Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Nimesoma Uzi wa member mmoja humu kuhusu adhabu za matofali wapewazo wanafunzi nikakumbuka miaka nikiwa nasoma.
Shule bila adhabu inakuwa ya kiduwanzi kichizi. Yaani inakuwa ya kimama. Raha ya shule iwe na hekaheka bhana! Yaani shule Kama ipo na Kuku WA broiler.
Shule gani haina Wezi
Shule gani haina matukio ya Mapenzi,
Shule gani haina matukio ya ubabe,
Shule gani haina mabifu ya kimapenzi baina ya waalimu na wanafunzi 😀😀.
Shule gani haina wanafunzi wavuta bangi, hiyo ni shule au utopolo.
Shule gani haina Watoro waliobobea,
Shule gani ambayo muhula unaisha hakuna hata mwanafunzi aliyepewa Suspension. Hiyo sio shule.
Shule gani haina walozi au wapenda kwenda Kwa waganga,
Shule gani hiyo isiyo na manabii na walokole pamoja na Maostadhi wenye misimamo mikali. Hiyo sio shule.
Kila Mwanafunzi akiwa shuleni anakuwa na kitengo chake kulingana na nature yake.
Adhabu za kikulungwa ambazo zinabamba ambazo Taikon ninazielewa ni hizi;
1. Kupiga matofali
2. Kuchimba visiki
3. Kuchimba mawe kwenye Shamba la shule lililopo Mlimani. Hii adhabu ndio nyoko kuliko zote hapo juu ikifuatiwa na yakuchimba kisiki.
4. Kupasua vigogo/Juni
5. Kuchimba mashimo
Adhabu laini laini;
1. Kuchapwa
2. Kufagia au kudeki Darasa/ofisi/bweni
3. Kudeki chooni
4. Kumwagilia Bustani
5. Kuokota karatasi au kuzoa taka
6. Kumwagilia Bustani.
Adhabu ambazo niliwa kuzifanya na makosa yake.
1. Kupiga tofali 200 kutokana na kuiba chakula cha waalimu na kukila chote😀😀.
Tulikuwa wanafunzi watatu tuliokamilisha Jambo Hilo.
Alafu baada ya Kula tukawaandamanisha wanafunzi wasile Makande kwani wamepikiwa Wiki nzima. Muda huo Sisi tumeshashiba,
Tulimshawishi Headboy na kumchochea akafanya hivyo bila kujua Sisi tuna agenda yetu ya Siri. Hiyo ilikuwa Kidato cha nne.
Baadaye Sisi tulichapwa viboko sita mbele ya shule na adhabu ya kupiga tofali kila mmoja 200 na viongozi akiwepo kiranja wakapwa suspension na wakija waje na tofali 200.
2. Kuchimba visiki Kwa kosa la Kusababisha Fujo kwenye mchezo wa mpira baina shule yetu na shule ya jirani iloyokuja kucheza pale shuleni.
Tulipewa Visiki viwili viwili.
Hii adhabu sio nzuri😀😀 ni Kama Ile adhabu ya kuondoa mawe kwenye Shamba la shule.
3. Kutoa Mawe kwenye Shamba la shule Kwa kosa la kutokomea siku ya Outing Day. Shule yetu kila jumapili ya mwisho wa mwezi ilikuwa siku ya kutoka kwenda kuzurura bila haya ya kuomba ruhusa Kwa sharti la kuwahi Kurudi kabla ya saa 12jioni.
Tukaondoka kutoka Matema Beach Mpaka Mbeya Mjini. Tukakaa huko tukarudi kesho yake jioni😊😊. Bakora kisha adhabu ya kuchimba nawe.
Nilipewa jiwe Moja, ambalo Kwa juu nililiona dogo kumbe limeenda chini. Mbona nilimenyeka. Hapo ilikuwa chini ya Safu ya mlima Livingstone.
Adhabu zingine zilikuwa za kawaida Ila hizo hapo sio mchezo. Unamenyeka Haswa.
Je, ni adhabu gani uliyoifanya shuleni ambayo hautaisahau?
Wasalamu!
Kwa sasa Dar es salaam