Je, naweza kufahamu kama Mzazi wangu marehemu aliwahi kufanya kazi Usalama wa Taifa?

Status
Not open for further replies.
ha ha ha ha ah ah ah hawasomeki nakwambia.
 

wanashiriki kama marafiki tu au jamaa wengine, kwani kwenye msiba mtu akisema tu ni rafiki, au mwalimu au mfanya biashara mwenzake. au wakasema ni mchango kutoka kwa walimu wenzake. sema hawashiriki rasmi na kama aliyefariki ni mkubwa wanaweza tuma muwakilishi lakini hawajitambulishi. huu ndio uelewa wangu km nimekosea watu watasema
 
mkuu sizungumzii mazishi yake, najua wao hawakuziki kama wao kwani hufanya kazi zao kwa siri.
Hii ishu unayotaka kuifwatilia inaonekana ni ngumu na itakuumiza akili na wala hautapata ukweli.

[emoji53] embu jaribu kuchunguza nyaraka zake alizoziacha.
Na ufuatilie mawasiliano yake iwe mobile phone, computer etc.

Majibu yako kwako ww mwenyewe na huku hautakaa uyapate majibu ya kukuridhisha zaidi ya myth tu.

Ww ndo unayemhua baba ako na familia yako kwa ujumla hivyo sisi hatuifahamu.
 
mkuu bahati mbaya nilikuwa bado akili ndogo, kwa bahati mbaya hakuna hata kimoja nachoweza kukipata katika vitu vyake. kwa ufupi hakuna. kuna briefcase moja mama alinimbia lilikuwa la mzee, la zamani limefungwa kwa namba. na kwa vile mama alisafiri nilishawishika siku moja nikalivunja, kumbe mama aliweka vitu vyake yeye japo alisema la mzee. nilimuelewa vibaya nilijua mzee aliliacha kama lilivyo na halijawahi kufunguliwa
 
Njoo PM na taarifa zifuatazo; any of his phone number ya zamani, full names na his last occupation and organization.
 

Je, ni nani alisimamia mirathi ni wewe au kuna mtu maalum aliteuliwa na kupitishwa na mahakama.

Kama yupo msimamizi wa mirathi basi ataweza kupitia kabrasha la marehemu mzee wenu na kila kitu kimeandikwa mle ingawa kunaweza kuwepo kabrasha mbili..

Tatizo linakuja kama hayupo huyo mtu na pia hata kama yupo awe na ruhusa maalum ya kusoma hilo kabrasha.

Halafu hizo kabrasha zipo hard copy na soft copy na hard copy ni classified hivyo haitolewi.

Je mambo kama wasia, mirathi na akiba kwenye mabenki yamemalizwa? Maana kama mafao basi yanapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti husika kama ile ya NSSF.

Yupo mtu maalum kwa kazi hiyo.

Vinginevyo wewe chukulia tu marehemu mzee wako alikuwa ni mhasibu kitaaluma na kama kila kitu kimekamilika basi hakuna taarifa zingine pana.
 
nashkuru sana mkuu, nilikuwa mdogo kwa hiyo sikumbuki chochote, ila mambo yote ya mirathi na yanayofanana na hayo yalishakamilishwa. kuhusu msimamizi ndio unanipa mwanga ngoja niulizie nijue kama yupo na hayo mambo ya kabrasha ( kama kweli mkuu kuna kabrasha hizo ntashukuru sana kwa kweli, ila najiuliza ni kwamba kama sijakuelewa vibaya, kweli wanatoa hizo kabrasha? sasa kama itahitaji ruhusa wanajuaje jama huyo waliyemkabidhi hatoyatoa? au na yeye anakuwa ni mtu wa aina gani, umenipa mwanga lakini umenipa na mwasali pia, maana je kama yule msimamizi hajui umuhimu wa hizo kabrasha akatunza vibaya vikapotea. ila nashkuru
 
Mwanangu kama upo serious na hilo swala nenda ofisi ya mkuu wa mkoa ukiwa well documented achana na siasa za mtandaoni.Naamini una vitu vingine zaidi ya kujua tu kama alifanya kazi au la. Ila pia kwa heshima ya mzee wako let him rest in peace for good
 
Anataka ajue alichokuwa analipwa na TISS ili afuatilie mafao ya marehemu baba yake!
kwa nini tunakuwa na dhana hizo, yani wewe huwezi kuhitaji kujua kuhusu mzee wako. mambo yote hayo yalishafinyika nishakuwa mtu na maisha yangu mkuu
 
Good sana upo vizuri mkuu!!
 

Sawasawa, ulikuwa mdogo na kila kitu kilimalizwa wakti ule.

Na miaka 20 imepita sasa, kilichobakia ni kumuenzi marehemu mzee wako kwa kupiga kazi na kujitafutia riziki kihalali, na kumuangalia mama yako/yenu.

Thats it.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] mkuu wee si umeambiwa afisa??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…