Nani kakudanganya,Azam ligi ya uingereza anaitaka leo kesho anaye mzuia DSTV,inasemekana kusini huku mwa jangwa la Sahara mwenye haki ya kuonyesha EPL ni DSTV pekee.
Azam walienda FA na pendekezo la kuonyesha EPL kwa Kiswahili,DSTV nae akawachukua akina Edo,Maulid wa Kitenge wakatangaze kwa Kiswahili.
Hiyo ligi ndio moyo wa DSTV,kama unakumbukumbu kipindi kile G-Sports walivyopewa haki ya kuonyesha mechi zote za EPL,DSTV akawa na hali mbaya sana ashukuru ule mtikisiko wa uchumi ndio ulimtoa G-Sports kwenye soko la sivyo ingekuwa tayari ishafutika Tanzania.
Na kuhusu quality DSTV game zenye quality nzuri ni za EPL na UEFA,La Liga lkn ligi wanazo onyesha za South Africa,Zambia quality yake sawa sawa na Azam na kama hujui mechi za CAF club bingwa na shirikisho zinazo fanyika Africa Mashariki na kati production yote wanafanya Azam.
Multichoice wamefanya uwekezaji wa zaidi ya 120b za kibongo,sidhani km Azam anaweza kufikia hata robo, watangazaji wa DStv wanakula mishahara minono ,wapo wanaokunja takoni mil40 za kibongo kwa mwezi.... sidhani km Azam wanaeza mlipa baruan muhuza hyo pesa,
Sio kweli kwamba Azam kashindwa kuonesha ligi ya premier kisa kabaniwa na DStv, sababu league ya uingereza ina package sio lazima upewe package nzima, Kuna highlights, interviews, fixtures ndo maana hata tbc anaonesha baadhi ya mechi, km ilivyokuwa kwa G tv ambae alikuwa anaonesha 20% ya mechi za ligi...
Hata package za DStv Zina channels za nguvu ukilinganisha na Azam ambazo nyingi Ni za uarabuni ambazo Ni free to air (FTA) kwa wakazi wa tanga mjini nadhani watakuwa wanajua,kabla ya kuhamia digital channels za mbc(1,2),star movie,star gold,e,zilikuwa zinapatikana free tu..
Kuwapeleka wakina kibonde,Edo kumwembe SA wakatangaze kwa kiswahili ni ushindani wa kibiashara umekuwa mkubwa kumbuka hapo mwanzo DStv ndo alikuwa babalao , alikuwa peke yake kwenye digital satellite ,halafu matangazo ya mpira yalikuwa kireno na kiingereza, ndo wakaongeza na kiswahili..
Kwangu mm naona Azam bado anahitaji kujifunza vingi kupitia DStv