walioamini kuwa angerudi kabla wao hawajafa lakini hadi leo ni miaka 2000 hajarudi.
Ufufuo plus ujio wa pili ni kama hekaya za Abunuasi, endeleeni kusubiri mkiamini atakuja.,.....lakini kaeni mkijua hakuna kitu kama hicho.
Siku moja sawa na dk 1 kwa mungu unaeona ni mda mrefu bas pole yako subiri na ujanja fake tanuri la moto linakusubir!
 
Ndugu yangu kumbe nayo majina hutia upofu.Sihitaji kujua kama wewe ni mkristo au vinginevyo ila itoshe tu kukuambia siku ya ufufuo kitakachofufuliwa ni roho na sio mwili.Mwili utarudia mavumbi ila pumzi ya Mungu aliyokupulizia na ndio roho ataihitaji kwa ajili ya hukumu.
So nawataoenda motoni kumbe watachomwa roho? Roho ni nini? Je ni pumzi ka ulivyoielezea? Na je roho inaweza ikafeel phyisical pain?
 
Mkuu hizo issue si za kweli ni mistori ya kutunga tu.

Ipo simulizi huko Asia Ndogo kuwa wakati Yohana Mpendwa mwanafunzi wa Yesu alipokuwa mzee sana, wanafunzi wake Kama vile Polikarpo wa Smyrna, walimchukua kumpeleka makaburini kama alivyowaagiza. Kufika huko akawaambja wachimbe kaburi. Nao wakachimba. Kisha akawaagiza wamwingize mule kaburini. Wakamwingiza na kumlaza kifudifudi. Akawaambja wamfukie kwa udongo, yaani wamzike. Wakabisha, akawaambja nifunikeni kitambaa usoni kisha mnifukie Kwa udongo. Wakafanya hivyo na kuondoka. Walipofika mjini wakasemezana 'hivi hatukumzika mtu angali hai jamani?" Si alituagiza mwenyewe na kutuambia kisha tuondoke? Hebo turudi jamani. Waliporudi kule makaburini na kuchimba mahali pale hawakupata mtu. Walichimba zaidi lakini hawakuukuta ule mwili wa Yohana walioufukia pale. Sasa wanahistoria wanaulizana huenda hii ndiyo ilikuwa maana ya Yesu kuwa hataonja mauti? Ipo nadharia kuwa Yohana hakufa isipokuwa Mungu alimtwaa kwa namna hiyo.
 
Haya maelezo ya kufufuliwa ni simulizi zaidi. Sasa ina maana baana ufufuo kutakuwa na kuamkina? Maana itakuwaje kwa wazee, watoto na vijana? Na je kuhusu me na ke itakuwaje?
 
Habari ya kuambiwa changanya na ya kwako
 
Ipo simulizi huko Asia Ndogo kuwa wakati Yohana Mpendwa mwanafunzi wa Yesu alipokuwa mzee sana, wanafunzi wake Kama vile Polikarpo wa Smyrna, walimchukua kumpeleka makaburini kama alivyowaagiza. Kufika huko akawaambja wachimbe kaburi. Nao wakachimba. Kisha akawaagiza wamwingize mule kaburini. Wakamwingiza na kumlaza kifudifudi. Akawaambja wamfukie kwa udongo, yaani wamzike. Wakabisha, akawaambja nifunikeni kitambaa usoni kisha mnifukie Kwa udongo. Wakafanya hivyo na kuondoka. Walipofika mjini wakasemezana 'hivi hatukumzika mtu angali hai jamani?" Si alituagiza mwenyewe na kutuambia kisha tuondoke? Hebo turudi jamani. Waliporudi kule makaburini na kuchimba mahali pale hawakupata mtu. Walichimba zaidi lakini hawakuukuta ule mwili wa Yohana walioufukia pale. Sasa wanahistoria wanaulizana huenda hii ndiyo ilikuwa maana ya Yesu kuwa hataonja mauti? Ipo nadharia kuwa Yohana hakufa isipokuwa Mungu alimtwaa kwa namna hiyo.
Tangu nizaliwe leo ndio nimesikia hiki kitu ulichosema.

Hebu tueleze haya mambo uliyapata wapi?..........Binafsi nadhani ni propaganda za kutengenezwa ili zi-fit utabiri wa Yesu ambao haukutimia.
 
Back
Top Bottom