Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

Je, naweza kuanza ujenzi nikiwa hivi?

KUNA MTU KATOA KOMENTI YA HOVYO

ETI FUNGUA BIASHARA KWA MAANA UNAWEZA KOSA MUDA WA KUSIMAMIA UJENZI

HOJA MBOVU KU JUSTIFY PUMBA
 
Wengi wenu hamna experience ya ujenzi, mnafikiri ujenzi ni rahisi, kama hauna usimamizi ni kama unagawa hela zako kwa mafundi. Utaibiwa mpaka mchanga na kokoto site.

The good idea, aanzishe biashara ata mkataba utakapoisha aikute biashara imesimama aendelee nayo. Ukijenga ukiwa hauna source nyingine ya income, ultimately utaiuza hiyo nyumba.
Nasimama na wewe, atakuja kusema ni heri ile hela ingekaa tu kwa aka akaunti. Attempt ya ujenzi kwa sasa angeiacha kwanza akatafuta biashara ambayo haitambana sana.
 
ukiangalia hiyo DP yangu ni chumba kimoja niliokuwa najenga 2021 kipindi nipo internship shirika fulani hivi walikuwa wanatulipa 300,000 per month, nilijiapiza sitoki nyumbani ntakula msosi wa kengele mpaka jambo langu litimie mungu kasaidia nimeweza, sasa hivi nimepata ajira ya kudumu nimenunua sehemu nyingine najenga tena nikiwa na experience.
kijana mwenzangu jenga hata chumba na sebule maisha ya tanzania yanabebwa na siasa,
hapo wanaokwambia uanzishe biashara ni hizi hizi tunazoziona umachinga au duka, mazao n.k hivi vyote mwanasiasa akikaa bungeni anapiga tu meza kumbe kapitisha sheria inayokuja kukunyoosha.
 
Watu mnagombana kisa ushauri tu je angesema awape hiyo hela si mngeuana kabisa😂😂🤣🤔
 
Biashara anaijua...kuna jirani yangu mwaka jana wamechukua mkopo wa million 20 wakasema wanafanyia baishara .

Kufupisha story baada ya mwaka baishara imekufa wamebaki na gari. Mkopo wanaendelea kulipa wakiwa nyumba za kupanga.
Sababu ya biashara kufa ni nini?
 
Anza kujenga kama inawezekana unaweza ukapandisha chumba kimoja na choo ndani ya ramani ya nyumba na ukahamia ili kukwepa gharama za kodi alafu mdogo mdogo unaendeleza ukiwa kwako. Baada ya muda unafunga nyumba nzima.
 
Nyumba kwa sasa haina umuhimu kwako, tengeneza income flow kwa sasa uwe na vyanzo tofauti tofauti halafu baada ndio ujenge...
 
Mdogo angu jenga tu.

Kazi yako ni ya mkataba na nadhani ina ku keep busy.

So nahisi ukifungua biashara hutapata muda wa kuisimamia hivyo utaajiri mtu asimamie, huyu mtu anaweza kula pesa yako buuureee.

So nadhani kwa sasa ni bora tu kujenga,kiwanja + nyumba ni mtaji tosha sana
 
Ukijichanga Tu hiyo pesa inaishia na upepo weko lengo ndani ya mwaka uwe na pagare lenye mpaka Bati...
Mwaka wa pili jaribu biashara yoyote na mtaji wa laki tano..
Fanya finishing taratibu kuanzia master
Anza na ujenz Ila usiache biashara kidogo kidogo upate uzoefu fanya kwa phase
 
Miaka yangu 26 ( me)..

1. Kiwanja ninacho 1
2. Bank nina mil 3
3. Tayari nimeshatoka nyumbani kitambo (najitemegea)
3. Nimeajiriwa kwenye N.G.O ( afya) kwa mkataba wa miaka 3.

Je, naweza kuchokoza ujenzi kwa sasa kwenye hicho kiwanja changu au niwaze biashara kwanza na vitega uchumi vingine?

Majukumu

1. Sina mke
2. Sina mtoto
3. Nawaboost wazazi kusomesha mdogo wangu ndio ameanza mwaka wa 1..
4. Kuhonga kwa akili
5. Kuwaboost wana & ndugu pale ninapohitajika
Jenga kwanza ukitaka kufanya biashara utaiweka nyumba collateral bank utapata mkopo wa kufanya biashara.
 
Back
Top Bottom