Habari mdogo wangu
Kiuchumi kama ukianza kujenga na huna uhakika wa kupata pesa nyingine baada ya hapo utajikuta unaishia kwenye lenta na hujui unapata wap nyingine
Ukianzisha biashara ukijikeep bize na biashara uliuoanzisha ikachanganya utakuwa na kipato endelevu ambacho utatumia kujengea huku biashara ikiendelea kumbuka mkataba utaisha na hata hivyo mdogo wangu kwani unalala njee?? Usifadhaike watakaocheka kwamba bado unakaa home tengeneza kwanza msingi wa uhakika cha kuingiza kipato ata kama umelalaa # WEKEZA MDOGO WANGU
USHUHUDA
mimi ni muhitimu wa chuo mwaka 2019 sina ajira mpaka sasa niliishi nyumbani mpaka 2022
Hapo katikati nlikuwa najishughurisha na shughuri mbalimbali ambazo nilikuwa najipatia kipato japo ni kidogo nikawa naweka, nilipendelea kusoma vitabu vya ujasiliamali nikawa naongeza maarifa, nilipiga bodaboda, mpaka kufika mwaka 2022 nikaomba kufanya kazi ya muda mfupi tuu ya sensa ya watu na makazi ambayo wala hakudumu sana lakini wewe yako ni miaka 3
Nilipata pesa nikaunganisha na zile nilizokuwa nikitafuta mwanzoni nilipata jumla ya akiba ya TSH 5,050,000 Milioni tano na elfu hamsini
Wenzangu niliofanya nao kazi ile wapo baadhi walikimbilia kujenga baadae nguvu zikaisha wakaishia njiani
Mimi sikupata mihemko waliyonayo ila kwa kuwa nilipata elimu ya ujasiliamali kupitia kusoma vitabu nikacheki fursa ya eneo nililopo mimi naishi Dodoma shughuli kubwa ni kilimo cha zabibu nakapiga hesabu kwa heka moja kwa kufata na ushauri pia wa wazoefu wa kilimo hicho kuanzia uandaaji wa shamba mpaka upandaji kilimo nilichofanya ni umwagiliaji ilighalimu pesa isiyozidi 4,000,000
Nyingine nilihifadhi kwa ajili ya emergence kama kununua dawa kutoa magugu n.k
Hivi leo naongea nanyi tayar makampuni ya mvinyo wameshaingia ubia kwa kutaka niwauzie zabibu hizo pindi tu zitakapokomaa
NB
Zabibu ni zao la muda mtefu mti mmoja unaweza kukaa ata miaka 30 mpaka 40 na kila mwaka huwa inaongeza kiwango cha kuzaa kilo moja ya zabibu ni 1500- 2500 heka moja inaweza kutoa kilo 8000 mpaka kg 9000 je utashindwa kujenga nyumba unazotaka hapa mjinii????
Nawatakia utekelezaji mwema ndugu wasomaji