Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

Je, nani anapokea mahari kwa binti aliyelelewa na mama pekee?

mkushite

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2021
Posts
666
Reaction score
1,619
Huyu binti kalelewa na mama yake pekee yake. Baba yake yupo hajafa ila binti hajawahi kukutana ana kwa ana na baba yake wala katika upande wa baba yake hamjui ndugu yeyote.

Je, kwa scenario kama hiyo binti anafaa kutolewa mahari na kuolewa?

Na taratibu za mahari zipoje? Kwani navyojua mahari ni ya baba na kama baba hayupo mahari ipokelewe na yeyote upande wa baba yaani shangazi au baba mdogo au mkubwa.
 
Komeni kuwaandama single mothers, ni ukosefu wa nidhamu na ni kinyume na utu.

Unasema mahari ipokelewe na baba ambaye hata hamjui binti. Hapo kuna baba kweli.

Unasema binti hafahamiani hata na ndugu mmoja upande wa baba, hapo undugu uko wapi?

Halafu taratibu za mahari za kwenu ni tofauti na watu wengine. Upande wa bi harusi ndio unaoandaa taratibu zote za mahari na namna gani mahari ipokelewe, sio wewe unayepanga.
 
Back
Top Bottom