Je, nani anastahili pongezi katika soka la Tanzania?

Je, nani anastahili pongezi katika soka la Tanzania?

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Yawezekana kuna watu watakataa lakini hilo ni 'non of my business '

Nije kwenye mada moja kwa moja, kwa maoni yangu naona soka la bongo limekuwa zuri haswa, yaani hata ukilipa au kutenga muda kuangalia mpira unafurahi.

Binafsi sikuwa mpenzi wa kukaa na kuangalia mpira wa Bongo katika TV ila majuzi niliangalia mechi ya Simba na Mbeya City, aiseee unaangalia mechi hadi unafurahi. Watu wanajua mpira na ni wa ushindani haswa.

Tulikuwa na watu pembeni ambao sio Watanzania yaani walikuwa wanafurahia haswa. Na kwa hili sikuwa na mpango wa kuongeza lundo la ving'amuzi ila sasa nitanunua cha Azam ili nisipitwe hata nikiwa nyumbani.

Kwa ambao hawajui, ligi ya Tanzania ndiyo ligi bora Afrika mashariki na kati. Sijajua ulinganifu wake na ligi ya Congo ila itoshe kusema ni ligi nzuri.

Katika kusoma kwangu mitandao, nimegundua inafuatiliwa nchi zote za Afrika mashariki, Zambia, Afrika kusini (Kuna watu watabisha).

Kuna habari ya mchezaji wa Plateau anayewaniwa na Simba. Katika habari hiyo inaonyesha timu za huko wanafatilia ligi ya Tanzania. Hii ni dalili njema ya kukua.

Swala langu la msingi leo ni kupongeza, je unadhani ni nani anastahili pongezi japo kwa ukuaji huu wa ligi yetu? Yawezekana sio nzuri kulinganisha na ligi za mataifa yaliyoendelea ila kuna maboresho makubwa.

Je apongezwe Azam kwa kuonyesha, ipongezwe serikali kuweka mazingira mazuri, au wachezaji wa kigeni kuleta ushindani au TFF kwa ubunifu?

Toa maoni yako.
 
Nina maswali kwako

1) Ni kigezo kipi ulichotumia kusema ligi yetu imekua? Kama ni mechi ya ushindani ni ushindani upi unaozungumzia ikiwa timu mpaka kipindi cha kwanza kaishaoga goli nyingi?

Kama unaozungumzia chenga twawala basi sawa. Binafsi sioni ligi kama imekuwa bali naona Simba ndio imekuwa zaidi.

2) Unabaki na king'amuzi cha Azam pekee kwasababu haupendi ama ligi za kimataifa mfano UEFA, euro, epl, la liga, serie A, n.k au hazivutii Kama ligi ya Tanzania?
 
Ofcoz kuna hatua imepigwa tofauti na mwanzo

Ila tunahitaji miundo mbinu bora kabla hatujaanza kusifia ukuaji

Ninachokiona kwa sasa ni kuongezeka kwa wafuatiliaji, hapa ndio haswaa kuna watu wa kupongezwa

Na kwa upande wangu, nawapongeza Azam, Simba, Mo na Manara

Hawa kwa upande wangu ndo wameifanya ligi yetu iwe na wafuatiliaji wengi.
 
Nina maswali kwako

1) ni kigezo kipi ulichotumia kusema ligi yetu imekua? Kama ni mechi ya ushindani ni ushindani upi unaozungumzia ikiwa timu mpaka kipindi cha kwanza kaishaoga goli nyingi?..
1. Mkuu, kama wewe ni mfatiliaji wa maoni ya wadau wa michezo ambao sio watanzania utasikia hizi comments. Mfano mzuri ni interview ya Onyango mchezaji wa Simba akieleza ni kwa nini anaona ligi ya Tanzania ni bora na kwamba Kenya wajifunze kitu.

2. King'amuzi cha Azam sikuwa nacho nilikuwa na vingine tu. Sasa kwa kuwa nimeona kuna burudani nitanunua ili niwe nafatilia.
 
Nina maswali kwako

1) ni kigezo kipi ulichotumia kusema ligi yetu imekua? Kama ni mechi ya ushindani ni ushindani upi unaozungumzia ikiwa timu mpaka kipindi cha kwanza kaishaoga goli nyingi?...
Wacha ujinga wewe kwenye pongezi tuwe na desturi ya kupongeza na co kuwa watu wa kulaumu laumu tu [emoji116][emoji116].

JamiiForums-585168039.jpg
 
Ofcoz kuna hatua imepigwa tofauti na mwanzo

Ila tunahitaji miundo mbinu bora kabla hatujaanza kusifia ukuaji...
Mo alikuwepo tangu kitambo na ligi haikuwahi kukuwa km sasa, au unampongeza kwa Simba kuingia robo fainali? Kwani ndo mara ya kwanza kwa timu za Tanzania kuingia robo fainali? Zimeshafanya hivyo Yanga na Simba miaka mingi iliyopita labda uwe mtoto wa juzi.

Unamsifia Manara kwa lipi hasa juu ya soka la bongo kukuwa? Au maneno maneno mengi ya kipuuzi ambayo tumezoea kwa wasemaji wa timu za bongo? Unadhani maneno ya kihuni huni ndo yanayokuza mpira? Hao wasemaji wahuni wenye mawazo ya kizamani ndio wanaosababisha tusiende mbali zaidi ya hapa tulipo na ningeshauri waondolewe ili tuwe na watu proffesional wanaozijua kazi zao na sio spokesmen wenye mawazo ya Simba na Yanga ni upumbavu.

