mnajidanganyaaa, Nyumba ya kupangisha inalipa sana, inategemea na eneo tu, mi nna Chumba sebule jiko, napangisha laki na nusu, na upande mwingine Ivyo Ivyo,
Yaan Nyumba moja ila ina pande mbili, kwaiyo nakusanya laki tatu kwa mwezi, na ya kawaida tu nje, ila ndani finishing nzuri,
Imenigharimu milioni 30,kujenga,
nimepaulia miti badala ya mbao za 4by 2..ila kwa upande wa 2by2 nimetumia mbao za Dawa, pia fishabodi mbao za dawa, mabati nimenunua ya gage 32 kwa Bei ya 16,000. Nimetumia bati sabini na tano tu, nyumba inalipa sana, ila usijenge kitajiri kama ni yakupangisha, na ikibidi mpaka mchanga nenda kanunue mwenyewe usimtume mtu, na misumari pia kanunue mwenyewe,
Yaan iyo million 150 mi najenga nyumba nne hapo za kodi ya laki tatu kwa mwezi,, ela Ya urithi niliifanyia jambo la maana nashukuru kwakweli