Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

sasa kodi ya nyumba ikiongezeka na bei za vitu vingine pia si inaongezeka, so huwezi kusema utakuwa unapata hela zaidi kwa sababu hela itakuwaimeshuka thamani pia
 

Maoni yako niya msingi tena ni very valid. Zipo nyumba sasa hivi maeneo kama sinza ambazo ziko vey outdated and old fashion mpaka inakua ngumu kupata wateja. Nyingi roof iko chini sana
 

Angalizo lako la mwisho nila kuzingatia
 
Pamoja na andiko lako, niseme kwa ufupi tu kuwa - nyumba kama nyumba - hasa kama ni kwa matumizi ya kulala na kuishi humo ndani, HAS AND WILL NEVER BE AN ASSET. Hasa hasa kama unajua maana ya ASSET. NYUMBA YA KUISHI NI LIABILITY, yaani inakutoa fedha kila wakati ukitaka kufanya matengenezo, kulipa bili za maji au umeme na mambo kama hayo. Tujitahidi kujenga nyumba ziwe ASSETS. Siku moja tutaongelea nini maana ya ASSETS NA LIABILITIES katika maisha yetu ya kila siku.
 
Hivyo viwango ni vya mwaka mmoja. Mfano TZS 100,000,000 kwa 3% kwa muda wa miezi mitatu = 100,000,000 X 3% X3/12 = TZS 750,000 faida kwa hiyo miezi mitatu. TRA watachukuwa hapo 10% kodi ya zuio hivyo utalipwa TZS 675,000
TPB wanatoa 12.0% per annum. Ila nasikia wanataka sitisha Sasa.
 
Pia uwekezaji wa kodi unayoipata kwa kila mwaka ni njia nyingine inayoweza kumtoa mtu. Hiyo kodi ya laki 6, kwa mwaka ni sh mil 7.2. Ukipokea hii mil 7.2 unanunua nguruwe, au kuku au bajaj au chochote unaendelea kupata faida zaidi na zaidi.

Usiangalie ile kodi tu, angalia hiyo kodi inazalisha nini?

Pia baada ya miaka 20, hiyo bado nyumba itakuwepo hata kama itahitaji marekebisho madogo. Kwa kweli uwekezaji kwenye real estate ni mzuri sana

utakopa fedha bank, utapata kodi utalipia mko[po kidogo kidogo n.k

Ushauri: Jenga nyumba ndogo (nyumba 2, jiko dogo na kasebule mil 20 tu pangisha kwa lak 2.5, hutajutia kamwe.
 
Nyumba ni Asset bana hata kama ni ya kuishi. Kama ni liability si uigawe bure uondokane na hizo gharama ukapange?
 
Nyumba ni Asset bana. Kama ni liability si uigawe bure uondokane na hizo gharama?
Kwa ufupi tu, ASSET ni kile kitu kinachokuingizia PESA! Chochote kinachokuchulia PESA ni LIABILITY. Nyumba ya kuishi tu ni liability inachukua PESA in forms of kodi/malipo ya umeme, kodi ya ardhi, kodi ya jengo n.k. Lakini ka a umeipangisha, itakuletea PESA utakayotumia kulipia hizo bili. Hautatoa hiyo PESA kutoka kwenye aidha mshahara wako au vyanzo vingine vya mapato. Hiyo ni kwa ufupi tu.
 
Nyumba ya Mil 20 upangishe kwa Laki 2.5 kw mwezi labda kama imejengwa Posta au kkoo...!!
 
Naomba niulize swali mkuu....kua magari yale ambayo ni 'rare' sana kiasi cha kwamba yanauzika bei nuksi.
Je ni ASSET ama LIABILITY maana zinahitaji matunzo kama magari mengine lakini akija iuza ana uwezo wa kudabo au kutripo bei aliyonunulia?!
 
Mkuu uwekezaji kwenye nyumba ni moja ya uwekezaji wenye faida ya uhakika,biashara sio kila mtu anaweza kufanya na kila siku bei ya nyumba inapanda hata kwa hiyo dollar ya mmarekani ambayo dhamani yake iko stable
 
Hapo kwenye bold ndo point yenyewe!
So ina maana nyumba ya kuishi si liability moja kwa moja na si asset moja kwa moja....inategemea na malengo & wakati husika si ndivyo
 
Hapo kwenye kodi ya nyumba kuna mambo 2
Kwanza hiyo kodi ya laki sita haitabakia hiyo hiyo itapanda kila mwaka
Pili nashauri uanzishe mradi mwingine mbali na hiyo nyumba hali ikiruhusu.
 
Hongera sana asee. Ukipiga hesabu mpk sasa hyo mil 30 yako haijarudi na faida kabisa
 
Wengi wanawekeza kwenye nyumba kwa sababu hawako tayari kuanzisha biashara zinazohitaji usimamizi makini...na mara nyingi wanaojenga nyumba za kupangisha fedha yake huwa hairudi.Nashauri kama unaweza kujenga nyumba ya kupangisha,ni bora ujenge lodge ndogo ya kisasa uwe unapata pesa kwa siku.
 
Hiyo rental yield % unaipataje ndugu?
 
Naomba niulize swali mkuu....kua magari yale ambayo ni 'rare' sana kiasi cha kwamba yanauzika bei nuksi.
Je ni ASSET ama LIABILITY maana zinahitaji matunzo kama magari mengine lakini akija iuza ana uwezo wa kudabo au kutripo bei aliyonunulia?!
Hoja au kigezo au kipimo ni kuwa je hilo gari, pamoja na bei yake mbaya, linakuingizia PESA SASA?! Hiyo ndiyo THRESHOLD, kigezo au kipimo kwa sasa. Ukiliuza hapo baadaye na kukupa mahela mengi, hapo sasa ni ASSET. Kitu KINACHO KUINGIZIA PESA ndiyo ASSET. Vinginevyo ni LIABILITY!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…