Je, naweza kufahamu kama Mzazi wangu marehemu aliwahi kufanya kazi Usalama wa Taifa?

Je, naweza kufahamu kama Mzazi wangu marehemu aliwahi kufanya kazi Usalama wa Taifa?

Status
Not open for further replies.
Mpm.... Waangalie database kama yupo maana hawa watu bana.... Nilisoma na jamaa olive.. Tukaachana kati kati hapo tukakutana first degree alikua anajinasibu kama afisa maendeleo ya jamii kaja Kuongezea Elimu ila tumemaliza chuo namuona kwenye misafara ya Rais mstaafu nkastuka hivi afisa maendeleo ya jamiii na kaunda suit vinaendanaje
ha ha ha ha ah ah ah hawasomeki nakwambia.
 
Hapo ni vigumu sana kufahamu mkuu kwani hawa jamaa(TISS) wanapomfunza mtu (shushushu) hawamwajiri kama usalama wa taifa bali huwekwa kwenye kada mbalimbali za taasisi za serikali hata binafsi kulingana na malengo/uhitaji..

mfano wengine unaweza kumkuta ni mwalim, asikari jeshi, polisi, magereza, madaktari nk. sasa hapo hata anapofariki process zote za mazishi hufanywa na taasisi au kada iliyokuwa imemuajiri na sio TISS, haijawahi popote kutokea eti shushushu anazikwa na idara ya usalama wa taifa ( TISS), Jiulize je hakuna wanausalama wanaokufa?

Inawezekana ukabahatika lakini si virahisi kiivo zaidi utaambiwa hawakuwahi kuwa na mtu kama huyo ijapokuwa kweli alikuwa TISS,

wanashiriki kama marafiki tu au jamaa wengine, kwani kwenye msiba mtu akisema tu ni rafiki, au mwalimu au mfanya biashara mwenzake. au wakasema ni mchango kutoka kwa walimu wenzake. sema hawashiriki rasmi na kama aliyefariki ni mkubwa wanaweza tuma muwakilishi lakini hawajitambulishi. huu ndio uelewa wangu km nimekosea watu watasema
 
mkuu sizungumzii mazishi yake, najua wao hawakuziki kama wao kwani hufanya kazi zao kwa siri.
Hii ishu unayotaka kuifwatilia inaonekana ni ngumu na itakuumiza akili na wala hautapata ukweli.

[emoji53] embu jaribu kuchunguza nyaraka zake alizoziacha.
Na ufuatilie mawasiliano yake iwe mobile phone, computer etc.

Majibu yako kwako ww mwenyewe na huku hautakaa uyapate majibu ya kukuridhisha zaidi ya myth tu.

Ww ndo unayemhua baba ako na familia yako kwa ujumla hivyo sisi hatuifahamu.
 
mkuu bahati mbaya nilikuwa bado akili ndogo, kwa bahati mbaya hakuna hata kimoja nachoweza kukipata katika vitu vyake. kwa ufupi hakuna. kuna briefcase moja mama alinimbia lilikuwa la mzee, la zamani limefungwa kwa namba. na kwa vile mama alisafiri nilishawishika siku moja nikalivunja, kumbe mama aliweka vitu vyake yeye japo alisema la mzee. nilimuelewa vibaya nilijua mzee aliliacha kama lilivyo na halijawahi kufunguliwa
 
Njoo PM na taarifa zifuatazo; any of his phone number ya zamani, full names na his last occupation and organization.
 
Habari waheshimiwa, kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza, JE naweza kufahamu kwa njia yeyote kama Mzazi wangu ambaye ni marehemu ( zaidi ya miaka 20 iliyopita) kama alikuwa ni mfanyakazi wa Idara ya Usalama hapa Tanzania. Sawa, mtu anaweza kuuliza kwanini au nini kimepelekea nitake kujua?

Ni kwamba miaka mitano nyuma katika tembea yangu mikoani huko nikafika mkoa wa nyumbani( mkoa ambao baba yangu alizaliwa na kusomea elimu yake ya sekondari) nikabahtika kukutana na mtu ambaye alisoma naye, katika kutambulishana bahati nzuri akasikia jina langu, na ikatokea kweli amemfahamu mzee wangu pamoja na ndugu zangu wengine ndio akadokeza hilo jambo. sikumbuki likuaje lakini akawa amelisema hilo na mimi sikuwa nafahamu chochote. nikaliweka nikasema ntalifatilia na wa kwanza kumuuliza ni Mzazi mwenziye yani mama yangu lakini na yeye hakujua kuhusu hilo ila tu akanieleza tabia za mzee alivyokuwa kwa uchache, Mzee wangu alikuwa ni mhasibu kwa taaluma, na alikuwa akifanya kazi katika shirika la wazungu lililopo hapa Tanzania linalojishughulisha na masuala ya kilimo. Kwa maelezo ya mama ni mtu mwenye kusafiri mara kwa mara, na kwamba alikuwa mtu wa watu sana, na marafiki wengi.

niliona kwa wenzetu shirika la ujasusi wa ndani wa Uingereza MI5 (The Security Service) huwa wanatoa majibu kwa Mzazi au ndugu marehemu kama aliwahi kufanya kazi kwenye shirika lao, ingia hapa (SSQ | MI5 - The Security Service) sehemu ya FACTS OR FINCTIONS. naona sio vibaya nikauliza hapa kwa wenye kujua,ili kama na hapa kwetu linawezekana basi nipate kufahamu.

