Je, Mwanamke anaweza kuwa sababu ya umasikini kwenye familia?

Je, Mwanamke anaweza kuwa sababu ya umasikini kwenye familia?

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
901
Reaction score
3,112
Imezoeleka familia ikiwa tajiri basi ni baba, na je? mwanamke anawezaje? kusababisha umasikini ndani ya familia?

Naongea hivo kwasababu mm nikipanga malengo ila kila ukizuka ugomvi mipango yote inaharibika.

Swali la ujumla ni je familia isiyokuwa na amani je inaweza kuwa na maendeleo?
 
Absolutely Yes 💯
 
HAPANA.
Mipasuko na kutoelewana ndan ya family huuwa umoja hata kiroho pia.

na ni mbaya zaid ukute nyota ya mwanamke ndo inayomsapoti mwanaume kupata mafanikio.
maana yake ukikorofishana nae tu ama kuachana nae, ujue mipango yako itafeli vibaya.
 
Ndiyo maendeleo yanaweza kuwepo, hio ni imani tu. Mfano mengi hakuwa na maelewano na mkewe akaenda kumuoa jack wa kigoma lakini maendeleo bado alikuwa nayo. Kukaa kusema mara mwanamke anagundu huo ni imani tu, we tengeneza mirija ya pesa vizuri, ishi vizuri na jamii inayokuzunguka na usisahau kutoa zaka utajionea mwenyewe.
 
Pole sana kijana, unafuga jini la umasikini ndani kwako, piga chini haraka sana.
 
Short story:

Kabla mwanaume hajaoa alikuwa na bidii ya kuboresha nyumba ya kiiijini kwao wanakoishi wazazi wake.
Baada ya kuoa, akaingiwa na uzito, haoni hela inakokwenda, kazi mkataba ukaisha kabla hata hajaoa, baada ya kuoa akawa anacheza kwenye biashara za familia ila pesa haijai na haoni inaenda wapi na akitafuta ajira anachagua sanaa.
Matokeo yake mke ndo akawa anabeba gharama za familia maana mke alikuwa na ajira kabla hawajaoana na baada ya kuoana.
Mke hakuwa na vitega uchumi zaidi ya ajira ya kudumu, baada ya kuolewa mke ndo alikuwa anabadilisha magari ya familia, mume akawa hajielewi pesa yake haionekani, hakuwahi nunua gari kwenye familia.
Watoto walipokuwa wakubwa mke kachoka vimbwanga vya mume akakimbia ndoa na akachukua watoto. ( mume alikuwa mlevi asiyejijali, mkorofi akilewa, gubu, ugomvi usio na kichwa wala miguu, na umalaya).
Baada ya kuachana mwanaume ndo kujiokota akaanza kujenga nyumba yake kuanzia chini peke yake, akanunua kiwanja kingine karibu na akawa na shamba mahali. Mke akabaki kuhudumia watoto shule chakula mavazi na kujigharamia kodi na gari huku akiendelea na ajira ya kudumu.
Mke alinunua viwanja viwili ila hakujenga sababu pesa yote alisomeshea watoto shule za maana.

Mwanaume anaishi nyumba ya kisasa nzuri well finished fully furnished na hawajarudiana hadi leo watoto wako na mwanamke na mke hakuwahi omba wala kudai hela ya matumizi wala shinkumi ya mwanaume kujimudu na watoto.

Mwanaume hajawahi hata siku moja kusema chukueni hela hii ya nguo za sikukuu au gharama ya shule au isaidie chakula nehii....

Hapo nani mwenye GUNDU?

NB: Mind you, hii ni true story.
 
Back
Top Bottom