Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

20.8333333333 miaka mpaka hela yako irudi na hapo kila kitu kiwe kizuri bila maintanance tc (which is next to impossible) Labda kama ulivyosema kuwa fadha ambazo huna kazi nazo...

Angalizo lako nila muhimu sana
 
Ni vizuri mtu ujenge mahala pakuishi kwanza then uje na ujenzi wa nyumba za kupangisha...na tena nyumba za kupangisha iwe ni unajega ghorofa hata floor mbili tu ili uanze kukusanya haraka kodi, pia nyumba za kupangisha kama upo eneo ni zuri usitumie gharama kubwaa kujenga maana itakuchukua muda kurejesha,
 
inategemea hiyo nyumba umeijengaje.. na umeijenga wapi...

kwa milioni 20 tu watu wanajenga nyumba na wanapangisha laki 5 .. hapo mchawi location tu..

Kwenye real estate ili upate faida unahitaji kuwa makini sana katika uchaguzi wa eneo na pia kama ni nyumba ya biashara basi angalia gharama za ujenzi na uzipunguze kadri uwezavyo. Sio maeneo yote yanalipa sawa.
 
Genius

Asante sana. Umetoa somo mubashara sana Chief.

Wengi sana wakichukua mikopo hufanya makosa kama ulivyoainisha hapo juu nakuishia kulia na kuhangaika. Sometimes mkopo hubadilika kua laana. Asilimia kubwa sana ya watu hawana elimu uliyotoa hapa - wengi sana
Kuna mmoja yeye ni dereva kwenye ubarozi wa nchi ya kibeberu flani. Amechukua mkopo milio 30,
Akanunua gari Subaru foresta nyingine akaanza kujengea saa hizi hiyo nyumba kaishia kupaua na hela naona imekata.
 
Ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00. Itakupa rental yield ya 4.8%, siyo nzuri saana, lakini haijambo.

Rental yield ya kuanzia 7% kwenda juu ni nzuri zaidi. Nyumba ni long-term investment. Wanaweza kuja kufaidi matunda watoto wako/wajukuu/vitukuu. Kila kitu ni timing. Hali ya real estate Tanzania kwa sasa ni tete sana.
 
Ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00. Itakupa rental yield ya 4.8%, siyo nzuri saana, lakini haijambo.
Rental yield ya kuanzia 7% kwenda juu ni nzuri zaidi. Nyumba ni long-term investment. Wanaweza kuja kufaidi matunda watoto wako/wajukuu/vitukuu. Kila kitu ni timing. Hali ya real estate Tanzania kwa sasa ni tete sana.

rental yield unaipata kwa formula gani??

mfano nikijenga nyumba kwa milion 20 nikapangisha kwa laki 4 kwa mwez.. rental yield ni ngapi?
 
Ngwanakilala,
Unaishi dunia gani nyumba ya TZS 150 M kwa laki 6? acha uongo,halafu thamani ya nyumba ni tofauti na lori,thamani ya nyumba inaongezeka wakati thamani ya magari inashuka,tatizo Watanzania wengi hatutaki kuwekeza ,tunataka tuanze biashara na faida hapohapo hatuangalii mbele au miaka 10 ijayo,halafu unajiita mfanyabiashara.
 
Ndachuwa, Mkuu naomba unielezee kwa Lugha Raisi, hapo! Nikitaka kuweka mpunga wangu kwa miezi mitatu faida inakua kiasi gani, hii chart hapa chini sijaielewa.
Screenshot_20190916-124749_Chrome.jpeg
 
Back
Top Bottom