Katika harakati zangu za utafutaji nimejikuta nakodisha banda liliko lipo wazi msimu wa mwaka jana.
Mtaa ninao kaa kulikuwa na mabanda mawili ya mpira ila msimu huu jamaa mmoja hakufungua kabisa.Kupita kuuliza nikaambiwa jamaaa kashindwa kwahiyo anakodisha pale
Mimi huyo na kiranga changu nikalipia miezi kadhaa na nikanunua azam tv nikafunga nilikuwa na TV yangu inchi 43 home nikataka kuichukua wife akakataa akasema km unafungua mpira TV itakuwa huko muda mwingi tununulie hata TV ndogo
Nikamuona kama miyeyusho nikaenda kununua TV used inch 46 nikafunga fresh
Nikaeka vimatangazo vya uongo uongo basi siku ya mpira ikafika ambayo ilikuwa YANGA VS CBE .ila waliingia watu 7 tu nikarudi na 3500 ts.
Siku ikaisha hivyo na nikajipa moyo kuwa kesho ni SIMBA VS ALAHLY TRIPOL naweza nikatusua lakin pia haikuwa hivyo nikapata watu 8 tu
Nikasema hapa mbona km jau matarajio sio kabisa. Kivumbi hiki
Nikajipa moyo tena kwakuwa ni wiki ya kwanza ngoja tuangalie next game ya yanga vs cbe aman complex
La haula hii ndio ikatia fora kabisa mana walikuja watu wawili tu.
Sasa najiuliza ni kuwa ya mabango haikutosha ?? Au TV inchi 46 bado ni ndogo ?? Mana banda la pili ana inchi 43 tu na kule nyomi ila siwez laumu kwa kuwa ana experience ya muda na yule alienikodisha mimi mwanzo alikuwa na TV ndogo ndio maana nikaona kama Alikuwa anafeli
NACHOOMBA WAZOEFU NA HIZI MAMBO MNISHAURI CHA KUFANYA
dogo niliemuachia banda kaniambia tumefungua banda kitoto sana hatujazunguka kwa waganguzi.
Majirani wengine wakasema mwenzenu kashawai kwa wazee porini kwa hiyo nyie msipoangaika mtakuwa mnalipa kodi na kingamuzi hakuna hela mtapata hapo. Hii kauli imetolewa na watu watatu tofauti hapa mtaani
Chakushangaza kabisa ndugu wa mpinzani wetu kutuambia nyie yule hamumjui kama ni mchawi?
Mimi nilichomwambia dogo ni kuwa game ya simba tunaweka promotion watu 5 wa mwanzo wanaingia bure ili kuhuisha brand mana tunapoelekea ntakata tamaa mapema mno.
Wadau mna maoni gani kwenye mabanda ya mpira je kuna nginjanginja hizi za kurogana mwengine asipate wateja.
Mama mimi sijawai kwenda kwa mganga tangia nizaliwe na sina mpango huo nimeamua kama watu hawatakuja hata kwa bure Bora nifunge banda au nikatafute sehemu ambayo haina kurogana lakini sio kwenda kusema TAWIRE mana mganga anapatiaga kwa kupita mule mule na Ramli zao chonganishi.
Ni hayo wadau