Je, na wewe uliziona ndege 12 zikitembea kwa mstari jana usiku?

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Usiku wa jana mida ya saa moja kuelekea saa mbili niliona ndege 12 zikiwa zinaenda taratibu sana kwa mwendo wa Pole zikipita kwenye anga la nyumbani kwangu Bahari Beach.

Mara ya kwanza nilidhania ni vimondo, ila nikasema hapana, nikadhania sasa haya ndio mambo ya UFO yenyewe, lakini baadaye nikaona ni ndege 12 zikitokomea taratibu.

Vipi huko kwenu mliziona?
 
Ni tofauti na zile za majuzi maana kuna mdau aliripoti humu kuziona mitaa hiyohiyo akasema ni setelaiti za Starlink
 
Wanadai ni satellite za starlink za bwana Elon Musk kwa ajili ya maswala ya kimtandao zaidi.
 
Ni satellites za internet 🛰️ ya StarLink za bwana mkubwa Elon Musk... Nchi nyingi tu huwa zinaonekana hata huko Marekani na nchi zingine za ulaya wanazionaga...
 
Ni satellites za internet [emoji2930] ya StarLink za bwana mkubwa Elon Musk... Nchi nyingi tu huwa zinaonekana hata huko Marekani na nchi zingine za ulaya wanazionaga...
Yaani ni Bora umenitoa wasiwasi maana hata Sisi huku Mbweni JKT mida ya saa mbili usiku kilichonishangaza ni ule mpangilio yaani nikasema kweli haya ni maajabu.... halafu in ten seconds zikapotea Ila kwa sisi wageni ile hali inatisha sana. Itabidi niwaambie majirani zangu maana nao walipata hofu.
 
Ni satellite za starlink, sasa mtaanza kuziona mara kwa mara ziko kwenye orbit yenu sasa , wachina na Amazon nao soon mtaanza kuziona pia, ninapoishi tumeanza kuziona almost 2 years sasa, big business lakini scientists wameanza kulalamika ni uchafuzi wa anga
 
Yeees, ilikuwa ni kopi ya treni ya SGR kwa ajili ya wale ambao hawakuiona mchana, mama ameupiga mwingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…