ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
- #281
Soma pitia comment kama unawezaThanks, naweka kambi hapa.
Soma pitia comment kama unawezaThanks, naweka kambi hapa.
Mkuu hiki ni sahihi kabisa,Ni ndoto chache hutokea kwa mfumo huo ukilinganisha na ndoto nyingi tunazoota huwa hutumika sana metaphor ndio maana wewe unaona kama ndoto unazoota ni za ujinga ujinga kwa sababu ya kushindwa kuzielewa.
Kuna wakati mtu anaweza kuota tukio fulani kisha akaja kuona tukio la kweli vilevile kwenye uhalisia kama alivyoota, kwahiyo ni vitu ambavyo vipo ila ni kwa uchache sana.
Kwahiyo kikawaida huwa tunaota tu hizo ndoto za matukio yajayo ila sema huwa tunashindwa kuzielewa wakati huo na tulivyo kwamba sio wafuatiliaji wa ndoto basi ndio kabisa.
Katika mada zangu pasua kicwa hii ni moja wapoNipo hatua kwa hatua na comment kwa comment. Tena nashukuru sana maana Uzi Bado ni mpya na watu wanatiririka vizuri sana.
Lakini mpaka Sasa page ya pili Bado watu wengi wanajibu ni kama ubashiri tuu Yaani hakuna fact unayoweza kuiweka sahihi kabisa kama ulivyouliza swali lako na mifano Yako.
Binafsi wanaosema ndoto ni mfumo wa akili/ubongo kuchanganua mambo Mimi nakataa kabisa maana akili hufanya jambo imefundishwa kufanya na ubongo ni kuitunza kumbukumbu tuu. Sasa Kuna muda unaota vitu ambavyo hujawahi kuviona, kuviwaza wala kuongea na mtu, Je! Akili huyatoa wapi hayo mambo??? Hapa ndipo nakataa kwenda na Hawa watu wanaoamini kwamba ni ndoto ni psychological thing, cos anything psychological must consist of fact and fact is among of touched things or seemed.
Hivyo kusema ndoto inahusiana na ubongo au daily activity hilo nalikataa totally.
Ila binafsi naamini ndoto ni spiritual thing na siku zote nimeamua kujiaminisha hivyo kwasababu zifuatazo-
Mosi: Mtu ni muunganiko wa vitu vitatu Yaani Roho, Moyo na Akili. Twende pamoja namimi hapa Kuna usemi fulani watu husema UFUATE MOYO WAKO ILA USIIACHE AKILI YAKO.
Sasa ili mtu aweze kukamilika ni lazima hivi vitu vitatu viungane na vyote viwe na maamuzi ya pamoja, Yaani MOYO wako ukubali na AKILI yako iweke fact zake lakini pia ROHO Yako( kuhusu ROHO hapa nazungumzia wasiwasi) binafsi Huwa naamini kwamba wasiwasi sio zao la akili bali huyu ni ROHO, watu wa Ibada sana humuita mtu wa ndani, wengine husema MACHALE yalinicheza.
Sasa ili mtu aweze kukamilika ni lazima hivi vitu vitatu viweze kuzungumza lugha moja na kuifanya akili iweze kufanya maamuzi.
Hivyo bhasi mimi naamini kwamba ndoto ni njia ya ROHO kuzungumza na AKILI kuhusu mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo pia naamini ya kwamba Kuna muda tunaota ndoto kwasababu ROHO inataka itambulike uwepo wake kwetu yaani ROHO inacreate awareness kwenye akili zetu.
Duh aisee🤔Mkuu hiki ni sahihi kabisa,
Binafsi naamini ndoto hunijulisha mambo matatu Yaani Mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo.
Mfano Kuna kipindi nilikua Tanga nalima, nyumba niliyopanga ilikua kijijini sana Yaani ushirikina wanafanya wazi na nje nje.
Nikitoka shamba nilikua na tabia ya kukaa nje kwenye valanda Sasa watoto wengi walikua wanapenda kunifuata nilipokaa, Aisee! Kila mtoto alikua amevalishwa hirizi, wengine shingoni, wengine mikononi, wengine viunoni kile kitendo kilinishangaza sana.
Siku moja niliona kamba imefungwa juu ya mlango wa kuingilia geto nikakata ule uzi nikaenda kuutupa chooni kumbe sijui ndio ilikua network ya mama mwenye nyumba aisee!😂🤔. Usiku wake nilikua kama naota ndoto lakini ilikua na uhalisia Yaani aliingia geto mtu mweusiii alafu amevaa mask ya kasuku pia sehemu ya macho ya ile mask inatoa miale miekundu nikabaki namshangaa yule mtu akapotea baadae nilishtukia amenikalia kifuani halafu ananikaba shingoni, nikaanza kupambana nae huku nasema kwa jina la YESU kwa jina la YESU, nilipokuwa nasema vile ile miale ya miekundu kwenye macho ikawa inapungua nguvu baadae kabisa aliishiwa nguvu, nikamgeuza nikamkalia alafu nikataka kumvua ile mask ili nimfahamu sura, aisee alipotea palepale.
Zilipita kama siku 3 pasipo kuonana na yule mama mwenye nyumba kitu ambacho haikuwa kawaida ila siku ambayo nimeonana nae aliniogopa alafu neno la kwanza aliniuliza UMEOKOKA? nikamjibu ndio akabaki kimya hapo nikajua ni yeye ambaye alikuja usiku.
Hivyo Mimi naamini ndoto ni uhalisia wa maisha yetu ya Kila siku