Je, mwenyekiti Mbowe ni mtu huru?

Sasa mkuu unataka waingie barabarani.

Nyerere asingekaa na wakoloni unadhan tungepata uhuru mwaka gani.
Mkuu Tanzania haikuwa koloni la Uingereza, bali uingereza alikabidhiwa kututawala hadi tuwe tayari kujitawala. Waingereza hawakuwahi kuwa na uchu wa kuitawala Tanzania, vinginevyo tusingepata uhuru wa maongezi. Huo uhuru tulipewa na UN baada ya Nyerere kwenda kusema tuko tayari, kumbe naye alitaka atutawale hadi afie madarakani. Kwa bahati mbaya aliharibu uchumi katika kiwango kilichomfanya aone aibu hadi kung'atuka.
 

Mbowe alichemsha baada ya kumpokea Lowassa, kwa sasa haamini kuwa hastahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA, ndio maana anajaribu kila njia ili ahakikishe anapata sifa kwa CCM baada ya kupoteza ushawishi kwa wafuasi wa CHADEMA.
 
Ni mfungwa huru kwasababu kesi ilimalizwa kwa mashart ndio maana alipotoka tu lupango kaenda moja kwa moja kuookea maagizo
 
Kama kawasahau wewe si una Mdomo? Kwani Mvowe kazaliwa kuwasemea nyie? Alivyo.kamatwa ulitoka hadhalinu kulaani?
 
Muacheni Mbowe maana hata akisema muingie barabarani mnajificha anabaki anateseka yeye na familia yake, mna ushujaa huku kwenye key board, amejaribu kila njia kuitsha maandamano, kupinga utawala na kususia uchaguzi lakini kila anachofanya mnamkebehi sijui mnataka afanye nini

Hebu kama mnaona ni rahisi nyie watanzania mnaohisi kusalitiwa anzisheni chama chenu muwapiganie watanzania wanyonge
 
Historia ndo utoa taharifa kamili ya mtu alivyo, mbowe ni muhuni tu kwa taharifa yako fupi alikuwaga Dj pale bilcans club,fatilia historia za watu aina ya mbowe utapata jibu.

Kuna mwenye proof kuwa huyu bwana alikuwa dj?
 
Kwamba CCM atawapa nchi kwa mazungumzo .
 
Wajasiliasiasa. Huwa wanakuwa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…