Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Mbona mnatupigia hesabu za UPE(Ualimu pasipo Elimu)? Yaan kwa miaka 29, kodi itakuwa hiyohiyo laki 6? Haiongezeki? Ni nani hapa amewahi kupanga nyumba na kulipa kiasi kile kile kwa miaka hata 5?

Inawezekana hii biashara ya nyumba za kupanga haina faida kivile. Basi tuipinge kwa hoja za kweli, sio za kuungaunga.
sasa kodi ya nyumba ikiongezeka na bei za vitu vingine pia si inaongezeka, so huwezi kusema utakuwa unapata hela zaidi kwa sababu hela itakuwaimeshuka thamani pia
 
Leo hii nikijenga nyumba yangu kwa Mil 50. Mpaka inafika miaka 10 au 15 mambo mengi sana yatakuwa yamebadilika; Nitatakiwa kufanya marekebisho pale itakapohitajika, teknolojia kwenye suala zima la ujenzi zitakuwa zimebadilika kitu kitachofanya materials nyingi nilizotumia katika ujenzi wangu kuonekana sio za kisasa tena( mfano nyumba yangu niliezeka bati za Champion leo hii katika ulimwengu wa mabati ya Rangi kama rangi kama Romantile, Versatile, Tekdek lazima nyumba yako ionekane ina bati la enzi za ukoloni pengine ukute bei ya bati kwa wakati huo inaendana kabisa na hii ya sasa kwa kiwango cha Rangi),design ya nyumba yako nayo pia inaweza ikawa ishapitwa na wakati kitu kitachofanya nyumba yako ionekana sio ya thamani hiyo ambayo unataka kuiuza.

Hivyo basi, ili nyumba yako iwe na ubora wa kuuzika kwa wakati huo lazima uipandishe hadhi kitu ambacho kitakulazimu uingie gharama nyingine.

Maoni yako niya msingi tena ni very valid. Zipo nyumba sasa hivi maeneo kama sinza ambazo ziko vey outdated and old fashion mpaka inakua ngumu kupata wateja. Nyingi roof iko chini sana
 
naamini kuwa watu wengi hukimbilia kujenga sababu aidha ya uoga ama kutokuwa na elimu ya biashara hivyo ujenzi wa nyumba ya kupngisha haihitaji ujuzi tele kuweza isimamia..

ila nyumba ni uwekezaji poa sana ukiufanya kwa umakini.
usiitegemee pekee kiwe chanzo cha kipato chako kwani kwa hasa sisi wa kipato cha chini matunda yake utaanza yaona huko mbeleni..
hiyo 150m ukiiwekeza kwenye FDR,Bonds & Units naamni italeta return kubwa zaidi..ila ujenzi pia ni muhimu sana sana!

yote ya yote USIWE NA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO!!

Angalizo lako la mwisho nila kuzingatia
 
Waheshimiwa

Kuna jambo moja ambalo watu wengi wamekua wanalikosea bila kujua. Kwa maoni yangu:
Ni muhimu kuelewa tofauti kati ya business na investments
Ni muhimu kuzingatia suala la return on investment au Retun on Asset wakati wowote unapofanya investment au biashara. Usipozingatia haya utasema huna bahati au unalogwa. Utakua frasturated na kuchukia biashara. Mfano


Mimi na wewe tunaweza kuchukua mkopo wa million 100, tukafungua biashara tofauti. Wewe ukawa unapata faida kubwa kwa haraka kuliko mimi. Au Wewe unaweza kuanzisha biashara ambayo ni capital intensive mimi nikaanzisha biashara ambayo sio capital intensive (haihitaji mtaji mkubwa). Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye matumizi mengi / higher expenses kama daladala/ malori kuliko mimi. Au wewe unaweza ukafungua biashara yenye risk kubwa kuliko mimi kama vile daladala zinazopata ajali kila mara nk. Au wewe unaweza kufungua bishara yenye mzunguko mkubwa wa mauzo kuliko mimi. Yote haya yataamua nani atafanikiwa kuliko mwengine baina yetu

Wakati mwengine hata structure ya biashara inaweza kuamua nani anafanikiwa kuliko mwengine. mimi na wewe wote tunaweza kuanzisha biashara inayofanana lakini tukatofautiana katika structure ya management au operations na hapo mmoja akafanikiwa kuliko mwengine. Kwamfano wote tunaweza tukanunua bajaji kwa million 6 wewe ukaingia mkataba na dereva awe anakuletea kiasi fulani mpaka itakapofika million 10 then bajaji itakua yake. Mimi nikaweka dereva tu akawa analeta hesabu na hapo mmoja wetu akafanikiwa kuliko mwengine.

