Ndoa ni njema sema watu hatuna elimu nayo na wanaotakiwa kuifundisha hawaijui.
Ndoa ndio kitu kinachoshikilia mahusiano ni mfano wa msumari na gundi unaounganisha mbao mbili ili ziweze kushikina na kuunda chombo kabati ukiiona imekamilika Ila imeunganisha na vipande vipande vya mbao mpaka kuwa kama ilivyo. Ndio ndoa ilivyo.
Pasipo ndoa hakuna mahusiano kwani kila mmoja anakuwa huru ni sawa na vipande vya mbao uviite kabati, meza n.k haiwezekani kabisa.
Shida inakuja watu hawalitambui hili pindi waingiapo kwenye ndoa.
Utamu wa ndoa unakuja hapa.
1. Unapunguza gharama za huduma kwa mwenza wako na kubakia huduma za msingi tu nazo ni pale kuna po kuwa na uwezekano tu mfano vizawadi zawadi ili kumfurahisha mwenza wako vinakufa. Hakuna uchunwaji kwenye. Mahitaji ya msingi ni kula, kunywa, Malazi, mavazi, na matibabu. Mke akipata hivi inatosha hivyo vingine ie kusuka, outing n. K ni pale mume apatapo nafasi tu si lazima. Kinyume na mahusiano nje ya ndoa huwa ni kipengele.
2. Mahusiano kuwa na usalama. Kuna ugoni kwenye ndoa sio rahisi kwa mtu kumkurubia mkeo au mumeo. Hata ukiugua una haki ya kuhudumiwa na mwanandani wako. Kinyume na nje ya ndoa huwa ni kipengele.
3. Upatinaji na tendo la ndoa ni asilimia Mia moja wakati wowote mpatapo nafasi.
1 Wakorintho 7
1. Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
2. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
3. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
5. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Nb. Akikunyima hata Mara moja pasipo sababu za msingi huyo ni huyo ni mzinzi hufungwi kumpandisha cheo kuwa mke au mume mkubwa.
Hitimisho; Ndoa ndio mwisho wa matumizi ya hovyo hovyo na maisha ya hovyo hovyo na inapaswa kuheshimiwa na watu wote hasa waliomo Ndani wanapaswa kuzingatia masharti yake na kuiheshimu sana. Sasa shida inakuja mtu anaingia kwenye ndoa anaanza kuleta za kuleta usipomtoa out, usipolnunulia wig Jipya, gari, usipomfungulia biashara, mkikosana kidogo, akila chakula asichopenda ananuna na kwanza kuleta shida ndio wanaoidhalilisha ndoa na kuifanya kukosa maana.