Je, ndio yamenikuta kwenye banda langu la mpira?

Hakuna cha uchawi hapo..wewe chakufanya kua tu mbunifu wa kazi yako.

Nb: sisi wenzako kule tunafataga vibe tu kutoka kwa wadau wetu wa soka.
Upoo mkuu aujakufikia tu

Kuna bar 2 hapa mtaan

Ajabu hata mm naruka bar ya kwanza nzuri kilakitu mechi projector. Kubwaa uliza wote tukikaribia tuanfunga macho

Na ina mabinti wazuri
 
Hilo banda lipo wapi
 
Banda umiza lina vibe sana hasa goli likifungwa, kuna wadau wanasimamisha hadi feni kwa kuishika kwa mkono na hawahofii chochote.
 
Kwani hujawahi kuona bar mbili ziko karibu moja inajaa nyingine haijai?
Huyo mwenzio ana wateja wake. Sasa na wewe tafuta wateja wako au mnyang'anye wateja kwa kuwa na kitu bora zaidi sio utopolo ule ule.
Hili ndio anapaswa kufanya aongeze ubunifu...anaweza kuanza kwa kutafuta wapiga kelele wawili wa kuleta amsha amsha bandani, pia aboreshe banda kwa kuliweka kwenye usafi wa hali ya juu.

Hata kwenye kuandika mechi ubaoni aandike na kuongeza maneno ya mbwembwe.
 
Upoo mkuu aujakufikia tu

Kuna bar 2 hapa mtaan

Ajabu hata mm naruka bar ya kwanza nzuri kilakitu mechi projector. Kubwaa uliza wote tukikaribia tuanfunga macho

Na ina mabinti wazuri
Vibe! Vibe! Vibe! Ndio kinachofanya uruke hyo bar uende bar ya jirani. Ukiwa mfanyabiashara hasa wa sehemu za starehe jikite sana kwenye kutengeneza vibe.
 
Pole na hongera mkuu kwa kujaribu.
Biashara hiyohiyo na mimi naifanya,nina mwezi na week 2 sasa, kuna wakati zaidi ya mara tatu au nne uwa nafungua hakuna hata mtu anaingia,yaan nawasikia kabisa watu wanapita nje na najua kabisa hawa wanaenda kuangalia mpira.
Uzuri au ubaya mimi bandani hapo nakaa mwenyewe. Mwanzoni ilinitesa sana ila sasa nmeshajifunza kukubaliana nayo.
Kama walivyosema baadhi ya wachangiaji,hakuna mafanikio yanayokuja haraka,jipe muda,acha watu wafahamu kuwa hapo kuna banda,ikizoeleka watakuja tu, binafsi nmeamua kuamini hivyo ili niweze kuendelea kufungua lakini pia inipunguzie huo msongo wa mawazo
 
Kanchi 43 munaangalia mwezi weka chombo 75 au 80 na spika ya singeli uone vibe lake always ukifanya kitu fanya bora zaidi hiyo 43 inatumwa chai tu .Hiyo ni football kaka inataka kioo kikubwa.
 
Banda umiza ninalotumia hata sio zuri ila lina vibe mno. Navuka 4 star hotel ina ukumbi nje mule sitaki kutazama mpira na wanywa bia hawajui kitu kwenye mpira, navuka banda jingine zuri naenda mbali kukutana na banda limejaa bodaboda. Hao boda wanajua sana ubishani wa mpira, formation, mbinu za kocha, kosa liko wapi, nani atoke sub aingie nani.

Kwa vile sijui mpira huwa napenda niwasikilize wao uko kwingine nikienda huwa simalizi mechi naondoka. Na ambavyo sina team nikienda lile banda huwa nafurahia kuliko nikitazama kwingine. Kwahiyo nahisi ni mazoea tafuta watu wenye ushawishi uwape ofa wavute na wengine.
 
Yaani hadi banda umiza watu wanaroga...

Ndio maana kuna muda unajikuta ushafika banda umiza hata hujui umefikaje na umeacha TV maskani...
Nimecheka sana ... wachawi noma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…