Hapo wa kupewa hongera ni Azam kwa kuonesha ligi yetu live cz kwa kufanya hivyo wameongeza mvuto wa ligi cz wachezaji wanakuza viwango ili waonekane zen wapate timu wanazoota kuzichezea, pia TFF japo sio sana lkn huwezi kukwepa kuwapongeza mana mafanikio ya ligi yanawahusu kwa asilimia nyingi.
 
Mshana umeona Simba tu??? Ila uongo mbaya Simba sijui walikosea wapi, safari hii walikuwa wanafika fainali...

Au mzee wa tunguli tuambie walikosea wapi?
Jamani chiefs wamempiga wydad kwao...so hawakumuotea simba. Wapo vizuri wale
 
Mshana umeona Simba tu??? Ila uongo mbaya Simba sijui walikosea wapi, safari hii walikuwa wanafika fainali...

Au mzee wa tunguli tuambie walikosea wapi?
Ulozi aisee.. Kama kuna mwaka Simba imerogwa na Yanga basi ni huu..huko vilingeni tunapata tabu sana
 
Ukweli utabaki kuwa, Azam TV wameleta hamasa kubwa sana katika ligi yetu. Na siyo mpira tu, hata michezo mingine mfano masumbwi (Vitasa). Nilikuwa sipendi masumbwi ya bongo, ila nimetapenda baada ya kuanza kurushwa na Azam!

Leo timu zote zinacheza kwa bidii, kwa sababu wanajua wanafuatiliwa kwenye TV! Mchezaji gani hataki kujiuza kupitia TV, ili asajiliwe timu kubwa?

Leo, huko ndani ndani Watanzania wengi tu wanafuatilia ligi yetu kupitia Azam TV!

Nikipata nafasi ya kuwashauri TFF nitasema kwamba, watafute mdhamini wa kueleweka na timu zibaki 18 au zifike 20. Hii nchi ni kubwa, kuna mikoa haina timu za ligi kuu.

Mikoa hii ikipata timu, hamasa itakuwa ni kubwa sana, na hela ipo kwenye mpira kwa sasa!

Hongera Azam TV!
 
Wacha ujinga wewe kwenye pongezi tuwe na desturi ya kupongeza na co kuwa watu wa kulaumu laumu tu [emoji116][emoji116]View attachment 1829072
Watu wanashangaza sana ligi yetu imekuwa na ushindani sana.

Ukiona timu kama mtibwa na kagera Sugar zinapambana kutoshuka daraja ni picha tosha ushindani umeongezeka.

NB: Ningependa Mbeya City wasishuke daraja msimu huu aisee.
 
Ukweli utabaki kuwa, Azam TV wameleta hamasa kubwa sana katika ligi yetu. Na siyo mpira tu, hata michezo mingine mfano masumbwi (Vitasa). Nilikuwa sipendi masumbwi ya bongo, ila nimetapenda baada ya kuanza kurushwa na Azam!

Leo timu zote zinacheza kwa bidii, kwa sababu wanajua wanafuatiliwa kwenye TV! Mchezaji gani hataki kujiuza kupitia TV, ili asajiliwe timu kubwa?

Leo, huko ndani ndani Watanzania wengi tu wanafuatilia ligi yetu kupitia Azam TV!

Nikipata nafasi ya kuwashauri TFF nitasema kwamba, watafute mdhamini wa kueleweka na timu zibaki 18 au zifike 20. Hii nchi ni kubwa, kuna mikoa haina timu za ligi kuu.

Mikoa hii ikipata timu, hamasa itakuwa ni kubwa sana, na hela ipo kwenye mpira kwa sasa!

Hongera Azam TV!
TFF wawe sirias, mpira unalipa kwa sasa. Watafute wawekezaji, wasiwe sehemu ya kukwamisha maendeleo ya mpira.

Logic ndogo tu! Miaka ya nyuma (2000 kurudi nyuma) timu za ligi kuu zilifika 20 kama sikosei, na wananchi walikuwa wachache tofauti na sasa.

Miundo mbinu ya usafiri haikuwa rafiki sana, na timu zilikuwa hadi zinalala njiani na mechi inahairishwa inachezwa siku nyingine, lakini timu zilipambana kumaliza mechi. Leo hii miundombinu ya usafiri imeimarika, sehemu yoyote ndani ya Tanzania hii ikiwa mbali sana unasafiri kwa bus na hazizidi siku mbili!

Kipindi hicho hela hazikuwepo nyingi kwenye mpira kama sasa, lakini wachezaji walijitolea sana miaka hiyo.

Leo, hamasa ya mpira imekuwa kubwa kila kona ya nchi, lakini TFF wanataka tuwe na timu 16, na baadae 14.

Leo, hela ipo kwenye mpira kupitia viingilio tofauti na zamani, lakini TFF wanataka kupunguza timu badala ya kuongeza timu.

Leo tupo watanzania milion 55-60, lakini TFF wanataka timu ziwe 16, kweli?

Afisa masoko wa TFF pambana, ligi yetu imechangamka kwa sasa, iuzeni ligi yetu mpate wadhamini.

Timu ziongezeke zifike 20. Mbona zamani iliwezekana?
 
Ulozi aisee.. Kama kuna mwaka Simba imerogwa na Yanga basi ni huu..huko vilingeni tunapata tabu sana
[emoji23][emoji23]Poleni sana wanavilinge wa Simba,wazee wa Yanga kina mzee Mpili wazee wa nyuklia wamefanya kazi kubwa.
 
Back
Top Bottom