Yawezekana kuna watu watakataa lakini hilo ni 'non of my business '
Nije kwenye mada moja kwa moja, kwa maoni yangu naona soka la bongo limekuwa zuri haswa, yaani hata ukilipa au kutenga muda kuangalia mpira unafurahi.
Binafsi sikuwa mpenzi wa kukaa na kuangalia mpira wa Bongo katika TV ila majuzi niliangalia mechi ya Simba na Mbeya City, aiseee unaangalia mechi hadi unafurahi. Watu wanajua mpira na ni wa ushindani haswa.
Tulikuwa na watu pembeni ambao sio Watanzania yaani walikuwa wanafurahia haswa. Na kwa hili sikuwa na mpango wa kuongeza lundo la ving'amuzi ila sasa nitanunua cha Azam ili nisipitwe hata nikiwa nyumbani.
Kwa ambao hawajui, ligi ya Tanzania ndiyo ligi bora Afrika mashariki na kati. Sijajua ulinganifu wake na ligi ya Congo ila itoshe kusema ni ligi nzuri.
Katika kusoma kwangu mitandao, nimegundua inafuatiliwa nchi zote za Afrika mashariki, Zambia, Afrika kusini (Kuna watu watabisha).
Kuna habari ya mchezaji wa Plateau anayewaniwa na Simba. Katika habari hiyo inaonyesha timu za huko wanafatilia ligi ya Tanzania. Hii ni dalili njema ya kukua.
Swala langu la msingi leo ni kupongeza, je unadhani ni nani anastahili pongezi japo kwa ukuaji huu wa ligi yetu? Yawezekana sio nzuri kulinganisha na ligi za mataifa yaliyoendelea ila kuna maboresho makubwa.
Je apongezwe Azam kwa kuonyesha, ipongezwe serikali kuweka mazingira mazuri, au wachezaji wa kigeni kuleta ushindani au TFF kwa ubunifu?
Toa maoni yako.