Habari waheshimiwa, kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza, JE naweza kufahamu kwa njia yeyote kama Mzazi wangu ambaye ni marehemu ( zaidi ya miaka 20 iliyopita) kama alikuwa ni mfanyakazi wa Idara ya Usalama hapa Tanzania. Sawa, mtu anaweza kuuliza kwanini au nini kimepelekea nitake kujua?
Ni kwamba miaka mitano nyuma katika tembea yangu mikoani huko nikafika mkoa wa nyumbani( mkoa ambao baba yangu alizaliwa na kusomea elimu yake ya sekondari) nikabahtika kukutana na mtu ambaye alisoma naye, katika kutambulishana bahati nzuri akasikia jina langu, na ikatokea kweli amemfahamu mzee wangu pamoja na ndugu zangu wengine ndio akadokeza hilo jambo. sikumbuki likuaje lakini akawa amelisema hilo na mimi sikuwa nafahamu chochote. nikaliweka nikasema ntalifatilia na wa kwanza kumuuliza ni Mzazi mwenziye yani mama yangu lakini na yeye hakujua kuhusu hilo ila tu akanieleza tabia za mzee alivyokuwa kwa uchache, Mzee wangu alikuwa ni mhasibu kwa taaluma, na alikuwa akifanya kazi katika shirika la wazungu lililopo hapa Tanzania linalojishughulisha na masuala ya kilimo. Kwa maelezo ya mama ni mtu mwenye kusafiri mara kwa mara, na kwamba alikuwa mtu wa watu sana, na marafiki wengi.
niliona kwa wenzetu shirika la ujasusi wa ndani wa Uingereza MI5 (The Security Service) huwa wanatoa majibu kwa Mzazi au ndugu marehemu kama aliwahi kufanya kazi kwenye shirika lao, ingia hapa (SSQ | MI5 - The Security Service) sehemu ya FACTS OR FINCTIONS. naona sio vibaya nikauliza hapa kwa wenye kujua,ili kama na hapa kwetu linawezekana basi nipate kufahamu.