Je, ndio yamenikuta kwenye banda langu la mpira?

Achana na hiyo sehemu, pengine wanaozunguka ambao ni wateja hawana mwamko, au wanaangalia kwao, kwa ujumla hakuna wateja. Achana na uchawi.
 
Unatoka nyumbani unaenda kusikiliza matusi na harufu ya ushuzi maana mtu akijamba na mlivyowengi aisee na joto la dar dunia unaiona chungu siji kufanya huo ujinga
Banda umiza au bar ndio maeneo yangu pendwa kucheki mechi..
Lile vibe kama upo live uwanjani, home unakua uketulia kama msibani vile.
Kule unakutana na wachambuzi wa mchongo wa kila namna.

Na sio kila banda umiza ni la hovyo, yapo yaliyojengw vizuri, makubwa na tv kubwa unaona vizuri kama upo kwako.
 
Bandaumiza sio la kukaa mtu unajielewa ukiona unaangalia mpira Bandaumiza ujue hujielewi jitafakari unazidisha safari ya huo umasikini wako
 
Kuna mtaa bar mbili zimekaribiana, kwenye mechi ya azam na kmc, bar moja iko nyomi mpaka viti vya kukaa vimekua vichache ila bar nyingine haina mtu hata mmoja sio mteja wala muangalia mechi.

Hii kitu acha tu.

Mkuu na pia wewe na huyo msimamizi wako tengenezeni marafiki na mlitangaze banda lenu bila kusahahu ushauri murua uliotolewa na Mad Max hapo juu.

Hiyo azam watu wengi wanayo majumbani mwao, ungeweka na ligi za ulaya esp epl ungedaka wengi.
 
Bandaumiza sio la kukaa mtu unajielewa ukiona unaangalia mpira Bandaumiza ujue hujielewi jitafakari unazidisha safari ya huo umasikini wako
Kama kujielewa au kutojielewa kwako ni kuangalia mpira banda umiza basi uko sahihi kwa upande wako jombaa.
Sikupingi.
 
Jiulize kwanza kwa nini mmiliki wa awali alilikodisha kwako
 
Chukuaa chumvi ya mawe wafishia hilo banda weka na malimao 3 asbh na jion njoo unipemrejesho
 
Hakuna cha uchawi hapo..wewe chakufanya kua tu mbunifu wa kazi yako.

Nb: sisi wenzako kule tunafataga vibe tu kutoka kwa wadau wetu wa soka.
 
Hakuna cha uchawi wala nini, mteja akishazoea sehemu huwa ni kama addiction, hivyo mwenzako ana wateja wake. Wewe tengeneza ladha yako upate wateja wako, usisibiri tu siku za mpira, jiongeze hata kuweka vipindi fulani au muvi siku za kawaida kulingana na mapendeleo ya watu wa hapo. Afu iwe ni free kuangalia. Ukiweza ongeza na playstation mbona utawapata wateja.
 
Ungenunua projector uachane na habari za Tv inchi 43.

Weka vinywaji bure hizi soda za jerojero na energy drinks.

Promotion ya bure kwa baadhi ya mechi hasa zile zisizo na umuhimu sana. Au unaunganisha bei kwa mechi mbili .

Angalia viti vya kukalia ( umeweka mabenchi /viti au nini?)

Weka Mafeni na Spika kubwa zinazotoa mlio mkubwa nje ili watu wajue kuna mpira unaendelea.

Inahitaji muda na pesa ili kuisimamisha biashara. Pia mwanzo usijiwekee matarajio ya faida , focus tu kwenye kuhakikisha pesa ya king'amuzi na umeme inapatikana.

Taratibu utaanza kuvuta wateja na kupelekea natural death kwa biashara ya mshindani wako.

Pia kila banda huwa kuna staffs , yaani wale watu machachari kwenye kushangilia na kuongea ongea ,utani mwingi wakati mechi zinaendelea.Hawa unatakiwa uwape free tickets kwasababu huchangia kuvuta wengine waje.

Mwisho mabango yako unatakiwa uyatege sehemu tofauti tofauti ili watu wajue ulipo na pia jinsi unavyochora matangazo yako na chaki unatakiwa uwe mbunifu ili kuvuta wateja mfano Ujugu.
 
chala41 uko mkoa gani mi nakupeleka bariadi ukaganguliwe ukirudi utaona moto.

Chungua udongo kwenye kona 4 za hilo banda, chukua na udongo wa katikati pamoja na huko wanakoingilia wateja wako.

hakikisha hautumii mkono wako.

Biashara za uswahilini hazihitaji branding usidanganywe my friend.

Uswahilini ni mambo ya witchcraft tu hakuna la ziada.

Hizo gharama za router sijui free wifi na nini we zikusanye uje tukupe maelekezo
 
Toa ofa ya bia za bure na energy drink bila kusahau sigara ndogo na kubwa kwa mwezi mmoja.
Biashara inataka uwe na mtaji sio njaa njaa tu huwezi kutoboa.
 
Nakupa mbinu jamaa yangu uswahilini kwetu alivyopata wateja

Kitaa Kuna mwana alikua anakimbiza sana,alikua peke yake..watu nyomi,jamaa akaanza kiburi na kujisikia na dharau kwa wateja,

Jamaa yangu akafungua banda kubwa zaidi ya lile,zuri zaidi ya lile,akaweka feni,radio kubwa,milango ya kutokea miwili..

TVs mbili inchi 72,moja EPL moja Vodacom premier league..

Halafu akajaza ma stolo wei(stoy away) waingia bure..

Weekends hata games ziwe 5,mechi ZOTE JERO (500) wakati kwa jirani yake ilikua kila mechi unalipia.,

Hadi now naandika hivi jamaa kwa siku kupata laki 3 hadi mbili kawaida..na kila mechi jero,big games kiingilio buku,,ikitokea Manchester na simba or yanga muda mmoja, kiingilio buku..na kaiba wateja wa jamaa WOTEEEEE


Ushajifunza kitu?? Mdau huko juu kakwambia ungeweka bure week ya kwanza,mimi ningeweka hata two weeks...hakuna uchawi know the game
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…