Je, nani anaweza kumzidi mwenzake soko kati ya Azam na DStv endapo hili likifanyika?

Azam hawezi kuonesha ligi ya uingereza kwani gharama zake ni kubwa mno base yake ya subscribers ni ndogo
Nani kakudanganya,Azam ligi ya uingereza anaitaka leo kesho anaye mzuia DSTV,inasemekana kusini huku mwa jangwa la Sahara mwenye haki ya kuonyesha EPL ni DSTV pekee.

Azam walienda FA na pendekezo la kuonyesha EPL kwa Kiswahili,DSTV nae akawachukua akina Edo,Maulid wa Kitenge wakatangaze kwa Kiswahili.

Hiyo ligi ndio moyo wa DSTV,kama unakumbukumbu kipindi kile G-Sports walivyopewa haki ya kuonyesha mechi zote za EPL,DSTV akawa na hali mbaya sana ashukuru ule mtikisiko wa uchumi ndio ulimtoa G-Sports kwenye soko la sivyo ingekuwa tayari ishafutika Tanzania.

Na kuhusu quality DSTV game zenye quality nzuri ni za EPL na UEFA,La Liga lkn ligi wanazo onyesha za South Africa,Zambia quality yake sawa sawa na Azam na kama hujui mechi za CAF club bingwa na shirikisho zinazo fanyika Africa Mashariki na kati production yote wanafanya Azam.
 
Multichoice wamefanya uwekezaji wa zaidi ya 120b za kibongo,sidhani km Azam anaweza kufikia hata robo, watangazaji wa DStv wanakula mishahara minono ,wapo wanaokunja takoni mil40 za kibongo kwa mwezi.... sidhani km Azam wanaeza mlipa baruan muhuza hyo pesa,

Sio kweli kwamba Azam kashindwa kuonesha ligi ya premier kisa kabaniwa na DStv, sababu league ya uingereza ina package sio lazima upewe package nzima, Kuna highlights, interviews, fixtures ndo maana hata tbc anaonesha baadhi ya mechi, km ilivyokuwa kwa G tv ambae alikuwa anaonesha 20% ya mechi za ligi...

Hata package za DStv Zina channels za nguvu ukilinganisha na Azam ambazo nyingi Ni za uarabuni ambazo Ni free to air (FTA) kwa wakazi wa tanga mjini nadhani watakuwa wanajua,kabla ya kuhamia digital channels za mbc(1,2),star movie,star gold,e,zilikuwa zinapatikana free tu..

Kuwapeleka wakina kibonde,Edo kumwembe SA wakatangaze kwa kiswahili ni ushindani wa kibiashara umekuwa mkubwa kumbuka hapo mwanzo DStv ndo alikuwa babalao , alikuwa peke yake kwenye digital satellite ,halafu matangazo ya mpira yalikuwa kireno na kiingereza, ndo wakaongeza na kiswahili..

Kwangu mm naona Azam bado anahitaji kujifunza vingi kupitia DStv
 
DStv hawezi kumzuia Azam kama atakuwa ameshinda mnada(bid) na ametimiza vigezo..kama amenyimwa licence ni kuwa hajatimiza vigezo.

Dstv wanaonyesha mechi zote 380 za EPL na bei ya leseni sio mchezo.
 
Sasa hiyo ndio inaonesha nini? Kwamba Azam ni bora zaidi ya Dstv?
 
Azam akifanya hao uliosema DSTV atafunga biashara kama GOTV.
DSTV ukitoa UCL, EPL na ligi nyingine hakuna cha ziada nakuambia ninayo mwaka wa 6 sasa.
Tena miaka ya hivi karibuni ndo wanajikaanga na mafuta yao wenyewe
Sasa azam ndio wana kipi cha maana ukiondoa vpl labda na local chanel.
Kwangu ukizungumzia dstv sikosi chochote kihusucho entertainment. Documentaries, music & movies
 
Wapambane wapate full rights za kuonyesha hizo mechi,Azam kwa EPL wanaonyesha mechi moja moja na huwa hawatabgazi,mfano Jana nimeona mechi ya Man City na thousampton
 
DStv hawezi kumzuia Azam kama atakuwa ameshinda mnada(bid) na ametimiza vigezo..kama amenyimwa licence ni kuwa hajatimiza vigezo.

Dstv wanaonyesha mechi zote 380 za EPL na bei ya leseni sio mchezo.
Ninacho ongea nakijua nina watu watatu niliofanya field TTCL 2012 wapo Azam pale upande wa Technical (Broadcasting Engineer).
 
Ikaja tokea DSTV akaonesha Mpira wa bongo just azam ndio bye bye!!!

DsTV Wana qualy nzuri ya picha zao
 
Ninacho ongea nakijua nina watu watatu niliofanya field TTCL 2012 wapo Azam pale upande wa Technical (Broadcasting Engineer).
Kwahiyo hao jamaa zako waliku-tell azam wamezuiwa na dstv kwa namna gani?
 
Duh! mleta uzi nikadhania unaifananisha DStv na Zuku maana ndio level yake, sababu hata Star Times na DStv kwa soko la bongo, bado Star Times ipo vyema ila Azam ni namba nyengine.
 
Mkuu umewakilisha mawazo yangu. Mpira wa bongo hata niambiwe simba na yanga wanacheza, na kiongilio ni bure na kinywaji juu siendi. Mpira umetawaliwa na usanii wa hali ya juu. Kwa sasa watu wameelekezwa kujadili mpira tu, lakini ukijadili mambo ya nchi hasa kwa approach ya kukosoa, imekula kwako.
 
Azam akionyesha EPL,
DStv atakimbia mji asubuh na mapema sana
 
Mimi nawashauri waanzishe virushi vya wiki wiki bana!! Wengine tunaangalia TV only on weekends bana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…