Je, ni adhabu gani uliyoifanya shuleni ambayo hutoisahau?

Je, ni adhabu gani uliyoifanya shuleni ambayo hutoisahau?

Wakuu kama kuna mtu anaifaham KIZUKA Atanishuhudia...
KOSA..NILIKUTWA NA PULI LA GANGA KWENYE SOCKS ASSMBLE.(zilikua kama stick 72)
1.NILILIMA NUSU HEKA KWA MKONO.
2.NILICHIMBA SHIMO FT 8.
3.WAKANIBUZA FIMBO 82-96.
Then nichague Suspnsn ya miezi 6 AU kusafisha mabanda ya nguruwe na kuziogesha miez 6...
NB:NLICHAGUA KUOGESHA NGURUWE.
Hahahahah [emoji1787],hawaja kupeleka kule kwenye kuibeba dunia au chumba Cha kiza!?
 
Nakumbuka siku wanatangaza viongozi Assembly na Mimi nilikuwa kwa list ila Mimi nilikuwa hostel na rafiki yangu mmoja tumepewa adhabu ya kuchimba shimo la urefu wetu na matron kisa tumechelewa kutoka bwenini asubuhi
 
Kuchimbua kichuguu na kumtoa malaika; kosa ni kuongea kiswahili
 
Kwema Wakuu!

Nimesoma Uzi wa member mmoja humu kuhusu adhabu za matofali wapewazo wanafunzi nikakumbuka miaka nikiwa nasoma.

Shule bila adhabu inakuwa ya kiduwanzi kichizi. Yaani inakuwa ya kimama. Raha ya shule iwe na hekaheka bhana! Yaani shule Kama ipo na Kuku WA broiler.

Shule gani haina Wezi
Shule gani haina matukio ya Mapenzi,
Shule gani haina matukio ya ubabe,
Shule gani haina mabifu ya kimapenzi baina ya waalimu na wanafunzi [emoji3][emoji3].
Shule gani haina wanafunzi wavuta bangi, hiyo ni shule au utopolo.
Shule gani haina Watoro waliobobea,
Shule gani ambayo muhula unaisha hakuna hata mwanafunzi aliyepewa Suspension. Hiyo sio shule.

Shule gani haina walozi au wapenda kwenda Kwa waganga,
Shule gani hiyo isiyo na manabii na walokole pamoja na Maostadhi wenye misimamo mikali. Hiyo sio shule.

Kila Mwanafunzi akiwa shuleni anakuwa na kitengo chake kulingana na nature yake.

Adhabu za kikulungwa ambazo zinabamba ambazo Taikon ninazielewa ni hizi;
1. Kupiga matofali
2. Kuchimba visiki
3. Kuchimba mawe kwenye Shamba la shule lililopo Mlimani. Hii adhabu ndio nyoko kuliko zote hapo juu ikifuatiwa na yakuchimba kisiki.
4. Kupasua vigogo/Juni
5. Kuchimba mashimo

Adhabu laini laini;
1. Kuchapwa
2. Kufagia au kudeki Darasa/ofisi/bweni
3. Kudeki chooni
4. Kumwagilia Bustani
5. Kuokota karatasi au kuzoa taka
6. Kumwagilia Bustani.

Adhabu ambazo niliwa kuzifanya na makosa yake.
1. Kupiga tofali 200 kutokana na kuiba chakula cha waalimu na kukila chote[emoji3][emoji3].
Tulikuwa wanafunzi watatu tuliokamilisha Jambo Hilo.
Alafu baada ya Kula tukawaandamanisha wanafunzi wasile Makande kwani wamepikiwa Wiki nzima. Muda huo Sisi tumeshashiba,
Tulimshawishi Headboy na kumchochea akafanya hivyo bila kujua Sisi tuna agenda yetu ya Siri. Hiyo ilikuwa Kidato cha nne.

Baadaye Sisi tulichapwa viboko sita mbele ya shule na adhabu ya kupiga tofali kila mmoja 200 na viongozi akiwepo kiranja wakapwa suspension na wakija waje na tofali 200.

2. Kuchimba visiki Kwa kosa la Kusababisha Fujo kwenye mchezo wa mpira baina shule yetu na shule ya jirani iloyokuja kucheza pale shuleni.
Tulipewa Visiki viwili viwili.
Hii adhabu sio nzuri[emoji3][emoji3] ni Kama Ile adhabu ya kuondoa mawe kwenye Shamba la shule.

3. Kutoa Mawe kwenye Shamba la shule Kwa kosa la kutokomea siku ya Outing Day. Shule yetu kila jumapili ya mwisho wa mwezi ilikuwa siku ya kutoka kwenda kuzurura bila haya ya kuomba ruhusa Kwa sharti la kuwahi Kurudi kabla ya saa 12jioni.

Tukaondoka kutoka Matema Beach Mpaka Mbeya Mjini. Tukakaa huko tukarudi kesho yake jioni[emoji4][emoji4]. Bakora kisha adhabu ya kuchimba nawe.

Nilipewa jiwe Moja, ambalo Kwa juu nililiona dogo kumbe limeenda chini. Mbona nilimenyeka. Hapo ilikuwa chini ya Safu ya mlima Livingstone.

Adhabu zingine zilikuwa za kawaida Ila hizo hapo sio mchezo. Unamenyeka Haswa.

Je, ni adhabu gani uliyoifanya shuleni ambayo hautaisahau?

Wasalamu!

Kwa sasa Dar es salaam
dar_story_1663157627952683.jpg
 
Nakumbuka siku wanatangaza viongozi Assembly na Mimi nilikuwa kwa list ila Mimi nilikuwa hostel na rafiki yangu mmoja tumepewa adhabu ya kuchimba shimo la urefu wetu na matron kisa tumechelewa kutoka bwenini asubuhi

Ulikuwa sister Duu sio?
 
Dah! Kipigo kama hicho nilikipataga nikiwa Form One Kantalamba sema mimi ilikua Smart Area,nilichezea bakora zisizo na idadi kutoka kwa Headmaster huku mabroo wa advance wakiwa wamenishikilia chini kama wanachinja Ng'ombe mpaka fimbo ikachakaaa


😂😂😂😂

Mpaka unakuwa maarufu
 
Back
Top Bottom