Wakati mwengine usimamizi tu unaweza kuleta tofauti kubwa sana. Wewe unaweza ukawa na Lori lako liko kijijini kwenu huko kaka zako wanasimamia na mimi nna Lori langu liko hapa Dar nasimamia mwenyewe au wote tunaweza kua na Fuso ziko dar lakini wewe ukapata dereva mwenye nidhamu mimi nikapata dereva asie mwaminifu na hapo tukapata matokeo tofauti kabisa

Tofauti hizi nyingi ndogo ndogo za kiufundi hua zinaleta matokeo tofautisana katika biashara na ni mambo ya kuzingatia kama unataka ufanikiwe kibiashara. ndio maana wewe unaweza ukawa na Daladala likakushinda ukauza mwenzako akanunua hioihilo akaa nalo miaka 10 ukabaki unashangaa

Kingine ni uvumilivu na kujifunza. Ukiwa na biashara na haiendi vizuri jitahidi kuvumilia na kujifunza na kurekebisha mapungufu yako katika biashara. Uyarekebishe na kuendelea. usiruke ruke na kuanzisha biashara mpya kila mwaka

Kingine Muhimu ni kuandika mapato na matumizi yote katika biashara yako ili baada ya mwaka au miaka 2 uweze kufanya tathimini na kuamua kama uendelee au la.

Mwisho nimalizie na mfano ulioko kwenye kichwa cha habari ya bandiko hili - case study. Nimekutana na rafiki zangu kama 4 ambao wanajilaumu kwa uamuzi wao wa kujenga nyumba na kuanza kukusanya kodi. Wamekuja kugundua baadae kua faida hua ni ndogo na inachukua muda mrefu sana kupata - inachukua zaidi ya miaka 20 kubreak even na kuanza kupata real profit. Yuko mmoja ameachiwa nyumba ya urithi na anasema anatamani angeweza kuuza na hizo fedha akaingiza kwenye biashara nyingine yenye high and quick return - familia haiwezi kumruhusu. Nyumba haimpi faida yoyote ya maana tena ni kubwa mno na wapangaji hamna. Yuko mwengine yeye alichukua mortgage kama million 200 pamoja na wife wakajenga nyumba. Wamekaa wamepiga hesabu na kugundua watakapomaliza kulipa baada ya miaka kama 15 watakua wamelipa kama million 400 kwa mbinde maana malipo ya mwezi ni zaid ya million 1 ambayo inawatesa sana kwasasa. Wanajilaumu. Kwamfano: ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00 kwa mwezi itachukua miaka 21 kuweza kukusanya kodi ya million 150. Kama unajenga nyumba ya kuishi ni sahihi lakini nyumba kama biashara it might be a challenge. Furthermore, kama una million 150 wapo wanaodhani unaweza kuiingiza kwenye biashara kisha ukatumia faida ya hiyo biashara kujenga nyumba polepole

Tupe maoni yako, tujadiliane, tubadilishane mawazo, tufundishane
Pamoja na andiko lako, niseme kwa ufupi tu kuwa - nyumba kama nyumba - hasa kama ni kwa matumizi ya kulala na kuishi humo ndani, HAS AND WILL NEVER BE AN ASSET. Hasa hasa kama unajua maana ya ASSET. NYUMBA YA KUISHI NI LIABILITY, yaani inakutoa fedha kila wakati ukitaka kufanya matengenezo, kulipa bili za maji au umeme na mambo kama hayo. Tujitahidi kujenga nyumba ziwe ASSETS. Siku moja tutaongelea nini maana ya ASSETS NA LIABILITIES katika maisha yetu ya kila siku.
 
Hivyo viwango ni vya mwaka mmoja. Mfano TZS 100,000,000 kwa 3% kwa muda wa miezi mitatu = 100,000,000 X 3% X3/12 = TZS 750,000 faida kwa hiyo miezi mitatu. TRA watachukuwa hapo 10% kodi ya zuio hivyo utalipwa TZS 675,000
TPB wanatoa 12.0% per annum. Ila nasikia wanataka sitisha Sasa.
 
Pia uwekezaji wa kodi unayoipata kwa kila mwaka ni njia nyingine inayoweza kumtoa mtu. Hiyo kodi ya laki 6, kwa mwaka ni sh mil 7.2. Ukipokea hii mil 7.2 unanunua nguruwe, au kuku au bajaj au chochote unaendelea kupata faida zaidi na zaidi.

Usiangalie ile kodi tu, angalia hiyo kodi inazalisha nini?

Pia baada ya miaka 20, hiyo bado nyumba itakuwepo hata kama itahitaji marekebisho madogo. Kwa kweli uwekezaji kwenye real estate ni mzuri sana

utakopa fedha bank, utapata kodi utalipia mko[po kidogo kidogo n.k

Ushauri: Jenga nyumba ndogo (nyumba 2, jiko dogo na kasebule mil 20 tu pangisha kwa lak 2.5, hutajutia kamwe.
 
Pamoja na andiko lako, niseme kwa ufupi tu kuwa - nyumba kama nyumba - hasa kama ni kwa matumizi ya kulala na kuishi humo ndani, HAS AND WILL NEVER BE AN ASSET. Hasa hasa kama unajua maana ya ASSET. NYUMBA YA KUISHI NI LIABILITY, yaani inakutoa fedha kila wakati ukitaka kufanya matengenezo, kulipa bili za maji au umeme na mambo kama hayo. Tujitahidi kujenga nyumba ziwe ASSETS. Siku moja tutaongelea nini maana ya ASSETS NA LIABILITIES katika maisha yetu ya kila siku.
Nyumba ni Asset bana hata kama ni ya kuishi. Kama ni liability si uigawe bure uondokane na hizo gharama ukapange?
 
Nyumba ni Asset bana. Kama ni liability si uigawe bure uondokane na hizo gharama?
Kwa ufupi tu, ASSET ni kile kitu kinachokuingizia PESA! Chochote kinachokuchulia PESA ni LIABILITY. Nyumba ya kuishi tu ni liability inachukua PESA in forms of kodi/malipo ya umeme, kodi ya ardhi, kodi ya jengo n.k. Lakini ka a umeipangisha, itakuletea PESA utakayotumia kulipia hizo bili. Hautatoa hiyo PESA kutoka kwenye aidha mshahara wako au vyanzo vingine vya mapato. Hiyo ni kwa ufupi tu.
 
Pia uwekezaji wa kodi unayoipata kwa kila mwaka ni njia nyingine inayoweza kumtoa mtu. Hiyo kodi ya laki 6, kwa mwaka ni sh mil 7.2. Ukipokea hii mil 7.2 unanunua nguruwe, au kuku au bajaj au chochote unaendelea kupata faida zaidi na zaidi.

Usiangalie ile kodi tu, angalia hiyo kodi inazalisha nini?

Pia baada ya miaka 20, hiyo bado nyumba itakuwepo hata kama itahitaji marekebisho madogo. Kwa kweli uwekezaji kwenye real estate ni mzuri sana

utakopa fedha bank, utapata kodi utalipia mko[po kidogo kidogo n.k

Ushauri: Jenga nyumba ndogo (nyumba 2, jiko dogo na kasebule mil 20 tu pangisha kwa lak 2.5, hutajutia kamwe.
Nyumba ya Mil 20 upangishe kwa Laki 2.5 kw mwezi labda kama imejengwa Posta au kkoo...!!
 
Pamoja na andiko lako, niseme kwa ufupi tu kuwa - nyumba kama nyumba - hasa kama ni kwa matumizi ya kulala na kuishi humo ndani, HAS AND WILL NEVER BE AN ASSET. Hasa hasa kama unajua maana ya ASSET. NYUMBA YA KUISHI NI LIABILITY, yaani inakutoa fedha kila wakati ukitaka kufanya matengenezo, kulipa bili za maji au umeme na mambo kama hayo. Tujitahidi kujenga nyumba ziwe ASSETS. Siku moja tutaongelea nini maana ya ASSETS NA LIABILITIES katika maisha yetu ya kila siku.
Naomba niulize swali mkuu....kua magari yale ambayo ni 'rare' sana kiasi cha kwamba yanauzika bei nuksi.
Je ni ASSET ama LIABILITY maana zinahitaji matunzo kama magari mengine lakini akija iuza ana uwezo wa kudabo au kutripo bei aliyonunulia?!
 
Mkuu uwekezaji kwenye nyumba ni moja ya uwekezaji wenye faida ya uhakika,biashara sio kila mtu anaweza kufanya na kila siku bei ya nyumba inapanda hata kwa hiyo dollar ya mmarekani ambayo dhamani yake iko stable
 
ASSETS ni kitu kinachokuingizia pesa/kipato mfukoni. Nyumba unayoishi wewe mwenyewe ni Liability coz haikuingizii kipato kwa muda huo ila ukiamua kuipangisha au kuuza inakuwa Asset coz itakuingizia kipato.

Na sio nyumba, mashamba nk na biashara ambao inakuingizia kipato kikubwa kuliko matumizi ni Assets.
Hapo kwenye bold ndo point yenyewe!
So ina maana nyumba ya kuishi si liability moja kwa moja na si asset moja kwa moja....inategemea na malengo & wakati husika si ndivyo
 
Hapo kwenye kodi ya nyumba kuna mambo 2
Kwanza hiyo kodi ya laki sita haitabakia hiyo hiyo itapanda kila mwaka
Pili nashauri uanzishe mradi mwingine mbali na hiyo nyumba hali ikiruhusu.
 
Hongera sana asee. Ukipiga hesabu mpk sasa hyo mil 30 yako haijarudi na faida kabisa
mnajidanganyaaa, Nyumba ya kupangisha inalipa sana, inategemea na eneo tu, mi nna Chumba sebule jiko, napangisha laki na nusu, na upande mwingine Ivyo Ivyo,

Yaan Nyumba moja ila ina pande mbili, kwaiyo nakusanya laki tatu kwa mwezi, na ya kawaida tu nje, ila ndani finishing nzuri,

Imenigharimu milioni 30,kujenga,
nimepaulia miti badala ya mbao za 4by 2..ila kwa upande wa 2by2 nimetumia mbao za Dawa, pia fishabodi mbao za dawa, mabati nimenunua ya gage 32 kwa Bei ya 16,000. Nimetumia bati sabini na tano tu, nyumba inalipa sana, ila usijenge kitajiri kama ni yakupangisha, na ikibidi mpaka mchanga nenda kanunue mwenyewe usimtume mtu, na misumari pia kanunue mwenyewe,

Yaan iyo million 150 mi najenga nyumba nne hapo za kodi ya laki tatu kwa mwezi,, ela Ya urithi niliifanyia jambo la maana nashukuru kwakweli
 
Wengi wanawekeza kwenye nyumba kwa sababu hawako tayari kuanzisha biashara zinazohitaji usimamizi makini...na mara nyingi wanaojenga nyumba za kupangisha fedha yake huwa hairudi.Nashauri kama unaweza kujenga nyumba ya kupangisha,ni bora ujenge lodge ndogo ya kisasa uwe unapata pesa kwa siku.
 
Ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00. Itakupa rental yield ya 4.8%, siyo nzuri saana, lakini haijambo.
Rental yield ya kuanzia 7% kwenda juu ni nzuri zaidi. Nyumba ni long-term investment. Wanaweza kuja kufaidi matunda watoto wako/wajukuu/vitukuu. Kila kitu ni timing. Hali ya real estate Tanzania kwa sasa ni tete sana.
Hiyo rental yield % unaipataje ndugu?
 
Naomba niulize swali mkuu....kua magari yale ambayo ni 'rare' sana kiasi cha kwamba yanauzika bei nuksi.
Je ni ASSET ama LIABILITY maana zinahitaji matunzo kama magari mengine lakini akija iuza ana uwezo wa kudabo au kutripo bei aliyonunulia?!
Hoja au kigezo au kipimo ni kuwa je hilo gari, pamoja na bei yake mbaya, linakuingizia PESA SASA?! Hiyo ndiyo THRESHOLD, kigezo au kipimo kwa sasa. Ukiliuza hapo baadaye na kukupa mahela mengi, hapo sasa ni ASSET. Kitu KINACHO KUINGIZIA PESA ndiyo ASSET. Vinginevyo ni LIABILITY!
 
Back
Top Bottom