Je, nchi kuchapisha pesa zake nje ya nchi ni sahihi?

^If a government cannot protect herself, if she cannot defend her own freedom and sovereignty, if she cannot help her own people to keep their properties and life, the only logical option for her is to remain a colony^ ~ Anonymous
 
Umewaza nini mkuu?
Nimewaza ingekuwa Tanzania tumepewa kazi ya kuchapisha noti za Kenya, tungewafanya kitu kibaya sana, sijui tumetumia akili za kichwani au za wapi kuwapa watu wengine kazi ya kuchapisha pesa zetu, halafu tunawalipa pesa hizo hizo walizochapisha kama malipo ya kazi yao, hivi vichwani mwetu kuna funza au ni nini?! 😂
 
Ila unahitaji lessons on ^Basics of Economy and Monetary Policy^
 
Umewahi jiuliza kwanini tuna viwanda vya sukari au karatasi lakini sukari au karatasi tunazozalisha hapa kwetu bei iko juu kuliko zinazotoka nje?

Kuchapisha pesa inahitaji uwekezaji mkubwa hasa upande wa teknolojia, ulinzi na usalama. Tukisema tuchapishe hapa usishangae tukatumia Tsh 15,000 au Tsh 20,000 kuchapisha noti ya Tsh 10,000.

Nakubaluana na wewe kwamba kuna vitu tumekubali viendelee kama ilivyokua ikifanyika awali bila kujaribu kuangalia namna gani vinaweza kufanyika kwa njia mbadala kwa ufanisi zaidi.

Sawa sawa na kuchenjulia madini nje ya nchi, ndoto za kuwa na mashine za kuchenjua hapa hapa sijui ziliishia wapi licha ya kuambiwa kwenye baadhi ya makubaliano ilikua kiwanda kijengwe nchini.
 
Kaka nimekuwa nakusoma muda mrefu tu maandiko yako, sio kweli kwamba hujui kilichopo juu ya hili au matumizi ya dawa, zote za mimea na wanyama na binadamu. Uzi naona umeuandika saa saba usiku
 
Sijakuelewa kwa kweli
 
Umewahi jiuliza kwanini tuna viwanda vya sukari au karatasi lakini sukari au karatasi tunazozalisha hapa kwetu bei iko juu kuliko zinazotoka nje?

Kuchapisha pesa inahitaji uwekezaji mkubwa hasa upande wa teknolojia, ulinzi na usalama. Tukisema tuchapishe hapa usishangae tukatumia Tsh 15,000 au Tsh 20,000 kuchapisha noti ya Tsh 10,000.

Nakubaluana na wewe kwamba kuna vitu tumekubali viendelee kama ilivyokua ikifanyika awali bila kujaribu kuangalia namna gani vinaweza kufanyika kwa njia mbadala kwa ufanisi zaidi.

Sawa sawa na kuchenjulia madini nje ya nchi, ndoto za kuwa na mashine za kuchenjua hapa hapa sijui ziliishia wapi licha ya kuambiwa kwenye baadhi ya makubaliano ilikua kiwanda kijengwe nchini.
Nani alisema inahitaji uwekezaji mdogo?
 
Back
Top Bottom