View attachment 411500

Je, ni nani alisimamia mirathi ni wewe au kuna mtu maalum aliteuliwa na kupitishwa na mahakama.

Kama yupo msimamizi wa mirathi basi ataweza kupitia kabrasha la marehemu mzee wenu na kila kitu kimeandikwa mle ingawa kunaweza kuwepo kabrasha mbili..

Tatizo linakuja kama hayupo huyo mtu na pia hata kama yupo awe na ruhusa maalum ya kusoma hilo kabrasha.

Halafu hizo kabrasha zipo hard copy na soft copy na hard copy ni classified hivyo haitolewi.

Je mambo kama wasia, mirathi na akiba kwenye mabenki yamemalizwa? Maana kama mafao basi yanapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti husika kama ile ya NSSF.

Yupo mtu maalum kwa kazi hiyo.

Vinginevyo wewe chukulia tu marehemu mzee wako alikuwa ni mhasibu kitaaluma na kama kila kitu kimekamilika basi hakuna taarifa zingine pana.
 
nashkuru sana mkuu, nilikuwa mdogo kwa hiyo sikumbuki chochote, ila mambo yote ya mirathi na yanayofanana na hayo yalishakamilishwa. kuhusu msimamizi ndio unanipa mwanga ngoja niulizie nijue kama yupo na hayo mambo ya kabrasha ( kama kweli mkuu kuna kabrasha hizo ntashukuru sana kwa kweli, ila najiuliza ni kwamba kama sijakuelewa vibaya, kweli wanatoa hizo kabrasha? sasa kama itahitaji ruhusa wanajuaje jama huyo waliyemkabidhi hatoyatoa? au na yeye anakuwa ni mtu wa aina gani, umenipa mwanga lakini umenipa na mwasali pia, maana je kama yule msimamizi hajui umuhimu wa hizo kabrasha akatunza vibaya vikapotea. ila nashkuru
 
Mwanangu kama upo serious na hilo swala nenda ofisi ya mkuu wa mkoa ukiwa well documented achana na siasa za mtandaoni.Naamini una vitu vingine zaidi ya kujua tu kama alifanya kazi au la. Ila pia kwa heshima ya mzee wako let him rest in peace for good
 
Anataka ajue alichokuwa analipwa na TISS ili afuatilie mafao ya marehemu baba yake!
kwa nini tunakuwa na dhana hizo, yani wewe huwezi kuhitaji kujua kuhusu mzee wako. mambo yote hayo yalishafinyika nishakuwa mtu na maisha yangu mkuu
 
Hapo ni vigumu sana kufahamu mkuu kwani hawa jamaa(TISS) wanapomfunza mtu (shushushu) hawamwajiri kama usalama wa taifa bali huwekwa kwenye kada mbalimbali za taasisi za serikali hata binafsi kulingana na malengo/uhitaji..

mfano wengine unaweza kumkuta ni mwalim, asikari jeshi, polisi, magereza, madaktari nk. sasa hapo hata anapofariki process zote za mazishi hufanywa na taasisi au kada iliyokuwa imemuajiri na sio TISS, haijawahi popote kutokea eti shushushu anazikwa na idara ya usalama wa taifa ( TISS), Jiulize je hakuna wanausalama wanaokufa?

Inawezekana ukabahatika lakini si virahisi kiivo zaidi utaambiwa hawakuwahi kuwa na mtu kama huyo ijapokuwa kweli alikuwa TISS,
Good sana upo vizuri mkuu!!
 
nashkuru sana mkuu, nilikuwa mdogo kwa hiyo sikumbuki chochote, ila mambo yote ya mirathi na yanayofanana na hayo yalishakamilishwa. kuhusu msimamizi ndio unanipa mwanga ngoja niulizie nijue kama yupo na hayo mambo ya kabrasha ( kama kweli mkuu kuna kabrasha hizo ntashukuru sana kwa kweli, ila najiuliza ni kwamba siajkuelewa viabaya, kweli wanatoa hizo kabrasha? sasa kama itahitaji ruhusa wanajuaje jama huyo waliyemkabidhi hatoyatoa? au na yeye anakuwa ni mtu wa aina gani, umenipa mwanga lakini umeniap namwasai, maana je kama yule msimamizi hajui umuhimu wa hizo kabrasha. ila nashkuru

Sawasawa, ulikuwa mdogo na kila kitu kilimalizwa wakti ule.

Na miaka 20 imepita sasa, kilichobakia ni kumuenzi marehemu mzee wako kwa kupiga kazi na kujitafutia riziki kihalali, na kumuangalia mama yako/yenu.

Thats it.
 
Mpm.... Waangalie database kama yupo maana hawa watu bana.... Nilisoma na jamaa olive.. Tukaachana kati kati hapo tukakutana first degree alikua anajinasibu kama afisa maendeleo ya jamii kaja Kuongezea Elimu ila tumemaliza chuo namuona kwenye misafara ya Rais mstaafu nkastuka hivi afisa maendeleo ya jamiii na kaunda suit vinaendanaje
[emoji3] [emoji3] [emoji3] mkuu wee si umeambiwa afisa??
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom