incognitoTz
Senior Member
- Apr 19, 2019
- 133
- 172
Wataalamu na watafiti wa elimu ya mendeleo ya watoto wadogo wanaamini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya maendeleo ya ubongo hutokea kati ya kipindi cha umli wa mwaka mmoja (1) hadi miaka mitano (5). Hiki nikipindi muhimu sana kwa mtoto na hapa huwa anajua kipi kizuri kufanyiwa na kipi kibaya kufanyia watu wengine. Kati ya miaka sita (6) mpaka nane (8) mtoto huwa anajifunza wastani wa maneno mapya ishirini (20) kwa siku, hiki ndio kipindi mtoto huwa anaanza kudevelop msimo na mitazamo juu ya watu na mambo yanayo mzunguuka na ndio kipindi kwa hapata nchini kwetu watoto huanza shule za msingi.
Mimi huwa naamini mtoto mdogo ni kama kompyuta mpya wewe ndio muamuzi wa mwisho ya namna unavyotaka uifanyie kazi, ukitaka mtoto akuchukie maisha yake yote, ukitaka mtoto akuhusudu, ukitaka mtoto apende shule ama ukitaka aichukie shule ni kipindi hiki. Hapa ndio mtoto huwa anaelewa kila unachomfanyia huwa unamaana gani.
Sijajua hawa wasasa lakini kipindi mimi nipo shule, walimu wengi walikuwa wanapenda kuona wao ndio most civilized people kwenye jamii, walikuwa na kiburi na maneno mengi ya karaha kwa wanafunzi, walimu walikuwa wanafanya watoto kama watumwa wao kwa kuwatumikisha sio kwenye mazingira ya shule tu bali hata majumbani mwao, walimu walikuwa wanaburuta watoto kwa viboko bila ya kuwaonea huruma yeyote ile.
Hawakujua walikuwa wanapandikiza nini katika maisha ya hawa watoto ambao baadhi yao watakuwa watu wanaoamuwa mambo muhimu huko maishani mwao hapo baadaye. kuna visa vingi sana ambavyo navikumbuka kuhusu walimu, ila vitu ambavyo sitaweza kusamehe ni utoaji wa adhabu zenye lengo la udhalilishaji mbele ya wanafunzi wengine ukiambatana na upendeleo kwa watoto wao ama wa ndugu zao, na hakuna kitu ambacho kilikuwa kinaniudhi kama kuwapo kwa Collective punishment kitu kinachopelekea baadhi ya watu kupata adhabu kwa makosa yaliyo tendwa na watu wengine.
katika survey ambayo nimeifanya randomly kwa watu mbali mbali kwenye maeneo ya kazi na kwa marafiki ambao sikuwahi kusomanao shule moja, watu nane (8) kati ya kumi (10) huwa wanaonesha kuwa wamebeba chuki dhidi ya walimu waliowahi kuwafundisha, wengine wanaenda mbali zaidi kufikia hatua ya kuwadhihaki kwa maneno kama "Karma is a Bitch".
Walimu wengi huwa wanaamini watoto wasio penda walimu ni wale watukutu na hawana ufauru darasani, lakini kuna wanafalsa wanaamini kuwa haukuna mtu mwenye akili anayefanyakazi serikalini na hata akiwepo, biashara zenye nguvu zitamuajiri kwa pesa nyingi, hii inamaana watu wanaofanyakazi serikalini ni hawa watoto wasikuwa na ufauru ama waliokuwa watukutu na walikuwa wakipokea vipigo na manyanyaso makubwa kutoka kwa walimu wao.
Hapa nchini Tanzania watumuishi wa umma kwenye kada ya uwalimu ndio wanaoneka kuwa na mazingira ya kufanyia kazi magumu na duni. Watu wengi wanadhani kuwa hakuna watu ambao wapo tayari kutetea manufaa ya walimu. Mimi binafsi naanza kushawishika kuwa hali hizo duni zinaweza kutokana na chuki na visasi kwa walimu kutoka kwa wanafunzi wao wa zamani .
Je na wewe unadhani Uhusiano mbaya kati ya walimu na wanafunzi ni moja ya chanzo cha kuwapo kwa maisha magumu kwa walimu? Piga kura yako hapo juu.
Ama unamtazamo mwengine? Changia hapo chini.
Kwa mnaoshindwa kuvote kwenye mobile app, vote NDIO au HAPANA kwenye reply