Je? Mwanamke anayejiuza anaweza kuwa mke mwema zaidi ya yule ambaye hajiuzi?

...malaya anawezaje kuwa mke wajameni?

....hamkomi tu hadi mnakuta wake zenu "vitandani" na marafiki zenu?na mnajua wazi mliwakuta wapi...!

Wee wako umemkuta bikra? Kama siyo bikra unajuaje kama alikuwa hajiuzi? Unajua definition ya kujiuza ni pana sana, na karibu sehemu kubwa ya wanawake tunaooa hivi sasa walishalala na wanaume zaidi ya kumi kabla ya kuolewa, sasa sijui huyu utamtofautisha na yule aliyeamua kujiuza rasmi.

Kumbukeni pia wapo wanaojiuza kwa shiniikizo, wapo wanaojiuza kwa kuwa maisha ni magumu na wanatafuta namna ya kupata chochote kwa ajili ya kutunza familia zao, kwa mfano namfahamu dada mmoja kutoka makete, ambaye hakuwa na baba wala mama, na aliachiwa wadogo zake wapatao watut akiwa darasa la sita tu. Hakuwa na namna ya kuwalea wadogo zake, ikamlazimu aingie kwenye kujiuza ili apate ada za wadogo zake na chakula nyumbani. Thank God hivi ninavyoongea mmoja wa mdogo wake amemaliza university (DUCE), and thank God yule dada sasa amepata mme wa maana na wanasaidiana kusomesha wadogo waliobaki ambao wengi wapo secondary.

Tuwe makini tunapotoa hukumu dhidi ya hawa watu. hakuna mwanamke mwenye akili timamu na mwenye staha anayefurahishwa na shughuli ya kujiuza. Ulizia kila mmoja utatambua ana sababu inayomfanya afanye hivyo. Vinginevyo awe ni mvuta bangi ambaye hana hata fikra juu ya maisha yake ya baadaye. Ninachokiona hapa mwanamke yeyote anafaa kuwa mke as far as ametubu na kukubali hilo jukumu la kuwa mke. Maana tukitaka kujua alikuwa anafanya nini kabla ya wewe kumpata basi unaweza kujikuta hata uliyenaye sasa alishafanya biashara ya kujiuza. maana baada ya bikra kutoka, hakuna tena ushahidi wa alishafanya ngono mara ngapi na katika mazingira yapi.
 
Umalaya ni tabia ya mtu, unaweza ukamuoa na ukampa kila kitu lakini bado akajiuza kwa thamani ndogo tu hii yote coz yeye ni tabia yake, na unaweza ukamnunua changudoa baada ya kumtuamia ukamuoa na kumpa kila kitu na akawa mke mwema, labda huo uchangudoa aliufanya kwa shinikizo tu na sio tabia yake.
 
mpaka leo na utu uzima wangu sijui maana ya Malaya?
Ni lugha ya watu wa Malaysia. Lolz!

Ninakubaliana na wewe kabisa Mkuu, na ninajibu kwa sababu sikuona kitufe cha Thanx.
Kwa nyongeza ya maelezo yako, kama mmoja alivyouliza, bora kwanza tungelifafanua maana za mke mwema na mke mbaya (sio kwa sura nadhani).
Ikiwa kwa mke mwame tunakusudia yule anayeheshimu ndoa yake na kuwa mama watoto mzuri, baadhi ya hawa wanaojiuza (tusiwaite malaya) wanaweza kuwa wake wema zaidi ya baadhi ya wasiojiuza, kwani kama wengi walivyosema hapa, umalaya ni tabia inayokwenda mbali zaidi ya hivyo kujiuza.

Tukumbuke na kukubali kuwa wengi wa wanaojiuza wanafanya hivyo kwa shida, na wengi wao huwa wanataka kutoka katika lindi hilo lakini hawana jinsi. Tukumbuke pia tendo lenyewe la kujiuza ni kujidhalilisha, na wao wenyewe wanajua hilo kwani ni binadamu, wana hisia, wanahitaji upendo kama binadamu (mwanamke yeyote). Ni wanawake kamili kama walivyo wanawake wote, kwa hivyo wanapopata watu wanaopendana nao, na wakahakikisha kuwa wanapata mahitaji yao muhimu bila ya kujiuza, wengi hutoka huko na kuanzisha familia kwa upendo.
 
Inawezekana haswa! Ila kama anafanya hivyo kama kazi na kaa ukijua asilimia kubwa ya machangu wana wapenzi wao na wengine hata wameolewa na wanafanya hiyo kazi kwa kujificha na unakuta kwenye mahusiano yao hali ni shwari tu!
 
Inategemea mkuu kwani hakuna kanuni juu ya hili.
 
hilo ni point la maana sana.
 
Du ! kwa kuwa maana ya "mke mwema " ni pana na subjective, sishangai kuhusikia haya ,
Ila kwangu mimi , once a bitch alwayz a bitch, na kuwahi tu kuwa malaya ni tayari dosari kuwa mke mwema
 
Kujiuza kwenyewe ni very subjective terminology. Kuna ambao wanajiuza na hawajui kama wanajiuza- hawa wengi wao wanaongozwa na dhiki na wanaweza kuwa wake wazuri, na kuna ambao wanajiuza na wanajua kama wanajiuza hawa wamekaa kibiashara zaidi na kama ukimpata wa aina hii mjomba utapata shida.
 
Mkuu tunaomba mrejesho plz...
 
mada moto moto haaaa haaa leo niingia Jf kujikumbushia enzi zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…