Je, ni adhabu gani uliyoifanya shuleni ambayo hutoisahau?

Je, ni adhabu gani uliyoifanya shuleni ambayo hutoisahau?

Mie nilikuwa mtoro sugu.... nilikuwa siendi shule hata mwezi mzima lakini walimu na wanafunzi wenzangu wananiona Kariakoo kwenye mishe zangu. Na bado baadhi ya walimu nilikuwa nawakopesha pesa sasa wakakosa la kunifanya.

Sasa kuna siku nimeenda zangu shule baada ya utoro wa karibia miezi miwili, nimefika class kama kawaida mara anaingia mwalimu mpya wa Physics(Mpya sababu sikuwahi kumuona).

Anadai aliacha notes na anakagua ambao hawajaandika. Kufika kwangu anaona sura ngeni. Ikabidi aniulize wewe umehamia hapa?

Darasa zima likaangua kicheko.[emoji23][emoji23][emoji23] ikabidi awaulize mbona mnacheka, wakamjibu huyo sio mgeni. Yule ticha kwa unoko akaenda kuchukua attendance ili atizame mahudhurio yangu.[emoji23][emoji23][emoji23]

Bwana wee si akaona nina muda mrefu sijafika shule. Akasema nimfate mpaka ofisini, na bahat nzuri nikamkuta yeye na mwalimu mwingne mgeni wakawa wananiuliza maswali ya kejeli. Na mie nikawa nawajibu kwa dharau.

Si waka-panick wakaamua wafunge mlango kwa ndani ili wanipige. [emoji23][emoji23][emoji23]
Asee niliwagezia kibano niliwabonda hadi wakaanza kupiga kelele za kuomba msaada.

Yani hadi kuja kufunguliwa na ufunguo wa akiba huko nje walimkuta mmoja ameshavimba manundu na mwingne yupo chini ana bleed puani. [emoji23][emoji23][emoji23]

Ila daaah... baadae yake ilipigwa kengele ya emergency na kupelekewa assemble then kupigwa fimbo 6 na kupewa suspension ya mwezi mzima. Na mzazi wangu akaitwa.

Mtaniwia radhi kwa uandishi wangu mbaya.
Chai Tena imepoa!...
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
Hivi vyuoni kunaadhabu zaidi ya kufukuzwa Chuo?
Anhaaa kaka kuna adhabu mbona , nishapewa suspension karibia na UE pia nishafukuzwa chuo huku nakabiziwa kwa maafande ila Mungu mwema kote nilipita swafi baada ya Mungu kuwatuma malaika zake.
 
Niliwahi mzingua madam flani,, nikapigwa sunspaah after two weeks nikatakiwa nirudi na mzazi,,, Bi mkubwa nikapanda nae assemble akaomba msamaha kwa niaba yangu ,,

Hii iliniadhibu psychologically maana aliongea kwa uchungu machozi yakimlenga lenga,,, nkaacha mafujo japo fimbo na adhabu nyingine hazikusaidia
 
Back
Top Bottom