Wana JF huyo Mdada anahitaji ushauri
Mimi ni msichana wa miaka 29 nina elimu ya form 4 na nikasoma Secretary VETA miaka 2 pamoja na Computer n.k Nikabahatika kupata kazi kwenye kampuni binafsi mpaka sasa hivi nina miaka 9 katika hiyo kampuni nikapandisha vyeo mbalimbali ila nafanya kwa ujuzi tu hizo kazi na sio kwa vyeti na mshahara wangu sasa hivi ni 1.million pamoja na marupurupu yote (Nimeelezea haya ili niweze pata ushauri unaofaa kwa kulinganisha kipato na hali halisi ninayoishi.) nina uhusiano na kijana mmoja hapa na nikazaa nae mtoto mmoja wa kiume ana miaka 2 sasa..tatizo kijana mwenyewe ni jeuri/dharau/hana upendo kabsaa na kikubwa zaidi yeye ana elimu ya darasa 7 na hata ufahamu wake ni mdogo yaani kazi anayofanay ni biashara za hapa na pale elimu kwangu sio issue muhimu ni Upendo n.k Japo anaonyesha nia ya kunioa lakin mmmh NIMESHINDWA.
Kwa bahati mbaya/nzuri nikakutana na kijana mwengine mtanzania ambae anaishi Marekani nae amezaa mtoto 1 wa kiume lakin bado hajaoa ..na ana passport ya Marekani (nimetoa hizo detailz ili mtakaponishauri mjue mnaanzia wapi) ..tulikuwa tunachat kwenye mitandao yaani tukawa tunapenda kama vile tumeonana..mpaka mwaka jana alipokuja tz tukaonana na kila mtu akaridhika na mwenzie .kwa kweli nina mpenda sana tu nay eye pia anaonyesha kunipenda ILA TATIZO NI KWAMBA HATA NIKIWA NA SHIDA HUWA NAIELEZEA KWAKE KAMA STORY YA KAWAIDA TU ILI WALAU ASEME OK NITAKUTUMIA PESA..HASEMI WALA HAJAWAHI NISAIDIA NA NA HATA UKITAMKA PIA ANASEMA HANA Ila hapa Dar es salaam amejenga nyumba nzuri tu amenipeleka pia kuiona n.k.
Kilichonifanya kuwauliza....ni hili Sasa hivi anataka kunioa ila yeye ni dini nyingine lakin nilipomwambia amesema yuko tayari kubadili kuja kwenye dini yangu Na anataka anioe na kwenda kuishi marekani na amesema atanitafutia Shule na mtoto pia atasoma n.kk na yeye pia ni msomi na ana kazi nzuri tu, na ni mpole sana, ana busara, ni mwepesi kuomba msamaha na hapendi nikasirike hicho ndicho nilichogundua kwa miaka 2 niliyomfahamu kwa kuongea na simu na miezi 3 alokuja tz tukawa pamoja.
1. SWALI LANGU NI HILI: JE KAMA HUYU MTU ANA UWEZO WA KUNIPELEKA U.S.A MIMI NA MTOTO NA AKATUSOMESHA SOTE IWEJE SHIDA NDOGO NDOGO TU ZA HAPA ANASHINDWA NITATULIA????? (Japo sehem kubwa ya maisha na mudu mwenyewe lakin kwasabab najenga huwa nakwama hapa na pale kibinadamu)
2. JE KWA MTAZAMO WENU HASA AMBAO WANAISHI U.S.A KITU KAMA HICHO KINAWEZEKANA KUMUDU MAISHA YA KUMSOMESHA MTU NA MAMA YAKE??
3. NA KAMA HAKUFANYA AKANIDANGANYA JE NITAFANYAJE????? (Naogopa kufanya tamaa kisa nimesikia Nje baadae nikajuta).\
4. Na kama ni kweli ATATUMIA UTARATIBU UPI WA MIMI NA MTOTO KUISHI PALE BAADA YA VISA HALALI KWISHA??
Niko njia panda naomba mnishauri Matusi na kejeli pia ntapokea Ila nitashukuru kwa wale wote watakaonipa hali halisi ya maisha ya U.S.A kulingana na story yenyewe NAKUWA NA WASIWASI SABAB KAMA NITACHEMSHA NA NIKAWA SIJAPATA CHANCE YA KUSOMA NIKIRUDI TZ NAJUA KAZI YANGU SITAIPATA TENA NATAKA KUJUA KAMA NADANGANYWA AU HIVI VITU VINAFANANA NA UKWELI. NIKO NJIA PANDA....NAHITAJI USHAURI WA UKWELI NIFANYEJE?
Ni kweli, if it were me, I would simply take atleast 2 months leave and not quit my job, maisha ya ughaibuni si sawa na bongo, lakini zaidi maisha ya kukaa wawili sio sawa na mlivyokuwa mbalimbali, japokuwa wanawake hatutakiwi kuwa tegemezi, there's no harm in she seeking or expecting some help...its expected of tht man to provide..naomba sana usiache kazi kabla hujatest zaliNafkiri kwamba sasa inakubidi ,uangalie kwanza maisha ya mtoto wako, pili akuakishie kama kipato chake kinatosheleza mahitaji yenu watu 3 + kuwasomesha ww na mtoto ,na sio akuoe alafu ukawe maza house ,lazima ufanye kazi kama alivyo kukuta ,usije ukajikuta unaondoka peponi na kuelekea motoni,maisha ya ulaya ni magumu asikudanganye mtu,kama anakupenda kweli akuthibitishie
Hilo,asije kuwa drugs dealer kule akutie matatizoni.x
Form 4 ... Amefanya kazi miaka 9... Analipwa Net 1,000,000/= : You must be very lucky!
Achana na mapenzi, jiendelezi kelimu!