Je, nani anaweza kumzidi mwenzake soko kati ya Azam na DStv endapo hili likifanyika?

Je, nani anaweza kumzidi mwenzake soko kati ya Azam na DStv endapo hili likifanyika?

Azam hata akionyesha Epl hataweza kushindana na Dstv sababu ni ndogo sana.

Management and Technology. Azam hawako serious hapa. Tena hasa tukija kwenye swala la customer care services na quality ya channels zao.Tukumbuke watu wengi now wana TV zenye technology kubwa.

Dstv ni ghali lakini experience yao kwenye hii sekta na seriousness yao kwenye kutoa huduma bora ndipo anapompiga bao Azam.

Azam akiweza kushindana na Dstv kwenye hizi vitu hakuna mbongo atataka Dstv.
 
Mkuu ukiachana m-net hizo nyingine azam anazo history ipo IDX ipo, national geographic ipo nk
Asante sana Mkuu kunijuza,sijapata hata muda wa kuangalia kama zipo hizo,mbali ya IDX,waongeze na zingine kama CBS Justice,na za habari za Kimataifa mbali ya AlJazeera! Hapo sasa kutakuwa na ushindani kweli.
 
Azam TV akionyesha izo league DSTV atafungasha mda mfupi sanaaa
 
Mi nauhakika Dstv amepiga hatua kubwa hadi sasa.Assume haonyeshi ligi pendwa ya bongo,vpl na bado anakimbiza,je akiweka na ligi yenu?? Kunawakumpinga?? Dstv ni level za Fox ,na sky sports uko
 
Endapo Azam ataonesha Ligi mbalimbali duniani

1. Bidding zake ilikuonesha ni ghali sana, itamlazimu kupandisha gharama hata mara tano au mara kumi ili apate faida. Wateja watapotea wenyewe. AZAM atapotea

2. Soko la AZAM lina upana namna gani hapa Africa (East, Southern, Northern na western) ukilinganisha na Dstv? AZAM atapotea

3. Professional na ubora wa vipindi mbalimbali hususani soccer...... AZAM bado sana.

4. Coverage sio kuangalia soko la ndani pekee AZAM na dstv wanatofauti kubwa sana ya coverage, kukubalika,
Hapo kwenye coverage za mpira hata dstv bado sana nenda kaangalie coverage ya league ya south Africa anayoonyesha ni yakawaida sana, hizo epl,uefa ni matangazo ambayo dstv anapokea yakiwa yametengenezwa na BT sport
 
Mkuu ukiachana m-net hizo nyingine azam anazo history ipo IDX ipo, national geographic ipo nk
Mkuu ujue kuna watu hapa waba reply ili mradi0 tuuu wapate reaction points.
Msamehe bure hajui alitendalo. Azam yupo njema sana hata kwa bei za vifurushi vinaendana na huduma halisi anazotoa. Yaan akionyesha UCL, EUROPA, EPL atamfukuza dstv asubuhi sana.

Azam kifurushi kinakata local chanels unapata. Dstv kikikata unambulia tbc na hapo hadi watu walivyolalamika.
Azam kifurushi kinakata redio unapata zoote. Dstv redio hata moja hupati kifurushi kikiisha
 
Wadau nimejaribu kuwaza endapo haya makampuni mawili yakafanya kile ambacho kila mmoja anafanya.

Je, nani atafungasha virago? Nani atapoteza pambano?

Najiuliza endapo Azam ataonesha UEFA, EPL na Europa ligue

Ama DSTV akionyesha Ligi ya bongo (VPL)

Nani atakimbia?
haiwezekani kufanyika hivyo peroiod!
 
Azam akifanya hao uliosema DSTV atafunga biashara kama GOTV.
DSTV ukitoa UCL, EPL na ligi nyingine hakuna cha ziada nakuambia ninayo mwaka wa 6 sasa.
Tena miaka ya hivi karibuni ndo wanajikaanga na mafuta yao wenyewe
DSTV wako aggressive kisenge yaani, Kwese mwenyewe hata miaka 2 sokoni hajamaliza, kasanda.
 
Wadau nimejaribu kuwaza endapo haya makampuni mawili yakafanya kile ambacho kila mmoja anafanya.

Je, nani atafungasha virago? Nani atapoteza pambano?

Najiuliza endapo Azam ataonesha UEFA, EPL na Europa ligue

Ama DSTV akionyesha Ligi ya bongo (VPL)

Nani atakimbia?
Kuwa serious basi jamaa yangu
 
1. Azam Bado wanafeli Sana katika quality ya picha. ( Bado wapo nyuma Sana ukilinganisha na DStv)

2. Hata wingi wa channels hasa wapenda movies, michezo Azam Bado Sana

3. Azam Bado katika Mambo ya kiufundi na umakini mfano katika vipindi vyao vingi hawatoi information ya kutosha kuhusu vipindi vyao pia hata huduma ndogo ya Reminder kwa kipindi mtazamaji atachotaka angalia muda fulani hawana.

Kiukweli Azam Bado Sana ku compete na DStv endapo hayo mtoa mada aliyoyasema yakifanyika. Ila endapo Azam akibadilisha mapungufu aliyokuwa nayo kwanza anaweza angalau kuwa good competitor wa DStv ila kwa Sasa Bado Sana yupo nyuma.
 
Azam hawa hawa ambao hata ukipiga customer care hawawezi kupokea simu..mzigo mzito unawapa ubora wa huduma sio vipindi tu
 
Mkuu ujue kuna watu hapa waba reply ili mradi0 tuuu wapate reaction points.
Msamehe bure hajui alitendalo. Azam yupo njema sana hata kwa bei za vifurushi vinaendana na huduma halisi anazotoa. Yaan akionyesha UCL, EUROPA, EPL atamfukuza dstv asubuhi sana.

Azam kifurushi kinakata local chanels unapata. Dstv kikikata unambulia tbc na hapo hadi watu walivyolalamika.
Azam kifurushi kinakata redio unapata zoote. Dstv redio hata moja hupati kifurushi kikiisha

Wewe nae anisamehe kwani nimefanya kosa gani? Huoni mwenzio tumejibizana vizuri tu.So wewe unaejibu hapa na wewe unatafuta hiyo “reaction points”.Jifunze kukubaliana kutokubaliana.Sio kila kitu lazima tuwe na mtizamo sawa.Haya mimi nasema Dstv yuko vizuri zaidi ya Azam na niko sahihi,Na wewe baki na mtazamo wako na uko sahihi pia,hakuna mshindi hapa.
 
Kibongo bongo,
mchawi ni LIGI KUU BARA

Atakaeonyesha ligi ndo atakaekamata soko.

Hizo Uefa, Europa.
Washabiki wachache.

Na Watu washazoea kuangalia kwenye mabanda umiza Miaka na Miaka.
Afu et uko serious kabisa yn
 
Back
Top Bottom