Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Je, ni busara kujenga nyumba kwa milioni 150 kisha kukusanya kodi laki 6 kwa mwezi?

Ukijenga nyumba kwa million 150 na kuanza kukusanya kodi ya 600,00. Itakupa rental yield ya 4.8%, siyo nzuri saana, lakini haijambo.
Rental yield ya kuanzia 7% kwenda juu ni nzuri zaidi. Nyumba ni long-term investment. Wanaweza kuja kufaidi matunda watoto wako/wajukuu/vitukuu. Kila kitu ni timing. Hali ya real estate Tanzania kwa sasa ni tete sana.
... pamoja na somo zuri, sijamwelewa jamaa mleta mada! Hivi kwanini uwekeze 150 m/- kwa return ya 600k monthly? Kwanini kwa the same capital usiwekeze kwenye guest house/lodge ambayo chumba ni 30k daily? Ukiwa na vyumba 20 daily unapata 60k ambayo utaipata monthly kwa nyumba ya kuishi! Anyway, hata hivyo alishaonya kwamba ni muhimu kuwa proper plan otherwise gonna fail! Nimemwelewa.
 
**Nilikua nalipa nyumba laki 6 mwaka 2016 Mikocheni nimehamia Sinza kodi 250,000/= Tshs. Toka nimehama Mikocheni ile nyumba mpaka Leo haijapata mtu. Mwenye nyumba ananipigia simu nirudi atanipunguzia kodi 50% (300,000 Tshs.) Ha ha ha!
Nimeuza mpaka gari ili kuendana na kasi. In short nimekubali kuwa zama zimebadilika and I'm happy.**
 
Hiwezi kujenga nyumba ya milioni 150 ukapangisha kwa laki sita, kwa nyumba ya gharama hiyo bila shaka itakuwa ina units zaidi ya mbili
... kwa mtaji huo jenga g/house/lodge unapata 30k daily per room; ukiwa na vyumba 20 unapiga 600k daily kwa mwezi almost 18m/- kabla ya kutoa gharama za uendeshaji (mishahara, utilities, etc.). Lakini it is far better.
 
... pamoja na somo zuri, sijamwelewa jamaa mleta mada! Hivi kwanini uwekeze 150 m/- kwa return ya 600k monthly? Kwanini kwa the same capital usiwekeze kwenye guest house/lodge ambayo chumba ni 30k daily? Ukiwa na vyumba 20 daily unapata 60k ambayo utaipata monthly kwa nyumba ya kuishi! Anyway, hata hivyo alishaonya kwamba ni muhimu kuwa proper plan otherwise gonna fail! Nimemwelewa.
Gharama ya kuendesha guest umeziangalia? Utilities, kodi na kulipa wafanyakazi?
 
Nimenunua plot Dar miaka 5 iliyopita sijajenga hadi leo nimejaribu kuuza bei iko chini ya nilichonunulia
Nimewaza kujenga naona gharama kubwa sana na hela zangu hazitarudi
Mkuu umenunua plot maeneo gani? na bei uliyotaka kuuza ni ipi? ni PM jibu tafadhali maana naona niko kwenye situation kama yko kwa kiasi flani
 
Mkuu naomba unielezee kwa Lugha Raisi, hapo! Nikitaka kuweka mpunga wangu kwa miezi mitatu faida inakua kiasi gani, hii chart hapa chini sijaielewa.View attachment 1208896
Hivyo viwango ni vya mwaka mmoja. Mfano TZS 100,000,000 kwa 3% kwa muda wa miezi mitatu = 100,000,000 X 3% X3/12 = TZS 750,000 faida kwa hiyo miezi mitatu. TRA watachukuwa hapo 10% kodi ya zuio hivyo utalipwa TZS 675,000
 
Unaishi dunia gani nyumba ya TZS 150 M kwa laki 6? acha uongo,halafu thamani ya nyumba ni tofauti na lori,thamani ya nyumba inaongezeka wakati thamani ya magari inashuka,tatizo Watanzania wengi hatutaki kuwekeza ,tunataka tuanze biashara na faida hapohapo hatuangalii mbele au miaka 10 ijayo,halafu unajiita mfanyabiashara.
Sasa mkuu unabisha nini? Acha jaziba tulia ajadili nawenzako vizri wewe unajua nyumba iko sehemu gani?
 
... pamoja na somo zuri, sijamwelewa jamaa mleta mada! Hivi kwanini uwekeze 150 m/- kwa return ya 600k monthly? Kwanini kwa the same capital usiwekeze kwenye guest house/lodge ambayo chumba ni 30k daily? Ukiwa na vyumba 20 daily unapata 60k ambayo utaipata monthly kwa nyumba ya kuishi! Anyway, hata hivyo alishaonya kwamba ni muhimu kuwa proper plan otherwise gonna fail! Nimemwelewa.
Mkuu guest house si mpaka upate kiwanja maeneo ya mjini kitu ambacho si rahisi kihivyo. Guest nje ya mji kupata TZS 30,000 kwa kitanda bado ngumu'; labda Dodoma ambako mahitaji yanazidi idadi ya guest zilizopo kwa vipindi vya vikao vya Bunge
 
Nilikua nalipa nyumba laki 6 mwaka 2016 Mikocheni nimehamia Sinza kodi 250,000/= Tshs. Toka nimehama Mikocheni ile nyumba mpaka Leo haijapata mtu. Mwenye nyumba ananipigia simu nirudi atanipunguzia kodi 50% (300,000 Tshs.) Ha ha ha!
Hivi ni kipi kimesababisha ugumu kufika level hizi??

Ni sera za awamu hii ya tano tu au kuna kitu kingine??

Au ni watu kuhamia Dodoma??
 
Hivyo viwango ni vya mwaka mmoja. Mfano TZS 100,000,000 kwa 3% kwa muda wa miezi mitatu = 100,000,000 X 3% X3/12 = TZS 750,000 faida kwa hiyo miezi mitatu. TRA watachukuwa hapo 10% kodi ya zuio hivyo utalipwa TZS 675,000
Basi kama hivi nadhani mkuu Biashara ya fixed deposit inahitaji mtaji mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom